Monday, 5 January 2015

Mume wangu anichukia, anikana nifanyeje?

"Habari za kazi dada. Nimevutiwa sana na Blog yako. Mimi ni Mama wa miaka30 nimeolewa miaka miwili iliyopita na tumejaaliwa Mtoto mmoja. Mume wangu ni mtumishi mkubwa Serikalini.

Tatizo nililonalo dada na wadau wote ni kwamba Mume wangu nimetoka nae toka shule, kwenye mapenzi yetu hakuwahi kuninunulia hata chips!

Sikujali kabisa kwani nilielewa ni Dent baada ya muda nilishika mimba na nilipomueleza hakujibu kitu na akanitoroka kitu kilichopelekea kukosa kote Shule na Boyfrend.

Baadaye, zaidi ya miaka mitatu akantafuta na kuniomba msamaha kuwa ni kwasababu ya mazingira alokuwanayo akaogopa nakunikimbia. Nilimsamehe kwavile nilimpenda toka moyoni.


Kwajuhudi zangu binafsi nilikazana sana na shule hadi aliponitafuta nilikuwa Form6 na yeye akiwa chuo mwaka wa tatu lakini nilikuja kuhisi ubinafsi wake hapo kwani sikuwahi kupewa japo Kadi ingawa Chuo huwa tunapewa boom.

Nilifanikiwa kupata nafasi UDSMd nikamaliza vizuri. Mpenzi wangu huyo aliniomba kwa machozi anioe, nilimzungusha kwa miaka kadhaa then nikakubali.

Toka tumeoana ni vituko ndani ya nyumba, mara anisimange, mara nimfumanie na wanawake wakifanya starehe na kunikataa kuwa mie sio mkewe. Mara anifukuze kwa kudai namng'ang'ania anasema alikosea kunioa ili mradi tu ni manyanyaso.

Hanihudumii kwa chochote kile yaani sigusi gari lake, biashara zake wala hela zake. Hakai na document yoyote ndani anampa mama yake nazingine anaficha ofisini.


Amejenga nyumba kadhaa kwa siri, amenunua viwanja vingi tu hapa dar kwa siri, account zake ni za siri, miradi yake ananificha nakuja kuambiwa na mahawara zake wakijisifia kwangu.

Kwa kweli inaniumiza kupita kiasi hasa ukizingatia napenda kumtumikia MUNGU wangu lakini yeye hana hofu ya MUNGU. Anawaza ubinafsi, chuki, uchoyo na anataka nimpe mshahara  wangu utumike nyumbani wakati yeye hajui wala kuhusika na mahitaji yangu.

Chaajabu nakuta anawatumia pesa wanawake wengine, mwingine anamwomba ampe gari, anawanunulia gold wakati mimi niliyemvumilia hata mia yake siioni!!

Hivi juzi kanunua Simu ya Milioni 1.5 wakati mie kisimu nachotumia Mungu anajua. Nimemuomba nikasome kanifokea kama mtoto!


Ndugu zangu anawachukia kuliko kawaida ila wake ndio anataka waje tukae nao. Jamani wapendwa nisaidieni, kama vikao tumeshakaa x3 anaomba msamaha na kuahidi kutorudia lakini wazazi na Wachungaji wakiondoka nakiona cha moto.

Ndoa nilofunga ni ya kikristo nami ni mdada mzuri sio najisifia bure hapana, msomi na mcha MUNGU siwezi kumsaliti ingawa natongozwa sana.

Mtoto wangu ndio kwanza ana mwaka lakini nimechoka. Nisaidieni ushauri jamani wapendwa".

**************

Dinah anasema: Habari ni njema sana, Heri ya Mwaka mpya na ahsante kwa ushirikiano.

Natambua kuwa baadhi ya Watumishi wa Serikalini Ndoa kwao ni "status" kwamba hulazimika kuoa kwa ajili ya nafasi zao za kazi (waijua ile kama huna Mke huwezi kuwa Rais sort of thing), sasa baadhi hufunga ndoa na yeyote anaepatikana kwa wakati huo ambae ana ka-historia nae.

Wengi huepuka kuibua mtu mpya na kufunga nae ndoa haraka, hivyo huamua kurudi nyuma na kuangalia nani "anafaa" na sio anampenda.


Sasa kutokana na maelezo yako nahisi kuwa wewe ni "victim" wa "ndoa kwa status" kwake na sio Mapenzi.

Huyo Baba hakuwa na mapenzi kwako na kithibitisho ni pale alipokukimbia baada ya kumuambia kuwa umeshika Mimba pia kitendo cha kutoonyesha hisia zake za mapenzi kwako kwa-mf. kukununulia zawadi (siamini katika kumtegemea mwanaume lakini naamini kuwa mwanamke anatunzwa/tunukiwa Zawadi kama sehemu ya mapenzi).


Ikiwa mumeo anakukataa/kana mbele za wanawake wengine kuwa wewe sio mkewe ni wazi kuwa wewe sio Mkewe. Kumiliki Cheti cha Ndoa kinachothibitisha Muungano wenu sio Tija ikiwa haumo Moyoni mwake na hashirikiani na wewe kwenye masuala ya kimaisha na kifamilia..

Sina hakika kwanini bado unaendelea kuwemo kwenye Muungano huo, natumaini kuwa Ukristo wako na Kumuamini Mungu kwako sio Kigezo cha kuvumilia visivyovumilika.


Angalia utaratibu wa kumtaliki kupitia Mahakama (Kisheria). Nenda kawaone Wanawake Wanasheria kwa ushauri zaidi wa wapi pa kuanzia na kwa ajili ya kupata "mafao" yaliyochumwa mkiwa kwenye Ndoa na matunzo ya Mtoto wenu.

Hata kama hakushirikishi kwenye Mipango ya maendeleo na Documents anaficha kwa mama'ke bado Kisheria unahaki ya kupata Mgao kwani yote hayo yamepatikana ukiwa kwenye ndoa.

Kama sheria haijabadilishwa, nadhani kuishi na mtu kama mume au Mke kwa miaka 2 Kisheria inachukuliwa kama ndoa hata kama huna Cheti(common law).


Nipo mbali na Tz, hivyo sio rahisi kwangu kukuelekeza kwenye Vikundi vingine vinavyosaidia Wanawake Kisheria.


Natumai wachangiaji wengine wanaweza kusaidia kwenye hilo na pia kukupa ushauri tofauti na wangu ili upate kufungua mawazo na kufanya uamuzi wa Busara.


Kuwa Imara, seek furaha maishani mwako, usikubali kuwa Mtumwa wa "ndoa" ambayo haina faida kwako.


Kila lililo jema.
Mapendo tele kwako...

3 comments:

Anonymous said...

Sister, si fikiri kabisa kama huyo jamaa inafaa hata kumwita yeye ni mmeo. maana kama toka muowane hajawahi kukupa zawadi yeyote.na wewe unaendelea kuishi nae na kumpa uroda kila siku. ni hatari kubwa kwako. maana jamaa anatoka nje sana na hata kukukana mbele za wanawake wengine. hivyo tegemea maradhi mazito mbele ya maisha yako au sasa hivi achana nae. vikao umekwisha kaa na ushauri mmekwisha pewa na jamaa hajabadilika hivyo wewe unangoja nini. Jamaa anakuterorize,na wewe unavumilia. tazama ustaarabu wako usiwe na khofu kazi unayo na chakula cha uhakika utapata na juu ya yote hayo utakuwa huru.Uhuru wako ndio kitu muhimu sana katika maisha yako yote. Hata ukiwa mke wa Rais lakini kama huna uhuru you are nothing.

Anonymous said...

Kwakweli Dada una moyo WA jiwe. Dunia ya Leo na elimu uliyonayo bado unakubali kunyanyasika kiasi hicho?? Ifike mahali usema IMETOSHA. Huyo sio mums Bali ni tatizo achana nae kabla hayajakupata makubwa zaidi ya hayo manake kama MTU anakufanyia ukatili kama huo na bado unaendelea kukaa huwezi jua anafikiria kukutendea nini kikubwa zaidi ya hayo, anaweza hata akakuua ili awe mjane afanye starehe kwa Uhuru. Amka mama kumeshakucha. Frm mama Olivia. Mwanza.

Kirungu said...

Hivi unawezaje kuishi na mtu kama huyo ambae ana Ku treat km mpita njia.. Wewe nenda TAWLA wakusaidie kumtaliki huyo ni shetani kbsa_(samahani) Sasa alikuoa ili iweje? Mijitu mingine shwaini kbsa.Hebu fanya hima kbla hujapta maukimwi kwa msaada zaidi check me up via Kirungu 6.7@gmail.com