Thursday, 5 February 2015

He cheated X4 with same kimama


hello dada Dinah.
Mimi ni msichana wa miaka 26, nina mpenzi wangu nampenda sana ila ame cheat na sio mara moja.

Nimekaa nae muda wa mwaka na nusu. Mara ya kwanza tulipendana sana na sikuhisi kitu nampenda mno nae ananipenda sana huyu kijana na ni wa umri wangu.

Siku moja nikawa niko kwake na laptop yake naangalia movie yeye hayupo....mara nikaingia kwa file la camera nikakuta videos kama 4. Kufungua video moja ni yeye yupo anafanya mapenzi na mwanamke pale ndani kwake kitandani anajirekodi kwa kutumia laptop.Nilipanic sana nka save zile videos. Mwanamke simjui ila anaonekana Malaya tu jinsi ananyoonekana. Alivyorudi  nikamuonyesha..akalia na kukiri ni shetani.....nkaondoka kama baada ya muda na kuomba msamaha nikasamehe.
Ila dada Dinah ishapita miezi kama minne ila kila mara nakumbuka ile video na nakosa raha, nakosa hamu ya kufanya nae mapenzi, nakosa raha kabisaa.Najaribu ila nimeshindwa kusahau namuangalia na kuumia sana kwanini anifanyie hivo
baaadae kabisa nkaja kujua huyo dada wa video ni bar maid.


Nkampigia Simu basi akasema ye keshatembea na huyu mwanaume wangu mara nne na anampa pesa, yeye anafanya tu biashara maisha magumu.


Inauma zaidi kua sio mara moja tu kalala nae ila mara nne anasema kaka alimuambia mimi siishi pale ndani ni wa kuja nakuondoka tu coz aliona nguo zangu na viatu na vitu wakati ukweli ni kwamba naishi nae pale ila nlikua nasafiri kikazi siku mbili au tatu ndio akamleta usiku.Dada dinah hata kwenye video anafanya nae mapenzi hata hajavaa kondomu, nliogopa sana juu ya afya yangu lakini
nampenda sana nae anadai ananipenda japo ana mapungufu.Tatizo ni kwamba nlikuta bado anampigia huyo barmaid tena usiku, nkamuuliza we mbona unawasiliana nae na nikakuuliza unawasiliana? akanidanganya eti rafiki ake ndio alikua anataka kuongea na huyo barmaid.


Dada Dinah sina uaminifu tena, nasahau week moja afu nakumbuka tena kila kitu naumia. Nataka huyu ndio awe mume wangu na tuko steji za kupanga ndoa sasa nifanyaje?

Confused,  nampenda sana ila hilo ndio tatizo naomba unisaidie nifanyaje.

Nashindwa kuamua natamani hata ningeondoka hiyo mwaka jana nlivoona hiyo video ila muda huu nimesamehe ila ipo kichwani yaani nahisi kama kila muda ana cheat tu.

***************

Dinah anasema: Hiya mrembo pole kwa maumivu ya moyo na maaumbuko ya akili.....mapenzi matamu ukimpata akupendae zaidi ya umpendavyo vinginevyo ni shida bin taabu. 


Mie huwa nashindwa kuelewa kinachowafanya watu kusamehe mtu alietereza nje......hilo kosa halisameheki na hakuna excuses ku justfy Umalaya wake na akome kumsingizia  Shetani kwa maamuzi yake machafu.


Mtu akiku cheat kamwe huwezi kusahau so ukisema umemsamehe ni wazi kuwa unajidanganya.


Cheaters hukimbii kulia na kuomba msamaha kama sehemu ya ku jitter na ku baki kwenye control.....kwamaana kwamba ukimsamehe hutoweza kuzungumzia uchafu wake tena.....umemsamehe so yameisha. ..sijui unanipata?


Na ukisha samehe cheater kwa mara ya kwanza.....utaendelea kusamehe tu na yeye anaendelea ku cheat kwa vile anajua "mapungufu" yako yalipo ambayo ni kumpenda kupindukia wakati yeye hana mapenzi kwako.Huyo mwanaume hana mapenzi,  utu,  heshima na hajui thamani yako kwahiyo hakufai so achana na " nataka awe mume wangu"....hawezi kuwa mumeo unless unataka kuishi unavyoishi maisha yako yote yaliyobaki bila kujua furaha na raha ya kuishi na mwanaume.


Mwanaume anafanya mapenzi na mtu kitandani kwetu na kutunza kumbukumbu ya video kitu kinachoashiria hataki kusahau halafu bado unataka awe mumeo? Really?


Akitoka nenda kachukue kilicho chako hapo kwetu au mwachie (ikiwa havina thamani) kisha sepa bila kumwambia.....Hata akikutafuta usimwambie kwanini umeachana nae na poteza mawasiliano yake.


Sio mara zote tuna achana na wapenzi tukiwa hatuwapendi....tunatoka kwenye uhusiano tukiwa tunawapenda na ndio mana huwa inauma sana.....Lakini kutokana na issues zisizovumilika inabidi kuanza upya bila yeye.


Ukijipa nafasi ya kulia (kuomboleza) na kukubali mwisho basi unasonga mbele kama ifuatavyo.

Kuna topic ya jinsi ya ku songa mbele nadhani niliandika 2014...ipi tie.


Ni binti mdogo na mrembo, kuwa Imara na songs mbele bila yeye kwani ana kupoteza muda wa kukutana na mwanaume mwema na mwenye mapenzi ya dhati.

Kila la kheri.

3 comments:

Anonymous said...

Mtu sio mume wako bado anakuumiza hivyo sasa akikuoa si ndio basi tena. Wazazi wetu walisamehe na kuvumulia kwa ujinga wao wa kuogopa jamii itawafikiriaje na baba zetu walendelea kuwa malaya kwasababu mama zetu waliwasamehe. Kama wangegoma kusamehe wanaume wangejenga adabu. leo hii hakuna kuvumulia upuuzi kama huu na hakuna kusamehe.

maisha yeye we yamejaa stress kwanini jitu lingine likuongezee stress kwa vile alilelewa kwenye familia ya mama msamehevu na baba malaya na kuona ndio kawaida na hivyo kuendeleza culture ya familia yake. his dad was his role model ni mwanaume wa kwanza anaejivunia na kama baba yake alimuumiza mama yake na mama akasamehe basi ataendelea kutegemea kusamehewa na hatoweza kuona thamani ya mwanamke. Kimbia mama Kimbia.

Anonymous said...

Dada shukuru Mungu hyo video umeiona kabla hamjaowana..Atleast umeeza mjua vzuri.
Songa mbele sababu utaendelea kujiumiza.

Anonymous said...

Duu,yani mi nlivyo na hasira mwa mambo kama hayo nsingeweza kuvumilia..hakika hakuna mapenzi ya dhati hapo na huyo bar maid ameshaiteka akili ya huyo mwanaume,na kwa vile yuko kibiashara itakuwa alimpatia mapenzi motomoto ili asimsahau na ndo mana amerecord..unataka Mungu akufunulie nn tena!ushaoneshwa ukweli amua kuchagua njia nyingine ya maisha,achana nae huyo.