Thursday, 19 March 2015

Dinahicious inakwenda PRIVATE...

Herooooo!

Dinahicious sio public transport tena  hihihihihi.....i mean Blog kuanzia Tarehe 23 Machi 2015.


Tangu kubadilika kwa maisha yangu nimekuwa mvivu....well sio mvivu bali priorities zimebadilika na blog is the last thing nafikiria(sio muhimu).Nimekuwa nikijisukuma huku watu wengine kutishia kuiiba Blog aka kui-teka hihihihi wakidhani Dinahicious Blog inalipa. Ningetaka mahela ningetoa masomo na ushauri via 0845 au 0900 numbers (£1to £3 per minute).....sio matangazo ya Google.Back to the point. Kutokana na mabadiliko ya Kisheria Google imeamua kuwa Blog zote zenye masuala ya Kingono na kwa uwazi ni vema ziwe Private.Google wametoa option 2. Moja ni kuweka onyo kuwa ingia only kama unamiaka 18 au kufuta topic zote zenye ungono kwa uwazi......ukishindwa basi wanaifanya Blog kuwa private.Ikiwa unataka kuendele kuiona Dinahicious kipembeni aka private aka kwa Usiri itakubidi ujiandikishe na uwe followe wa Blog husika.


Kwa miaka 7 topic ni nyingi mno na sina muda wa kuziondoa zote so nimezificha baadhi kama Mia Nne hivi nikachoka. Hata hivyo sitaki tena kuandika kuhusu Malavidavi na kungonoana miaka SABAAAA inatosha kwakweli....hata kama ni Ajira ningekuwa nimepanda Cheo au kuhama eneo.


Anyway....endelea kuwa nami kwenye blog ile nyingine http//www.Kilakitumie.blogspot.com ambayo ina mambo mchanganyiko ambayo hayahitaji matumizi ya akili kufikiria au kuandika ktk mtindo wa kufundisha ili nieleweke hali inayofanya niandike nikiwa popote au wakati naangalia Tv oh pia hakuna Siasa.....just life.


Walionitumia maswali wiki iliyopita na wiki hii nitawajibu moja kaa moja via emails zenu. Sitojibu email yeyote itakayoingia leo na kuendelea.Ahsanteni wooote kwa Ushirikiano....Uaminifu wenu kwa Blog hii kwa Miaka yote Saba na ushehe.

Kila la kheri kwako.

Mapendo tele.

5 comments:

Anonymous said...

Nitaikosa sana hii blog. Mwenyezi Mungu aendelee kukubariki kwa kujitolea muda wako kwa miaka yote hiyo.

Anonymous said...

Asante kwa kuwepo miaka yote hiyo. Mola aendelee kubariki familia yako.

Anonymous said...

Thanks Dinah. Mimi mwenyewe nimefaidi blog hii kwa kweli umefanya kazi njema ndani ya hiyo miaka 7. Nikweli inavunja moyo mimi mwenyewe nimeshuhudia kwenye mitandao ya kijamii wakicopy and paste your topics. For sure inajunja moyo sana. Ni vema ungeendelea kutupa room ya kuwasiliana kwa email ili kutusaidia wahanga wa mahusiano. Mie nikupongeze na Mungu akutunze.

Mille Moyens said...

Dada mpendwa nimatumaini yangu humzima wa afya.
Nimetaka kuelewa kuwa private inakuwa na maana gani hasa, ndo itafanywaje? Kama nimekuelewa vizuri dada inamaana tusisubutu kukuandikia mazwali tena kwenye hii apa?

Kwaupande wangu ntasikitika kukukosa manake ndonilikuwa naanza sasa nufaika kwavile bado mgeni kwenye dinahicious.

Licha yakwamba unastahili shukrani zisizo weza kutamkwa, na pongezi zisizo weza kuwa na kipimo kwa kazi unayo fanya; Siwezi kosa ku express my regret kama ndo mwisho wakuwa nawe kwenye Dinahicious!

Nakama ndo mtu atakuwa na matatizo ya uusiano utawezaje kumusaidia? Kwa kweli nasikitika kwani hii abari sio nzuri kwangu hata kidongo! Tafadhali Dada yangu mpendwa, ni fafanulie ili nielewe nini lakufanya ntakapo itaji msaada wako pale ntakapokuwa na swali. Mungu Akubariki, Akulinde, Akuneemishe, Akuwekee wepesi, Akuinuwe zaidi na zaidi amina.

Anonymous said...

Ubarikiwe dada.ulichokuwa ukikifanya ni cha mno zaidi.wengi tumejifunza na tunaamini siku moja utaamua kutengeneza hamasisho lingine iwe ni kwa email au popote.usijali na changamoto,let me be the first one to encourage you here from kenya,YOUR REWARD IS IN HEAVEN.May God bless anythng you do.SUCCESS!