Tuesday, 10 February 2015

Mume mlevi na anakisukari....

Da Dinah pole sana na majukumu ya kusaidia shida za watu mbalimbali. Mimi ni mpenzi sana wa blog yako.Ni mama wa mtoto mmoja nilifunga ndoa miaka sita iliyopita na Elimu ya chuo ila bado sijaajiriwa nafanya ujasiliamali.Miaka minne iliyopita tuliishi maisha ya furaha sana na mume wangu, tulikuwa watu wenye hofu ya Mungu.


Ikatokea mume wangu akaamishwa kazi kutoka tulipokuwa tunaishi so tukakaa mbali mbali kwa mda wa miaka miwili. Ndani ya mda huo mume wangu akaanza kuwa mlevi na mvutaji wa sigara kupita kiasi.Hata akija nyumbani kusalimia hurudi saa tisa usiku akiwa chakari na kuanza kunitukana.


Alianza kujiskia vibaya kiafya na baada ya kwenda kupima akakutwa na sukari na akazuiliwa kunywa na kuvuta.


Kwa sasa nimemfuata tuko pamoja ila tabia yake inaniumiza sana ya kuchelewa kurudi nyumbani na akiwa amelewa na kuvuta sana sigara.Nimekuwa sio mtu wa furaha tena kila siku ni stress na pia anawivu sana kiasi kwamba ananihisi vibaya wakati yeye ndio alikuwa mwanaume wangu wa kwanza na sijawahi kumsaliti hata siku moja.Mara nyingine nawaza sijui niondoke maana sioni tena raha ya mapenzi da Dinah please nahitaji msaada nifanyeje maana anaahidi kuacha ila kila siku kasi inaongezeka.

*************

Dinah anasema: Ahsante mrembo na shukurani sana kwa ushirikiano.

Unajua binadamu hupenda ku-adopt mazingira mageni ili kuweza ku-fit in.....hii tuwatokea watu wengi tu hata mimi ni mmoja wao ila tofauti ni kwamba ninajijua so huwa natulia na kujikumbusha mimi ni nani na sihitaji ku fit  in bali kuwa mimi as an individual.Wengine huanza ulevi kama mumeo, baadhi huibua tambia za ajabu ajabu au za kitoto, wengi huamua kuacha familia zao na kuanza maisha upya (wakipandishwa vyeo) na wachache hutumia pesa kiholela.


Nahisi kuwa mumeo alikuwa akipata shida kuwa mbali na familia yake akakutana na wafanyakazi wenzake wenye tabia aliyoi-adopt na akaizoea na mazoea yakajenga tabia.


Kumbuka mumeo hakuwa na mahali pa kwenda baada ya kazi kama alivyozoea kabla ya kuhamishwa.....kwani alikuwa anarudi kwako mkewe na mtoto, huko mbali ilimuia vigumu....nadhani.


Sitetei ulevi wake ila najaribu kukufanya uelewe kuwa huenda uhamisho na upweke umepelekea  awe na tabia aliuonayo.Baada ya kugundulika kuwa anakisukari na hataki kufuata ushauri aa Daktari  wa kuacha pombe na sigara ni wazi kuwa anataka kufa kabla ya wakati wake(anajiua).


Kabla hajafa kuna matatizo mengine ambayo yatabadilisha maisha yenu kutokana na  ugonjwa wake huo na bila kuwa na mke supportive hakika maisha yatakuwa magumu.Tafuta muda uzungumze kwa hisia na mumeo (akiwa hajalewa)na kuweka wazi hofu yako juu ya Ugonjwa wake na tabia yake ya kurudi usiku wa manane akiwa chakari.Kisha mpige mkwara......mwambie wazi kuwa kama mkewe unalojukumu la kuhakikisha anakula vizuri na anafuata masharti ya Daktari ili kuweza kuepuka madhara makuu ya Kisukari.


Ongeza.... Lakini unanikatisha tamaa na nisingependa kuanza kuuguza au kuwa mjane ningali kijana kwa sababu za kujitakia.
Endelea, imefikia mahali nahisi pombe au unaokunywa nao ni muhimu kwako kuliko mimi na mwanetu.....unatumia muda mwingi na wao ukiwa huna pombe.....ukirudi nyumbani unapombe kichwani!Sikutambui tena kwani mume wangu hakuwa hivi.....mume wangu hakuwa mlevi na mume wangu hakuwa akirudi nyumbani kesho yake......nimemkumbuka mume wangu namtaka mume wangu!(toa na machozi hapa....lia haswa).Usipo acha pombe na kubadilisha tabia na kurudi kuwa mume wangu niliyekupenda bila pombe basi nitabeba mwanangu na nitaondoka nikuache ujifie peke yako. Nakupa wiki ubadilike.Mumeo anahitaji support kutokana na Kisukari chake....sio big deal ila watu tunapokea magonjwa ya kudumu tofauti  hivyo basi wakati umempa Mkwara na muda anza kuonyesha support ya Kisukari chake kwenye lishe unayomtayarishia.


Mkumbushe kila kwa wakati, hakikishs kila mlo iuna matunda na mboga za majani nyingi kuliko wanga na nyama.


Anywe maji zaidi na asitumie sukari kabisa au atafute mbadala n.k.

Asipobadilika baada ya mwezi tangu umpige mkwara basi hamishia kesi kwa aliewafungisha ndoa na wazazi wenu.

Natumai maelezo haya yatakusaidia kwenye kufanya maamuzi yenye busara.

Kila la kheri.

No comments: