Mume wangu ni Shoga?(repost from 2014)

 Habari dada Dinah, hongera sana kwa kazi yako nzuri mno! nimekuwa nikisoma Blog yako siku zote na kuifurahia sana. Leo nami naomba ushauri dada yangu.Mimi ni mama wa watoto watatu, nimefunga ndoa ya Kikatoliki mwaka wa 11 sasa. Siku zote tumeishi vizuri na Mume wangu, makwaruzano ndani ya Ndoa hayakosekani ila siku hizi Mume wangu amebadilika sana kiasi cha kunifanya nipate mawazo mabaya juu yake.


Hakuwa na kawaida ya kujipulizia perfume ila ghafla ameanza kijipulizia hadi sehemu za siri!!Inaniogopesha sana. Anatumia muda mwingi kwenye kioo! anavaa Macheni na Mapete makubwa makubwa! Nimejaribu kumuuliza sababu ya kufanya hivyo kawa mkali kama pilipili.


Dada yangu inawezekana akawa amejitumbukiza kwenye masuala ya Ushoga? Na mwanaume akiwa Shoga anaweza ngonoka na Mkewe kama kawaida? nifanyeje kukomesha tabia hii ambayo inaninyima raha katika Ndoa yangu?


Pole kwa maswali marefu naomba unisaidie dada-Asante(tafadhali hifadhi jina langu).

**********


Dinah anasema: Habari ni njema, ahsante sana kwa ushirikiano.


Ulivyo-panic umenifanya nicheke ghafla!....Miaka 11 ni mingi kiasi. Je mnampeana attention ya kutosha kama wapenzi au mnamchukuliana kama Wazazi tu? Mumeo ana umri gani kwani? Maana kuna baadhi ya wanaume wakifikia umri fulani 49+ huwa wanabadilika ghafla.


Kuna Makala moja ya Uchunguzi nilisoma mwaka jana wakazungumzia hilo na hitimisho lao lilikuwa sio Ushoga bali Mwanaume kuelekea kwenye "kikomo cha Hedhi" usishituke, sina neno lingine la kiswahili la "Menopause". Mie nikabisha(as usual) kwa kusema kuwa mbona wanaume hawana Hedhi sasa "kikomo" kinaibukia wapi? Mpaka leo sijui na sikufuatilia tena.


Kuna umri fulani hufikia na watu kutamani au kutaka kujiamini tena kama walivyokuwa enzi zile kabla ya Ndoa na watoto, kwasababu walikuwa busy sana na majukumu ya "uzazi" sasa watoto wamekua na wao wanaamua kufurahia maisha yao.


Sasa mume wako kaamua kubadili Mtindo wa mavazi.....wengine huamua kufunga ndoa na mabinti wadogo, wengine kupunguza mwili, kurudi shule, kukimbia familia na kununua magari/pikipiki n.k ili kujiongozea hali ya kujiamini. Mumeo ama hataki kuzeeka, kachoka kuonekana vilevile kwa miaka yote 11 au ame-miss attention aliyokuwa akiipata alipokuwa Kijana hivyo akivaa anavyovaa anazipata au alitegemea kupata....mf: wewe mwenyewe unampa attention japo sio nzuri (aliyotegemea ndio maana akawa mkali).


Nadhani ni vema kubadilisha uulizaji wako....badala ya kumkalipia, kumuita Shoga au kumkataza asivae anavyovaa kwavile anaonekana Fala. Pia ni vema kujipanga kwenye suala la Mavazi ambayo unadhani yatampa akitakacho lakini atapendeza na kutavutia kuliko sasa.


...mwambie kwa upole na kujali, "Mume wangu najua unapenda kuvaa unavyovaa, lakini uvaaji huo wala hauendani na wewe,.....jaribu kuvaa hivi".....onyesha mavazi ambayo unadhani yatamfanya Mumeo aonekane kijana na kuvutia na sio "Pimp"....Mvishe Mumeo.


Ushoga sio kitu/tabia za kujiingiza bali ni "ujinsia" ambao mtu anakuwa nao....kwamba anavutiwa na watu wa jinsia yake kingono/mapenzi. Inategemea na jamii inayomzunguuka au "utayari" wake kuishi kama Shoga....wengi huishia kuoa na kuzaa ili kuficha "Ujinsia"....nikijibu swali lako ni kuwa sio lazima Shoga ashindwe kufanya Ngono/Mapenzi na Mkewe, anaweza kukufanya vema tu na akatoka akaenda fanywa/mfanya na mwanaume mwenzio vizuri. 


Mashoga huwa hawavai kama ulivyoelezea, Pimps ndio huvaa hivyo. Suala la kujipulizia Manukato sio tatizo, katika kujipenda na kujijali kunukia nayo imo!


Ila kujipulizia Manukato sirini mwambie aache kwani Manukato yana "alcohol" ambayo hukausha ngozi na hata kusabbaisha muwasho na maambukizi mengine ya Ngozi kutokana na joto la mahali huko(sirini), pia inabadilisha balance asilia ya ngonzi(PH) ambayo ikisumbuliwa inasababisha maambukizo kama nilivyogusia hapo awali.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments