Friday, 22 August 2014

Chuki ya Mzazi kwa Mpenzi...

Dada habari za wakati huu mimi ni kijana wa kati nina mpenzi wangu ambae tunapendana sana pia tumefikia hatua ya kukubaliana kuoana.

Uhusiano wetu sasa una mwaka na nusu tatizo limetokea upande wangu ambapo mzazi wangu anaonesha hali ya kutompenda huyu nimpendae.

Halafu mara nyingi humuonesha Mpenzi wangu na sio mimi yaani hajaniambia hamtaki sasa mpenzi wangu anaumia coz tunapendana kweli nae anaogopa baadae inaweza kutokea akajateseka.

Sasa hii imeleta hofu ya kuishi na mimi na sijui nifanye nini maana amekata tamaa kiukweli, naumia sababu sihitaji kumkosa kwani nampenda sana.***********

Dinah anasema: Habari ni nzuri kabisa, ahsante na shukurani kwa ushirikiano.
Issue yako ni ngumu kuhakiki na sio vema kwenda kumuuliza Mzazi wako kwanini anaonyesha kumchukia mpenzi wako wakati huna uhakika.
Pia huwezi kumkatalia Mpenzio kuwa anachosema au kukiona kutoka kwa Mzazi wako ni Uogo!

Mapenzi ni ya wawili hivyo mwambie mpenzio kuwa wewe ndio umechagua kuishi nae na unampenda. Kuwa na wewe sio kuwa/kuishi na Mzazi wako kwazi Mzazi wako alikuwa na maisha ya yake ya Ujana na mpenzi wake na yamepita, haya ya sasa ni yako wewe na yeye.
Baada ya kumhakikishia mpenzi wako Msimamo wako na hisia zako kwake, anza kuweka "ukuta" baina yao....yaani Mpenzio na Mzazi wako.

Hakuna haja ya Mpenzi wako kwenda kwa Mzazi wako.....yeye anakupenda wewe na sio lazima ampende Mzazi wako au Mzazi wako ampende huyo Binti(Upendo haulazimishwi).

Suala muhimu kwao hao wawili ni heshima, so long mpenzi wako anamuheshimu Mazazi wako na Mzazi wako anamheshimu mpenzio inatosha.

Ni kawaida kwa Wake(hasa wanawake) kudhani kuwa wana nguvu sana kwenye maamuzi ya kimapenzi ya watoto wao kwa sababu tu waliwazaa.

Baada ya kuweka "ukuta" kati yao(hawaonani) fanya uchunguzi kivyako ili ugundue ukweli kuhusu Chuki ya Mzazi wako kwa Mpenzio au Mpenzio kwa Mzazi wako....maana baadhi ya wanawake huwa na yao!


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

1 comment:

Anonymous said...

wapo baadhi ya wanaume huwaacha wapenzi wao kwa kisingizio cha wapenzi hao kutokubalika kwa wazazi.
Utaratibu huo ni mbaya na unavunja moyo wa mwathirika na kumfanya kutompenda mpenzi mpya kwa kuhofia kukataliwa na wazazi kama ilivyotokea ktk penzi la awali.

Nawasihi wazazi kuacha kuingilia mapenzi ya vijana wao kwani mwisho wa ubaya ni AIBU!