Wednesday, 3 December 2014

Mbinu za Kupendwa Ukweni!

"Dinah habari, nilikuwa nataka kujua jinsi ya kuelewana na kupendana na ndugu wa Mume wangu katika kutafuta google ndio nikakutana na Blog hii.

Mie na Mume wangu tumefunga Ndoa miaka kadhaa na tumejaaliwa watoto Watatu. Mwanzoni hatukuwa na matatizo yeyote kati ya Shemeji na Wifi zangu.

Matatizo yameanza hivi karibuni na chanzo sikijui. Nimejitahidi sana kuwapenda ndugu wa Mume wangu lakini hawapendeki. Kila wakija kwangu ni maneno, imefikia hatua wanasema nimembadilisha Kaka yao.


Nikiongea na Mume wangu kuhusu habari hizi, yeye anaishia kusema niwadharau.

Je, nifanye nini ili kuwe na Amani miongoni mwetu? Naomba ushauri au kama kuna hatua, mbinu zozote za kuwafanya ndugu wa mume wangu wanipende, wanikubali. Ahsante".


**************


Dinah nasema: Nakumbuka nilikwisha zungumzia kuhusu hili ila kwa namna nyingine kati ya mwaka 2007 na 2008 (angalia kwenye Topic zilizopita hapo Kulia).

Niligusia kuwa wakati unaandaliwa(Fundwa) ili uende kuishi na mtu mwingine(Mume) na watu wengine (ndugu zake), unaonywa wazi kabisa kuwa uwaheshimu ila usilazimishe wakupende na kamwe usijipendekeze kuwapenda!

Kibinaadamu huwa inatokea una-click na baadhi ya watu na mnakuwa na mahusiano mazuri kama Wifi/Shemeji na wakati mwingine unachukiwa kabla hata hawajakufahamu.


Kosa Kuu ni kuwa tunaaminishwa kuwa ni "lazima" uwapende ndugu wa mwanaume na matokeo yake unasahau kuwa hao "ndugu" ni Binadamu na Binadamu anahisia na hisia hizo sio lazima ziwe za upendo kwako.....sasa ukienda Ukweni full force "nawapenda ndugu zake" hakika itakuumiza.

Pia wakati mwingine wewe mwenyewe inatokea tu unampenda "Wifi" yako na unatamani mngekuwa "marafiki" ukidhani atasaidia kulinda Ndoa yako in case ikabuma.

Ninachojaribu kukuambia hapa ni kuwa, ni muhimu kumchukulia kila mtu kama alivyo na kumheshimu (so long anakuheshimu pia), kama hawakuheshimu basi achana nao (wadharau).

Kumbuka Upendo haulazimishwi. Kama ilivyo Shuleni au Kazini, unakutana na watu ambao huwajui, hujawahi kuwaona maishani mwako lakini inatokea unapatana na baadhi na wengine inakuwa Hola(huwapendi au hawakupendi).

Na pengine unawachukulia kama walivyo tu bila kuwa na hisia ya chuki au upendo kwao hivyo wanakuwa Wanafunzi wenzio au Wafanyakazi wenzio na sio Rafiki zako.

Hakuna mbinu zitakazowafanya ndugu wa Mumeo wawe kama unavyotaka au ulivyotegemea. Wanamaisha yao na familia zao (Wake/Waume na watoto wao).....usipoteze muda na nguvu kulazimisha Upendo ambao haupo, Wekeza Muda na Nguvu zako kwenye zingatia maisha yako, ya wanao na Mumeo.

Likitokea jambo la kuwakutanisha kama Ukoo(tangu umeolewa na Kaka yao) shiriki bila kinyongo, ongea nao kama watu tu (sio Wifi-Shemeji).

Kila lililo jema.
Mapendo tele kwako...

3 comments:

Anonymous said...

14006346
15819555403256Dada yangu umepata ushauri mzuri sana kwa dada Dina. La kuongezea tu usikubali kunyenyekea sana na ukaja sahau utu wako au heshima yako. maana ukitaka wakupende ni lazima ufuate vile wenyewe wanavyotaka! pengine watakavyowao sio utakavyo wewe, hivyobasi usikubali kuwa mtumwa wa kutaka kupendwa na kaka/dada wa mmeo. umekwishapendwa na mmeo vivyo yatosha.wewe waheshimu kama jamaa au ndugu wa mmeo na usikubali kudharauliwa nao. endelea na maisha yako na wala usijali wafanyalo. mwisho wakishindwa watakupenda tu.

Anonymous said...

Mweee dinah umenigusa kwa ushauri utadhani umenisoma.mi Mwenyewe huwa clazimishi wanipende wala kujipendekeza na pia siwadharau.huwa najisemea kwenye Cheti chá ndoa hakuna sharti lá mpaka upendwe na ndugu

Anonymous said...

Ndugu wa mume hawapendeki ht kidogo waheshimu tu full stop