Monday, 7 July 2014

Tofauti ya Dini yaweza kuwa kikwazo

shikamoo da Dinah,
pole na hongera kwa majukumu. Nimerudi tena baada ya
kunufaika na ushauri wako wa kwanza. Naomba nsaidie katika hili.


Hivi karibuni nimekutana na mwanaume ambaye ni 10 yrs older than me na
mimi ni 22, ana mtoto mmoja. Nikamuuliza kuhusu mama wa mtoto, akanambia ilishindikana kumuoa kwasababu za kiukoo tu so mpaka sasa imeshindikana.

Sasa he is too fast! kantongoza tu next week anataka nimpe penzi eti
atajisikia vizuri na atakuwa na uhakika na mimi. Nikajiuliza kwani sex
ndio kipimo cha upendo? Sababu kuna vijamaa vishawahi kunambia hivo
nikavitolea nje lakini mpaka sasa vinanisumbua.


Sasa kuna mwanaume ambaye nampenda ila ni Islamic na mimi Christian na familia yangu
haitaki kusikia habari za mahusiano kama hayo.


Nikionana na huyu jamaa
baada ya salam automatically kifuatacho ni romance but bila sex, zaidi
ya nakupenda hajawahi nambia chochote kuhusu mimi na yeye.


Nishawahi kumuuliza akanambia a better future awaits, hakusema kingine tena mpaka leo na sasa ni zaidi ya mwaka. Kiukweli nampenda Dini inanipa shida.


majukumu mema!


**********


Dinah anasema: Marhabaa mrembo, shukurani kwa ushirikiano na Karibu tena.


Huyo mwenye Mtoto ambae sababu za kiukoo ni Muhimu kuliko hisia za mwenzie hafai kabisa! Bora hata angesema "things didn't work out".....kwani kuzaa na mtu sio Tiketi ya kufunga Ndoa.....Mwache AENDE.

Dini: Mrembo sote tumelelewa katika Mzingira ya Dini/Imani fulani lakini sio lazima kufuata Dini/Imani hizo bali unachagua kufuata na kuishi maisha ya kufuata Dini/Imani husika.

Suala la Dini ya familia yako lisikusumbue kwenye "stage" hii (liache) muhimu ni hisia zako kwa sasa. Tukisha pata commitment na kujua kama kuna "future" na Muislam then tutatafuta namna ya kushauriana(kutegemeana na uamuzi wako sio Wazazi wala huyo mkaka).

Pamoja na kuwa Muislam analeta matumaini ila nae haeleweki (kutokana na maelezo yako), ni vema kwamba hasumbui kuhusu Ngono, anakupenda na wewe unampenda, Chemistry yenu ni MOTO, nakubaliana nae mambo mazuri hayataki haraka....lakini nisichoelewa ni kutokuonyesha commitment kwako.Nijuavyo mimi kwa Muislam wa kweli(alieamua kufuata Imani kwa kuipenda, sio kwa kurithi), Uislamu wa mwanamke ni muhimu zaidi kuliko hisia za kimapenzi, na uislamu huo usiwe wa kulazimishwa.....mf; wewe uamue kuwa Muislamu sababu ya kumfurahisha au Ndoa bali kwa faida yako na Moyo wako.

Mwaka ni muda mzuri wa kuhoji "uhusiano" wenu ambao unaonyesha kuwa sio rasmi.

Sio mbaya kama utamuuliza....tumuite Mahmood sawa?!! "Mahmood tuna chemistry nzuri, tunaelewana na ninakupenda, ila sina uhakika kama tupo kwenye uhusiano au tunapotezeana muda".

Akijibu ki-hasi kwamba haonyeshi ku-commit na kuwa na uhusiano aka exclusive lakini anataka muendelee na mlichonacho....Muulize "unadhani tutaendelea hivi mpaka lini? na je hiki tulichonacho kwa mwaka sasa ni nini hasa?"

Jibu lake hapo ndio litakufanya ufanye uamuzi wa kuachana nae au kuendelea na kufurahia hicho mlichonacho bila kuwa na haraka wala Matumaini ya "siku tutafunga ndoa"....enjoy yourself as a woman....ikitokea Ndoa safi, isipotokea Ndoa poa vilevile.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

3 comments:

Anonymous said...

Kuwa makini wasikilize wazaz wako

Anonymous said...

Ni kikwazo kikubwa mno, na nakushauri kabisa usithubutu kuolewa na mtu wa dini totauti yako.Itakutesa sana labda kama mungu unamfanya spatre part za magari,lakini kama kweli una imani inayoongoza na kulea maisha yako katika unyoofu wa moyo mtu wa dini nyingine assinmgie kwenye anga zako za kimaisha.Hata ukibadili dini kwa ajili yake au ukibadili dini kwa ajili yako bado haitakuwa afya kweny mtasuguana mahali fulani.Imani ni kitu cha ajabu mno usikichezee.

Anonymous said...

Ahsante kwa ushauri.. nitazingatia