Monday, 12 January 2015

Kupenda Attention kwenye Uhusiano.

"Mimi ni mdada wa miaka 30, sijaolewa na wala sina mtoto ila nina mpenzi ambae ndio kwanza tumeanza mahusiano, tuna miezi miwili tu.

Tatizo langu kubwa ni kwamba huyu mwenzangu ni mvivu kuwasiliana yaani kutuma msgs ni mpaka awe ametoka kazini au Mara chache akiwa kazini atatuma msg labda moja au anakaa kimya kabisa.

Pia nikimtumia ananijibu kwa ufupi tu and mara nyingine hajibu labda mpaka usiku kabisa ndio atapiga simu. Sasa Mimi ni mtu ambae napenda "attention" na isitoshe nafanya kazi Mkoani kwahiyo naona kuna ugumu kidogo hapo kwangu.


Kiukweli nampenda na yeye pia anaonesha kunipenda, sasa je nafanyaje juu ya hili suala?


Ina ishu ya Pili je ni mapema sana kuanza kuongelea mambo ya maendeleo Kati yetu? Yeye ni mkimya kidogo kuliko Mimi Kwahiyo pia ni Mzito kidogo kusema kama labda amekwazika kitu Ofisini.

Atasema amekwazika ila hatasema wazi ni nini kimemkwaza labda mpaka niulize sana, hapa pia nahitaji msaada wa namna ya kukabiliana na hii hali da Dinah?

Natanguliza shukrani zangu kwako na kwa wadau wengine.


**********

Dinah anasema: Shukurani kwa ushirikiano.


Unamiaka 30 hivyo nachukulia kuwa mwenzio ni wa umri huo au Mkubwa zaidi. Watu tulio 30+ huwa hatufanyi mambo kama teen au early 20, moja ya mambo yaho ni kupiga siku kila baada ya nusu saa na texts msg kila baada ya dakika 5.


Kwenye umri huo(nilioutaja) tunakuwa na mambo mengine muhimu yanayohitaji muda kuliko kutuma msg au kupiga simu mara kadhaa kwa siku.


Tangu uhusiano wenu bado ni mpya huenda hataki kuonekana "needy" kwako na ikawa sababu ya wewe kumkimbia(baadhi ya wanawake hukimbia needy men kwani wanakua kama Mama na sio Wapenzi kwa wanaume hao).


Sidhani kuwa ni uvivu, inawezekana kabisa ni kutingwa na Kazi....angalau anakukumbuka kabla siku haijaisha au baada ya Kazi hiyo inaonyesha anakujali.

Sote tunapenda "attention" na isipokuwepo au usipopewa na Mpenzi wako hakika utahisi upo "single" kwenye uhusiano na mpweke if that make sense! Mpenzi asipokupa hitaji hilo ni wazi anakudharau au hau-exist....upo tu kama Meza au Kiti (unatumika ukihitajika ila sio muhimu).


Jaribu kuzungumza na mwenzio na kumwambia umuhimu wa ninyi kuwasiliana kutokana na umbali ulipo kati yenu. Hisia za mapenzi pekee hazitoshi kuwafanya muwe karibu wakati kuna umbali kati yenu, mawasiliano ndio yatakayowasogeza na kuwapa ukaribu mnaouhitaji ili kuwa na uhusiano wenye Afya.


Onyesha kuwa simu yake kwako ni muhimu sana kwani inakupa Amani moyoni na kukuondolea hofu ya kama yupo salama au la!

Kubalianeni muda wa kuwasiliana, mf: asubuhi kabla na mara mkifika Kazini....wakati mnatoka na mkifika Nyumbani na kabla hamjalala. (This worked for Us kitamboo kati ya London na Scotland)....so ijaribuni.


Issue ya pili; Ndio ni mapema sana kuanza kuzungumzia masuala ya maendeleo kati yetu, lakini unaweza kuzungumzia masuala ya Kimaendeleo kwa ujumla....hii itamfanya ajue ni mwanamke wa namna gani linapokuja suala la Maendeleo.


Uhusiano ukikomaa ingia full-force na kumtuka kutumia "yetu" (badala ya yangu), "sisi"(badala ya mimi) kwenye mazungumzo yenu ya kimaisha na kimaendeleao.


Nadhani most wanaume huwa sio muongeaji kuhusu changamoto za kazini, hu-prefer kuumia kimya kimya kisha kudharau na kusonga mbele. Wanaume hubadilika wakishafunga ndoa au kuwa kwenye uhusiano na mwanamke kwa muda mrefu na kumuamini.

Kutokana na "umri" wa Uhusiano wenu sio rahisi kwa jamaa kujiachia kwako kwa kila jambo, hapa nadhani kuwa mvumilivu na akiwa comfortable ku-share mambo yake ya kazini na wewe atafanya hivyo.


Pamoja na kusemaa hivyo sio mbaya kuonyesha nia ya kuwepo kwa ajili yake. Always offer kuwa akama anataka kuzungumzia lolote asisite kwani upo pale kwa ajili ya kumpenda na kumsikiliza na kumshauri kama atahitaji.

Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...

No comments: