Tuesday, 1 July 2014

Wanataka nioe "Mtoto" ili asinizeekee!

Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa blog yako,nikupongeze kwa kazi yako nzuri
unayoifanya.

Umri wangu ni miaka 24, nipo kwenye uhusiano na binti mwenye umri wa miaka 23. Tumekuwa pamoja tangia nikiwa kidato cha Tatu na mwenzangu cha pili, hivi sasa niko Chuoni mwaka wa pili.

Kiuweli tunaelewana vizuri na
tumepanga na kuahidiana mambo mengi sana ikiwemo kufunga Ndoa hapo baadae.

Tatizo linalonisumbua ni umri! Yaani umri wake na wangu tofauti ni
mwaka mmoja je, hii mbeleni haitasumbua? kwa sababu wanaonishauri wengi
wanasema atanizeekea!

Ama pengine itapelekea nianze kuchepuka nje ya Ndoa angalau nitafute ninaye mzidi miaka 5 au mpaka 10.

Kiukweli inanichanganya coz nakumbuka alishawahi kukataa uchumba kwa
ajili yangu, naogopa sana kumuumiza.

Na je, kama tatizo ni umri sasa
ni tofauti ipi inafaa ya umri. Naomba ushauri katika hili ili nifanye maamuzi sahihi. Asante.


**********


Dinah anasema:Hi Dogo, Shukurani kwa ushirikiano.


Mpenzi wako akipunguza miaka na akakuambia anamiaka 10 au 16 itakufanya ujisikie vema na kuwa na uhakika hutoCheat baada ya ndoa kwenda kutafuta mwenye umri mdogo zaidi eti?

Hao marafiki zako au washauri need to go out a bit more, wanamawazo ya Kizee yaliyopitwa na Wakati au niwaite maPedo (wanapenda watoto wadogo kingono which ni Kosa Kisheria).

Umri ni namba ambayo "Mzungu" katulazimisha tuamini kuwa siku unayozaliwa ndio siku ya kwanza kuanza kuhesabu umri wako. Unauhakika gani kuwa miaka 24 uliyonayo ni kweli 24? Pengine ni 12 au 48!!...kwa mfano.


Kinachomzeesha mtu ni mawazo yake, mwili na jinsi anavyojiweka/beba sio siku aliyozaliwa kwani inaweza kubadilishwa wakati wowote.

Wewe na yeye wote mtazeeka ila kumbuka siku hizi wanawake wanajipenda sana, wanajua kujitunza nje na ndani, wanaijua miili yao hivyo utajikuta wewe umezeeka kuliko yeye....hii ni 2014 babaa, sio 1994!


Kinachopelekea watu wawili kukubaliana na kufunga ndoa Mara zote ni mapenzi sio Umri, kama mnapendana, mnaheshimiana kweli na mmepanga na kukubaliana kufunga ndoa, stick to it, achana na hao "washauri" wako ambao inaonyesha ama wanakuonea Wivu au hawampendi Mpenzi wako.

Kutoka nje ya Ndoa kunategemeana na tabia yako binafsi na heshima uliyonayo kwa Wanawake (mama yako incl) na Mkeo, sio umri wa mtu.


Nikijibu swalo lako la mwisho; hakuna umri sahihi au unaofaa kufunga Ndoa ailimradi tu mhusika na wewe mwenyewe mpo juu ya Miaka 17(Chini au hapo ni abuse dhidi ya mtoto na ni kosa Kisheria).

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

3 comments:

Anonymous said...

dinah mi kila siku nakukubali kwa ushauri wako. mi ni mwanaume nina mpenzi wangu anaye nizidi miaka 3 lakini tunapendana. miaka siyo shida, shida ni kujielewa

Anonymous said...

Word Dina. Nilimzidi miaka miwili marehemu mume na uhusiano wetu kwa kweli ulikua mzuri mno na umri haukuwa shida kwake wala kwangu. Moende mwenzako 'age is just a number'

Anonymous said...

mm mke wangu kanizidi mwaka 1 kamili. but haijawahi nipa shida hata siku moja. She's very mature na tunapanga mambo vizuri sana na yanaenda. Sijawahi hata kudhani umri utakuja kutupa shida coz umefunikwa na vitu vingi vizuri zaidi.