Friday, 1 August 2014

Mwaka kama wapenzi(online) ila hataki tuonane.

Am sorry dada dinah nina mpenzi kwa mwaka na nusu tangu tuwe kwenye mahusiano lakini hatujawahi kuonana.Mpenzi huyu nilimpata kwenye Mtandao flani. Shida inakuja kwenye kuonana, hivi kwanini hataki niende kwake kwa suprise.


Hebu nisaidie je ni mtu mwema kweli?Dinah anasema: no bother Mrembo, ahsante kwa Ushirikiano.


Sasa mdogo wangu humjui huyo mtu, hujawahi kumuona zaidi ya maandishi, simu na labda Picha....Kitu gani kinakufanya utake kum surprise nyumbani kwake? Akikubaka au kukuchinja je??!!Mtu wa mtandaoni anaweza kuwa anybody kuanzia mtu genuine mwema tu Muuaji sugu.
Logically unapokutana na mtu Mtandaoni na kuanzisha uhusiano au kudhani mnauhusiano na kuitana majina matamu (ya kimapenzi) unashauriwa kuonana nae ana kwa ana mahali ambapo kuna kadamnasi ya Watu.

Hupaswi kukubali kwenda nae hotelini, guest au kwako/kwake ukiwa peke yako. Hakikisha unapokwenda kukutana nae watu wako wanajua na kama inawezekana wajue ni wapi hasa unaenda ili kuepusha Mauaji au Ubakaji.
Watu wa Mtandaoni wengi wao (Wake kwa Waume) huwa ama waongo au kuna walakini kwenye Utambulisho wao, kwamba maisha yao ya "online" ni tofauti na maisha yao halisia.Siwezi kusema huyo bwana ni Muuaji au Mbakaji, ila nadhani atakuwa ama kwenye uhusiano au hataki kuwa na wewe kama mpenzi ila anafurahia ku-flirt tu na wewe.Mapenzi ya Mtandaoni ku- pass time hasa kama ana issue na Mpenzi wake.Kuna wengine hu-pretend kuwa wanaume/wanawake ili kuendesha maisha yao ya Mtandaoni.....ni tatizo la akili na linajina lake (nimelisahau).Sasa mtu kama huyo hatokubali uonane nae, achilia mbali kum-surprise nyumbani kwake!!!
Nikijibu swali lako: Siwezi sema kama ni mwema au sio Mwema, ila nadhani hana mpango na wewe in real life, anafurahi na wewe kimtandaoni tu.
Natumai maelezo yangu ambayo hujayaomba(nimehisi kuwa responsible kukueleza) yatakusaidia kupanua upeo wako kuhusu Maisha ya Mtandaoni.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

No comments: