The suffering African Muzungu wives...

 Najua ulikuwa unakuja humu mara kwa mara kuangalia kama nimepost kuhusu  Wake wa Wazungu ambao ni waafrika(maana visits vimekuwa mingi mno), The suffering Wives of Afrikan husbands zimekupita, zisome hapa sema nimegundua kuwa nikiwa naweka post bila kanuni nakuwa na-miss blog yangu, kama hivi nakuja nachapa takataka zangu,  hivi kuna AI ya Kiswahili? maana hiyo biashara ya kuandika blog kwa kutumia Chatgpt(sijui inaitwaje) inakatisha tamaa. Achana na hili, endelea na topic iliyokuleta humu.


Changamoto za wake(waafrika) wa wazungu  ni nyingi ila binafsi sina uzoefu kwasababu wengi huwa wasiri sana na wakifunguka huwa hawasemi ukweli, so yafuatayo ni yale machache niliyosoma, sikia/ona youtube  hivyo ninagusia juu kwa juu na kuchomekea nini cha kufanya kwako wewe mpya ambae unataka ukawe Mume ya Muzungu; 


-Moja ni kuolewa na Mwanaume ambae unadhani ni wa kariba fulani, kisha ukienda kuishi nae huko kwao, unagundua anaishi maisha ya kawaida sana pengine ni chini zaidi kuliko maisha uliyoishi Tz au popote Afrika utokako.


Wazungu wanaokuja Afrika(nitaegemea Tz), wengi huja kwa ajili ya kutalii kingono, wachache kukuza profiles ili kupata ajira za juu iwe Serikalini nchini kwao au Umoja wa Mataifa/Ulaya na Nchi nyingine zilizoendelea, kupata Miakataba sekta ya Madini/Utalii, bila kusahau kupata ngazi ya juu kwenye NGo's za kusaidia watu Afrika(kupata donation kwa kutumia video/picha za umasikini uliopitiliza).


Unless unamipango mingine na nia yako ni kuingia tu Ulaya kisha ufanye mambo mengine(jilinde usishike mimba), ila kama unapanga kuja kuishi nae ili kubadilisha life yako iwe ya maana hakikisha unafanya uchunguzi, je anafanya kazi? Elimu yake, Wazazi na ndugu zake wanamsimamo gani kisiasa, wanaichukuliaje Africa na watu wake? Je ana Kesi au amewahi kuwa na Kesi/mikiki na Polisi? anaishi wapi(eneo)? na pia usisahau kuzijua Sheria za Nchi yake ka' kuona inakulindaje wewe kama Mhamiaji, hasa ukiwa umezaa na Mzungu wako(hasa Ufini, Uholanzi, Norwe,Ugiriki na nchi zote za Scandanavia)hayo yote na zaidi yanapatikana kirahisi tu Online.


Sio unakuja Ulaya kuboresha maisha yako halafu mkibaba anakupokea yapoti(Airport), kisha mnaenda chukua Basi hatua ndeefu(nusu saa), unafika kwake unakuta ni bedsit sio nyumba...baada ya mwezi anakuambia tafuta kazi ili umsaidie kulipia Kodi ya nyumba na bills nyingine wakati wewe ni mwanamke na mgeni nchini kwake...Hii ni true stori ya mdada wa kikenya niliona last year on Youtube hihihihihi, mkenya yule alinikosha, Pili.


Picha from KentOnline.


Tatu,wake waafrika wa wazungu kutoka Nchi za Scandavia wengi huwa wana dhurumiwa watoto(sina hakika kama kuna Sheria inawapendelea Wazungu wabaki na watoto) maana kuna kesi nyingi sana za Wanawake wa kiafrika kunyang'anywa watoto na kurudishwa kwao(Afrika), Russia na nchi nyingine za Ulaya Mashariki wanakuacha na watoto wako(Ubaguzi bado ni wa hali ya juu halafu wanabenda kuonea wake zao, so hata kama wanao ni nusu kwa nusu, bado life itakuwa ngumu kwao na mkiachana Dingi anaona  bora uende na wanao ili asibaki na doa).


Nne, Mke ya mwafrika wa Muzungu anafanya kila aina ya ngono kwasababu huna uzoefu wala mipaka na pengine ni mpenzi wa picha za X (formally known as twitter...natania hihihihi) unadhani kuwa anayajua mapenzi kuliko Bwana Rashidi Kimweri Prince wa Tabata, kumbe yote anayoyafanya/kukufanyia ni kwasababu ya asili/rangi yako....kumbuka kwasababu  tu kakuoa na  anaishi na wewe haina maana kuwa sio Mbaguzi. Jielimishe  ujue tofauti na hakikisha unashiriki kwasbabu unataka, upo comfortablr na sio kulazimishwa.


Tano, Inasemekana ukiachana na hao niliwataja hapo awali, kuna wale huwaga baridi aka plain mno to the point inabidi Mke ya muzungu atafute motomoto ya Afrika, maana Waafrika wajua sugua to create faya(sababu hawapendi BDSM? ewww),,,,ewww to BDSM not Faya, I love and live for the  fire fire.


                                  
                                                   Moscow, pic kutoka Gugo.

Sina hakika kama bado Waafrika wanaamini kuwa wazungu ni "wakombozi", yaani ukitoka na hatimae kuolewa na mzungu  ujue umefanikiwa, kwamba utapendwa, utapewa kila ukitakacho and much more....wanasahau kuwa Wazungu ni binadamu kama waafrika na tofauti ni utamaduni, malezi, pengine Siasa na mazingira. Kuna wema, wanyanyasaji, washenzi, wakatili na wanaharamu n.k.


Natambua kuwa penzi halichagui, likikufika unadondokea huyo mwafulani iwe ni Muzungu au Muafrika, pamoja na kusema hivyo usiende na Muzugu kwasababu ni bora kuliko Kimweri Prince of Tabata. Nenda sababu umekufa umeoza ila usisahau kutumia akili, kuchunguza as you go na wekeza(kiuchumi). Kumbuka as mgeni(kama huna karatasi za ukazi wa kudumu), huna kinga nyingi kisheria kwenye nchi ya Muzungu wako.

Bbai.

Comments