Tuesday, 13 January 2015

Mume wa Ndoa, kaikataa Mimba!

"Ni mume wangu wa Ndoa na tumezaa mtoto mmoja mwenye mwaka, nimeshika Ujauzito tena wenye mwezi na nusu lakini Mume wangu kaukataa kwasababu nimechelewa kumuambia.***********


Dinah anasema: Hello there! Hawezi kukurupuka tu na kuikataa Mimba wakati wewe ni Mkewe na mnafanya Ngono bila Kinga (obviously).


Mumeo nae wa wapi?!! Chini ya Miezi mitatu ni mapema sana kwa baadhi ya wanawake kujua kama wameshika Mimba unless ajipime au akapimwe, Tena baada ya kuzaa ndio kabisaa, maana mabadiliko ya mwili bado hayaja-settle hasa kama ulikuwa unanyonyesha.


Inawezekana kutakuwa na sababu ya kumfanya aikatae Mimba, huenda anatafuta namna ya kukuacha/achana nawe......kabla hatujamjaji hebu nisaidie....Je maisha yenu ya kimapenzi yakoje au yalikuaje kabla hujashtukia una Ujauzito?

Ulipopata ujauzito wa kwanza hali ilikuaje kabla ya tukio? Mlikubaliana mzae au ilikuwa "bahati mbaya" ?

Uchumi wenu ukoje? Je mnaweza kumudu mtoto wa pili? Mlikuwa mnatumia dawa za kuzuia Mimba?
Au labda kuna vijitabia ulivianzisha vinavyomfanya ahisi kuwa Mimba sio yake? Asije kuwa alikutegea kwa kutokukojoa ndani lakini akajifanya kakojoa na wewe bila kujua ukadhani umebeba manii yake.

Bila maelezo kamilifu kwakweli siwezi kusaidia kimawazo. Nahitaji maelezo yakinifu na yaliyojitoshereza.
Mapendo tele kwako...

No comments: