Wednesday, 16 July 2014

Sitaki kufika 30yrs nikiwa Bikira

Habari dada, Natumaini hujambo. Naomba ushauri wako kwa hili. Mimi ni msichana soon will turn 26. Nilikua na bf lakini tuliachana miaka 2 iliyopita na tulikaa kwa miezi ka 6 tu kabla hajaniacha.


Alikuja niambia baada ya muda bila mimi kumuuliza sababu ya kuachana na mimi ni alirudiana na Ex wake.

Kipindi tulichokua pamoja kama couple hatukufanya sex wala hakuniforce kufanya coz alikua anajua sijawahi kufanya sex before.


Baadaa breakup tukawa friends tu though deep down ile breakup iliniuma sana na ilichukua muda kumove on, karibu mwaka.

Mwaka huu tumekutana kwenye course fulani tunafanya wote, dada naona bado yupo moyoni.

Tatizo niliambiwa ni player lakini nampenda bado, naona awe tu my first guy kwenye sex coz sioni mwanaume mwingine wa kufanya nae na umri ndio hivyo unakwenda na sina boyfriend.


Sijatokea kumpenda mtu tena baada yake nisije nikafika 30's na bikira yangu. Naweza sema he is my first love coz sijawahi kumpenda mwanaume yeyote na mapungufu yake kama yeye!


*******

Dinah anasema: Mie sijambo, ahsante kwa ushirikiano.

Sasa Mrembo, kama umeamua na unataka (unaona) awe tu wa kwanza kwako, mimi nishauri nini hapo wajameni? Ila kama unataka niseme on that here we go;


Yack! Katoka kwa mtu kaja kwako, karudi kule tena yamemshinda (au bado anae) bila kinyaa wala second thought upo radhi kujiachia kwake for the name of first love? what is the 1st/childhood love do to people's lives? NOTHING so it is NOT that important/special. Mwanamke labda hupendi kuwa Bkira basi angalau jithamini.


Sio kwamba hakuna mtu uliempenda kama yeye bali hukujipa muda wa kumsahau huyo Ex au hukutoa nafasi ili kupendwa/kupenda kwa sababu ya kushikilia hisia zako kwa mtu ambae alikuwa bado na hisia kwa Ex wake.


Kitendo cha yeye kutotaka Ngono na wewe kwa miezi Sita haina maana kuwa alikupenda, was more to do with his feelings to his Ex.....alimheshimu Ex wake na sio wewe, nadhani alikutumia kupitisha muda au kumtia Wive Ex aliemrudia.


Usikate tamaa na kujishusha kiasi hicho! Hata kama hutaki kuwa Bikira by the age of 30 na hakuna mwanaume "msafi" umpendae basi bora u-pretend not to be Virgin (in your Head) uendelee na maisha mpaka utakapopenda na kupendwa ila sio huyo.


Usikimbilie kujitoa kingono kwa kuhofia kufika miaka 30 na Bikira, fanya ngono kwa sababu unataka na upo tayari, Likitokea la kutokea ni your responsibility.


Mwanamke usikate tamaa na kujitoa utu wako kwa huyo Ex, toka nje ya mzunguuko wako eeh! Tanzania kubwa sana na inawanaume wengi tu ambao hawana Mizigo ya madeni ya hisia Exes (wasafi).


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

6 comments:

Anonymous said...

Mmmmhuh! wengine wanatamani wangebaki na ubikira hadi waolewe wengine wanapanga namna ya kuuondoa!! Mimi nilidhani ungejivunia sana kwamba umemudu hadi miaka 26 umekuwa bikira kumbe tena unaichukia unatafuta mtu wa kuiondoa.

Mimi nakushauri uondoe mawazo hayo badala yake muombe Mungu akupe mwanaume wa kukuoa ambaye ataifurahia hiyo bikira na utakuwa umempa zawadi kubwa sana na atakuheshimu. Huyo mwanaume unayemuwangia nadhani hakufai kwa mujibu wa maelezo yako.Kama unajua ana mwanamke mwingine unachoendelea kukitafuta kwake nini hasa?Hebu fikiri zaidi,Dina kakushauri vizuri thamini utu wako na jikubali na lingia ubikira wako.

Anonymous said...

acha mawazo potofu dada mtunzie mmeo utae funga nae ndoa ili aje akufurahie zaidi ukimpa huyo hutamsahau hata ukiingia kwny ndoa

Anonymous said...

dada acha mawazo potofu

Kirungu said...

Chezea kupukuchuliwa wewe? He he dada kashtukia anapishana na mautamu.Chamsingi zingatia malengo yako lkn pia afya yako.Usikubali kupukuchuliwa bila mpango.After all kuolewa na bikra inakuongezea heshima kwa mumeo so think twice kabla ya kutoa hicho kiharage.Kuhusu ex kama unataka kulilia chooni mpe hicho kidudu ushajua ni player inatosha acha hata mfikiria vijana waaminifu wengi tu.

Anonymous said...

I wish nikuoe kabisa mimi ili unizawadie hiyo bikira yako uwe malkia maana kwa karne hii hiyo kitu adimu kabisa.

Anonymous said...

I wish nikuoe kabisa mimi ili unizawadie hiyo bikira yako uwe malkia maana kwa karne hii hiyo kitu adimu kabisa.