Friday, 9 January 2015

Mpenzi Busy na Kazi/Familia yake

Shikamoo dada Dinah & hongera kwa kazi nzuri unayofanya. Mimi nipo kwenye uhusiano kwa miaka miwili sasa.


Nampenda sana mpenzi wangu naye ananipenda. Napenda sana mpenzi wangu awe ananishirikisha kwenye mambo yake lakini huwa haniambii chochote kuhusu plan zake.

Kingine ni kuwa hatuna muda wa kuonana inaweza pita hata miezi mitatu yupo busy na kazi & I understand that, Weekends anakuwa na familia yake so kwa mimi hana muda.

Tunawasiliana kwa simu but yeye ni mvivu mpaka sometimes huwa naamua kukaa kimya. Atanitafuta na kuniuliza kwanini nipo kimya?

Napenda kuwa karibu naye na awe ananishirikisha mambo yake nifanyaje?
God bless you!!


******

Dinah anasema: Marhabaa mrembo, ahsante kwa ushirikiano.


Kwani mna muda gani tangu mmekuwa pamoja? Inashangaza kuwa mtu unaemuita Mpenzi hana muda na wewe isipokuwa Kazi na Familia yake.

Mtu anaekupenda siku zote atatafuta namna yeyote tu ya kuwa na wewe ana kwa ana, haijalishi yupo busy kiasi gani na Kazi au Familia yake.


Nahisi kama vile wewe sio muhimu kwake au kwenye maisha yake kama unavyodhania.


Inawezekana ni mapema sana kuanza kukushirikisha kwenye masuala yake ya kimaendeleo au pia inawezekana kwenye mipango yake ya kimaisha huko mbele wewe haupo....yupo nawewe ili kupoteza muda (sio serious kwenye Uhusiano).

Lakini!!! Kama anapata muda wa kuwa na Familia yake(hope ni ndugu na Wazazi wake na sio mke na watoto) ni wazi anaweza kuugawa muda wake huko kati yako na Familia yake....Mf: J'mosi anakuwa na wewe na J'pili anakuwa na Familia.

Weekend ina Masaa 48....kati ya hayo masaa ni kweli hawezi kutenga masaa 10 ya kuwa na wewe?!! Unless otherwise mnaishi mikoa mbali-mbali.

Kukutafuta kwa simu baada ya kumchunia sio kithibitisho cha Upendo au mapenzi.

Huyu mwanaume sio Mvivu bali hajali hisia zako kwake au haoni umuhimu wa kutumia muda wake na wewe bali watu wengine (kazini) na familia yake.

Tafuta nafasi ya kuzungumza nae ana kwa ana(sio simu wala texts) mueleze jinsi unavyojisikia kutokana na ukosefu wa mawasiliano(ya ana kwa ana).

Mwambie, Mapenzi pekee hayatoshi kuimarisha Uhusiano wetu, isipokuwa mawasiliano ya mara kwa mara na kutumia muda kuwa pamoja na kuzungumzia masuala ya kimaisha.


Ongezea, sio tu kwamba huwa nakosa amani kwa kutokuonana kwa muda mrefu, pia huwa na wasiwasi kama kweli unanipenda kama ninavyokupenda.

Endelea, mapenzi yangu kwako huongezeka kila tunapokuwa pamoja hata kama ni kwa Sekunde 60(Saa moja).

Malizia...naomba tuboreshe mawasiliano ya simu na ya kuonana ana kwa ana ili kuimarisha uhusiano wetu.

Majibu yake, kujitetea kwake au maelezo yake yatakufanya ujue umesimama wapi....

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

No comments: