Friday, 5 December 2014

Mzee aniharibia Nyumba!

"Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, mpenzi wangu ana Ishirini na Tisa na tumeishi nyumba moja yapata mwaka.

Kwa sasa tunatofauti kidogo. Mpenzi wangu alianzisha uhusiano na Mzee ambaye ni mkubwa kwetu. Baada ya muda niligundua kuwa kabla ya uhusiano wao huyo Mzee alikua karibu na familia yake.

Hivyo tuligombana na ugomvi ulikuwa wa muda mnamo /11/2014 niliamua kumpigia simu huyo mzee na alikua mstaarabu na kuahidi kuachana na huyu Msichana.

Alipojua nimefanya hivyo tuligombana kwa maneno mpaka ikafikia hatua ya kupigana, nilimuumiza na yeye akaamua kwenda kwao.
Kwa sasa ninajaribu kurudisha penzi letu lakini napata shida sana nifanye nini ikiwa bado namuhitaji?"


*************


Dinah anasema: Habari gani? Ahsante kwa ushirikiano.Ikiwa Mpenzi wako amekusaliti kwa kutoka na mzee huyo na ukajaribu kukomesha uhusiano wao kwa kuzungumza na Mzee husika ili akuachie Mpenzio. Lakini Mpenzi wako akakasirika na kugombana kutokana na kitendo cha wewe kupigania penzi lenu unadhani Mwanamke kama huyo anakupenda au kukuthamini?

Mtu anapofikia mahali anatetea Kosa lake au kutafuta sababu ku-justify anachokifanya au mtu anaetenda nae kosa ni wazi kuwa huna umuhimu kwake.
Kitendo cha wewe kumpiga na kumuumiza sio kizuri(ni Kosa Kisheria), pamoja na kumpenda kwako sidhani kama ni sahihi kuendelea kupigania Penzi ambalo ni la upande mmoja tu (wako), angekuwa anakupenda kwa dhati msingefikia mlipofikia.
Jitahidi kusahau na utafute namna ya kusonga mbele na maisha yako bila yeye.


Nakutakia kila lililo jema.
Mapendo tele kwako...

1 comment:

Anonymous said...

Nyie ndo mnaletewaga magonjwa after that manaanza kulaumu na kusema Laiti kama au ninge zinakuwa nyingi.Hv huoni tu kuwa hakupendi?rudia kwake bc akukomeshe,au lbd We ni wale wanaume wanaopenda kushare penzi pasina kinyaa