Thursday, 12 March 2015

Kanisaliti na kuzaa x2 na vibaba 2 tofauti....ataka tufunge Ndoa


Habari za siku nyingi Dada mpendwa. Natumaini Mungu bado anakulinda. Na afya yako inazidi imarika kwa neema ya Mungu.

Dada mpendwa mimi niko katika hali ya sintofahamu, naamini kwako ntapata uvumbuzi.

Miaka ya nyuma nilikuwa naishi Bujumbura, nikaanza kupendana na Binti flani. Kwa vile nilikuwa na soma  ilinibidi nitoke kidogo ili kujianda kwa ajili ya Mtihani mkuu.  Nilipo rudi nikakuta yule Binti ana Mimba ya mwanaume mwingine!

Tangu apo mawasiliano yakakoma. Alipo jifunguwa baadaye  akaniomba msamaha nakuhitaji turudiliane tena, nikamsamehe nakurudiliana naye kimapenzi!

Baada ya muda Binti uyo akaitwa na kakaye huko Afrika ya kusini(South Africa) ili aende kusoma na kuniacha Bujumbura!

Alivyofika huko mawasiliano yetu yakaendelea lakini baada ya muda yakazimika kwamba simu yake ikawa haipatikani!


Jinsi muda ulivyokuwa unakwenda na mimi nikajaaliwa kwenda Africa ya Kusini(South Africa). Siku moja nilipokea simu ya yule mwana dada niliyekuwa napendana naye bila kujuwa amepata wapi namba yangu ya Simu!


Huku akiniomba turudiane tena wakati alishazaa mtoto mwingine na mwanaume mwingine Afrika ya Kusini(South Africa)!
Na amewahi ishi na huyo Baba mtoto kama mumewe. Ila kwa bahati mbaya hawakuweza elewana wakaachana.

Mimi binafsi sikuwa namfikiria tena na nilikuwa tayari nilisha pendana na Binti mwinhine ambaye nilikuwa na tarajia kuowa tangu nilipofika Afrika ya Kusini(South Africa). Ila bahati mbaya huyo Binti nilie tarajia kuowa naye kaniotea meno ya juu na mapenzi ya mimi naye yakaisha!

Kwavile nilikuwa katika mahitaji ya kuowa ukizingatia nilie tarajia kuoana naye kaniotea meno ya juu, basi nilikuwa sina jinsi, nilikubali kumsamehe nakurudiliana na yule mpenzi wangu wa zamani ambaye kwa sasa ana watoto wa wili.

Mwana dada huyo ameniomba tuwe mke na mume (tuowane) tusameheane na kusahau yalio pita. 

Kwa kweli na mimi najihisi kumpenda, licha ya disappointments. Pia amekubali kunisaidia katika mpango wangu wakusoma kwavile yeye anafanya byashara na anauwezo kunizidi.

Sasa mimi nina wasiwasi  kwa sababu amesha nisaliti mara mbili na kuzaa watoto wawili na wanaume tofauti! Huwa nahisi huenda akajakunisaliti tena baada ya kumpa moyo wangu na kumchukua kama mke wangu.

Kwa kweli Dada mpendwa  nahisi kumpenda nakuwa tayari kumuowa huyo mwana dada licha ya disappointments zilizo tokea  na watoto wawili anao sasa!

Ila nazungumuza na nafsi yangu ya kwamba nisisubutu kumkabidhi moyo wangu hadi pale ntakapo ona mapenzi ya dhati kwake.

Mimi sina mtoto wala sijawahi kucheat. Dada mpendwa je ni busara kwangu kuowa huyo mwana dada?

Nini hasa kinaweza nipata kwa siku za usoni? Tafadhali Dada yangu mpendwa naitaji ushauri kwa hali na mali ili nisije kujutia baadaye. Asante kwa msaada wako Mungu akujali.

*********

Dinah anasema: Ni njema kabisa kaka Mpendwa, ahsante kwa ushirikiano.

Huyo mkimama ni mapepe. Sio mwanamke wa kuishi nae kwa kumuamini kama mkeo sio tu kwa vile anawatoto wawili bali jinsi alivyowapata hao watoto wake.


Mara zote anakuterekeza halafu anaenda na mkibaba mwingine na kuzaa.....logically unadhani anafaa kuwa mkeo?Mke/Mume ni mshiriki wako wa kudumu anaepaswa kukuoenda, kukuheshimu na kukuthamini, kuku-support na kukushauri sio kukimbi kwa wanaume/ wanawake wengine kila unapokuwa mbali au kila likapotokea tatizo.Anatumia "mali" ili akupate kirahisi.....anajua unahitaji la kusimama huko SA pia anajua unahitaji la kuoa baada ya kutolea nje last minute na Moyo wako bado haujapona vema hivyo Kisaikolojia na Kihisia haupo sawa.


Hali hiyo inaweza kukufanya uingie kwenye ndoa au uhusiano ili kujirudishia ile hali ya kujiamini tena baada ya kuachwa. Hali ya kuhisi kuwa unapendwa baada ya uliempenda kuingia mtini.Ukiachilia mbali hali yako Kihisia na Kisaikolojia.....je ni kweli kabisaaaaa upo tayari kuishi ukiwa unasikia kuhusu Exes na kuona (watoto) wao waliozaliwa baada ya huyo mkimama kukusaliti?


Ingeleta unafuu kwa mbali kama aliwazaa hao watoto kabla hamjakutana japo sio rahisi kuishi na mtu ambae ex zake wanahusika kwenye mahusiano na maamuzi yenu kwenye maisha yenu yote yaliyobaki.Mf: Ex kamuudhi mkeo kutokana na mtoto wao.....mkeo anakununia au kukufokea wewe na mengine mengi.....trust me ni mzigo.


Fact of life(usinihukumu Maisha magumu bana): Sasa kama upo Single Kaka yangu na unahitaji msaada alioku-offer chukua lakini hakikisha humpi Mimba na wala hakutegeshei kushika Mimba na usionyeshe kuwa unataka sana mtoto(jifanye 2 alionao wanatosha) na kubwa lao USIFUNGE NAE NDOA.


Jiwekee mipango inayokwenda na muda kwamba ndani ya  miaka miwili nitakuwa nimemaliza Masomo au nimesimama Kibiashara (hakikisha haimuhisishi yeye) Ukikamilisha mipango yako achana nae.


Ni vema kumwambia ukweli kuwa 2 kids ni hell of Mzingo na huwezi kuwa wanakupa kumbukumbu mbaya kila ukifikiria walivyopatikana.Atakulaumu umemtumia nakadhalika.....ungekuwa kwenye Uhusiano ningekushauri vinginevyo.

Kila la kheri.

1 comment:

Mille Moyens said...

Dada mpendwa dinah, nakushukuru sana tena sana, sijuwi nidhibitishe namna gani shukurani zangu kwako! Umekuwa mwokozi wangu kuhusiana na hili Changamoto! Mwenyezi Mungu azidi kuku ongezea Hekima na Busara zake ili uzidi kuudumia watu wake daima. Ubarikiwe Dada