Monday, 23 February 2015

Nilitaka pasipo....

Hello Dinah,

Shaka message hii itakufikia ukiwa salama wa salimini. Napenda nitangulize samahani kwa kuchukua muda wako, lakini pia naomba unipe nafasi ya kusikiliza tatizo langu ambalo nina imani utanisaidia ki ushauri!.


Ni tatizo ambalo lilinitokea miaka 28 iliyopita ingawa kwa wakati huo kulikuwa na sababu ya msingi kiasilia na likapita kwa kuwa liliendana na wakati wake!.Mimi ni kijana wa miaka 39, nimeoa na nina watoto 3. Mimi na mke wangu tuna miaka 15 ya ndoa sasa. Wakati wa ujana wangu kabla sijaoa nilikuwa na vigezo fulani vya nje na ndani kwa mwanamke ninapenda kuoa.
Lakini pia nikajiwekea nadhiri kuwa kama nitampatia mimba mwanamke wa ujana wangu sina budi kumuoa kwa kuwa kama nimeridhika kushiriki naye tendo la ndoa nimempenda!.
Nikija kwenye tatizo nililogusia hapo juu. Wakati nabalehe nilipatwa na ugonjwa wa kupenda kama sio kutamani iliyonipelekea kujihisi naumwa homa, kukosa hamu ya kula huku nikihisi njaa sana.Tatizo hili nilipoendelea kukua lilitoweka.Sasa ni hivi karibuni nilipokutana na mwanamke mmoja(mke wa mtu)ambaye kwa macho yangu ana vigezo vyote vya nje nilivyokuwa nimejiwekea ujanani!.  Nilihisi mapigo kwenda kasi lakini nikaamua kuuchuna.
Tulipokuwa kwenye mazungumzo ya kawaida tulibadilishana namba za simu, kumbe naye alikuwa amepatwa na yale yaliyo nipata wakati tunaonana kwa mara ya kwanza.Baada ya muda fulani tulianzisha uhusiano wa kimapenzi wa siri, mapezi yetu haya tumekuwa tukiyafurahia ajabu tunapokuta.


Sasa mimi nimekuwa nikijiuliza kwa nini napatwa na hii hali ya kama vile ndio nina balehe!? Yaani kukosa hamu ya kula nisipo muona kwa siku kadhaa, kujisikia kuumwa, kumfikiria sana nk.Hali hii inaniathiri hata kushindwa kuchangamka na watoto wangu kama kawaida. Hii hali nitaishinda vipi wakati nipo katikati ya bahari siwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma? Nisaidie dada Dinah tafadhari.

Nategemea kusikia machache kutoka kwako ni mimi. KPM


***********

Dinah anasema:  Hello.....bila ya samahani. Ahsante kwa ushirikiano.

Hehehehe nahisi unaogopa Uzee. Miaka 40 sio uzee mwenyewe naisujiria kwa hamu hapa.(still nina hasira na wewe kwa kuumiza watoto).


Inasemekana kuwa watu wakikaribia kufika miaka 40 huanza kujisikia kama walivyokuwa na miaka 20.....mwili unataka kizunguuko mingi ambayo pengine mke hawezi kuitoa kwasababu ama yupo busy na watoto au anajihisi kuwa kungonoka sio muhimu tena bali future ya watoto in your case mnao 3.Bila kuwa wazi kwa mkeo kuhusu hisia zako ni wazi utaishia kutafuta mbadala ili kutimiza haja zako. Sasa suburi mkeo afikie hapo ulipo ndio utakapojua tamu ya chungu.Sio kila mtu anajua suala hili la miaka 40.....baadhi  huamini kuwa wanapepo lakini ni mabadiliko tu ya kibaiolojia.Kufanya ngono na kusababisha Mimba which ndio sababu kuu ya kungokoka sio mapenzi na haimaajishi kupenda. Ulijidanganya na matokeo yake umeleta watoto 3 Duniani ili wateseke......wakose mapenzi ya Baba kwa sababu nafasi yao imechukuliwa na hawara ambae ni mke wa mty.


.....ulitakiwa kujua kosa lako kabla ya kupoteza muda wa mkeo kwa miaka 15 na kukongoroa mwili wake kwa kukuzalia watoto 3.  Vilevile kama kweli ulijua mama wa watoto wako 3 sio "type" yako hukupaswa kuendelea kuzaa past mtoto mmoja.Cheating haina excuses....na excuse yako hapa hainifanyi nikuonee huruma wala kukuelewa. Huyo mwanamke unaetoka nae ni mke wa mtu ni wazi kuwa ni Malaya na hana heshima kwenye ndoa yake kama wewe.

Since unaonyesha kutokutaka kuendelea na huyo mwanamke ni wazi umegundua value ya familia yako.


Kumbuka kuwa wewe upo kwenye control. Ulienda mwenyewe kwa huyo mwanamke.....hakukushika shati na kukuvuta so jirudishie control hiyo na acha Uzinzi.


Ukiendelea kufanya siri ni wazi kuwa utaendelea na cheating. So ni vema kumueleza mkeo ulichokifanya ili aache kukuamini hali itakayokusaidia kwani atakuwa akikufuatilia......kabla hujamwambia soma hapo chini. Ukishamsogeza karibu ndio umwambie ili kuepuka uwezekano wa kukutaliki.Unakaribia umri wa miaka 40.....wanao 3 wanakuhitaji zaidi kuliko huyo mkimama.  Jiulize ni legacy gani utawaachia wanao?Update uhusiajo wenu kila mwaka ili moto uendelee.....weka effort kwenye ndoa yako na uanze kustarehe na mkeo.


Kama sio kawaida yako mkeo atashtuka....mueleze unavyojisikia na pamoja msaidiane. Hali hiyo itakyishia by the time umegonga 40 au 42. So imagine kupoteza familia yako ya miaka 15 kwa ajili ya hisia za miaka 2.


Kapime HIV.....ilinde familia yako....ipende....itukuze.

1 comment:

Anonymous said...

Kumbe! sikujua umri huo ukifika inakuwa hivi. Ahsante kwa somo, bila shaka mwenye tatizo amekuelewa