Sina raha na Ndoa Yangu!

Hi, dada Dinah,
Hongera kwa kazi nzuri ya kuelimisha watu mbalimbali hususani juu ya suala la mahusiano au love affairs.


Mimi ni mmoja kati ya wadau wa blogu yako. Nimekuwa nikisoma na kujielimisha mengi yahusuyo love na relations kupitia ushauri unaotoa kwa wengine.


Unfortunately, leo nami nimejikuta naingia katika orodha ya watu uliowashauri kutokana na ishu ambayo imekuwa ikiniumiza kichwa katika ndoa yangu. Ishu yenyewe iko hivi:


Umri wangu ni 26 years, niimeoa mwaka mmoja na miezi nane iliyopita, Mwaka wa kwanza wa masomo yangu ya Chuo. Mke wangu ana miaka 24 sasa.


Kabla ya kuoana, tulikuwa tukifanya mawasiliano nae tangu niko form 5 na tukakubaliana ya kwamba tusubiri mpaka nimalize masomo yangu. Kutokana na utaratibu wa Dini, hatukuweza kuingiliana kimwili ingawa na admit kwamba mara kadhaa tumewahi kufanya romance ambayo ni kutokana na msimamo wake tuliweza kutoingiliana.

Nilikubali matokeo na kuvumilia. Sometimes she used to call me na kuniambia anahitaji tukutane kimwili but when tukiwa wawili tu akawa anataka tufanye tu romance kwani anaogopa kupoteza Usichana wake kabla ya ndoa. I agreed with her and let things go.

Hali yangu ya kiuchumi haiko sawa coz i had no Kipato cha maana sana kama Mwanafunzi wa Chuo, ishu ya Ndoa ilileta hali ya kutoelewana katika familia yao lakini akashikiria msimamo wake kwa kuwa alinipenda mno. Upande wa familia yangu was ready to support me mpaka namaliza Chuo.

Siku ya kwanza tukiwa katika honeymoon. Akaanza kulia na kunambia hayupo tayari kukutana nami kimwili. Niliumia mno. Mara akadai anaogopa kuitoa Bikra yake. Mara akadai kuwa dada yake hajaridhika na Ndoa yake.


Nikajitahidi kumliwaza na kumbembeleza sana asiwaze kuhusu ndugu zake coz maisha yashakuwa ni yetu wawili sasa hivyo ajali maisha yetu tu. Hakunielewa. Nilihisi ni njozi tu. Nikajipa moyo na kujaribu kumsahaulisha.


Nilipoona kaanza kuwa normal tukaendelea, mara baada ya tendo lile nikawa na kibarua cha kumliwaza tena.

Kwa ajabu akaanza kunambia kuwa haitaji tena kuwa nami na akawa anadai Talaka yake. Nilidhani ni masihara tu, kumbe she was seriuos. Akawa anajibu ovyo na kwa mkato. I was geting hungry. I slaped her once.

Toka siku hiyo Ndoa yangu ikaanza kupoteza mvuto na thamani. Hakutaka tukutane kimwili akidai anajiskia maumivu. Nikakubali kuvumilia but life yangu ilianza kuyumba slowly chuoni.


I decided to pospone my studies without informing my guardians. She did not want to hear kila ninachomuelekeza. Ujeuri ukawa ndio silaha yake kubwa. Niliumia mno.

Sometimes nilijaribu kuwaeleza ndugu zake ambao pamoja na kumkanya lakini niliona dalili za kumsapoti kwa kile anachokifanya. Nilizidi kuumia.


Mpaka hivi sasa, maelewano yetu si mazuri ingawa tukiwa nje watu wanaweza kusema tunapendana. Imefikia wakati hatuongei siku nzima. Dah!


Sawa na kipato changu cha Uanafunzi bado nimekuwa nikiacha pesa ya kawaida kwa ajili ya matumizi ya ziada coz mahitaji muhimu yote yapo, but wakati mwingine nakuta pesa imetumika kwa jambo lisilo na maana. Nikiuliza naamiwa 'mwanaume nina gubu unaulizia hadi chenji?' Sipaswi kuuliza pesa imetumikaje.


Maisha yamekuwa ni ya kununiana, kujibiana mkato mpaka inafikia muda sioni mapenzi kabisa. Sioni faida ya Ndoa tena.


Nikimuelekeza asifanye jambo fulani baya leo, kesho anarudia. Anaomba samahani then anaendelea kulifanya. Hana heshima kwangu kama mumewe no matter what i am trying to be.


Hivi sasa nimepanga nihamie hosteli za Chuo mara baada ya Masomo kuanza then nimrudishe kwao akapumzike au nimpeleke kijijini kwetu akakae mpaka nimalize masomo kwanza.


Nahisi ataniharibia future yangu na ya familia yangu ingawa bado hatujafanikiwa kupata mtoto.Nahitaji kuwa free ili nipange life yangu upya.


Nahitaji ushauri wako juu ya nini cha kufanya kabla sijachukua maamuzi mengine ambayo yanaweza kumkwaza yeye na famila yao.

Nimechoka kuishi maisha yasiyo na muelekeo mzuri. Please, dada ushauri wako ni muhimu mno kwangu.

************


Dinah anasema: Hello! Ahsante sana na shukurani kwa ushirikiano.


Muhimu: Kutokana na tabia za kitoto na kibinafsi za Mkeo usifikirie kabisa kuahirisha (tena) au kuacha Masomo kwa ajili yake. Unaweza kuacha mengine kwa ajili yake lakini sio hilo.

Hapo ulipompiga kibao Mkeo pameniudhi kweli, najua kuna maudhi yanakufanya utake kumdunda mtu(mke/mume).....sipendi watu wanaopiga wenzao bila kujali Kosa ni kubwa kiasi gani! Ni vema kujifunza kuzuia hasira zako Kichwani, usiziache zishuke "mikononi" na kufanya uharibifu!!

Kutokana na maelezo yako inaonyesha ama Mkeo hakuwa tayari kuolewa na wewe ukiwa Mwanafunzi, labda alitegemea mkifunga Ndoa utaacha Masomo na ufanye kazi (uwe na Kipato Kizuri)....possibility ni kubwa anafanya Visa na Vituko akitaka kufikisha ujumbe. Hilo moja.

Pili, inaonyesha ama huko kwao wanapenda kuolewa na watu wa "aina na kipato fulani" na Dada mtu ndio kinara (tumuite Control freak) anatumiwa "kuharibu".


Pia huyo Dada mtu(shemeji yako)inawezekana ama ana wivu (kama hajaolewa/kaachika).....maana wakati mwingine Adui mkuu anaweza kabisa akawa Ndugu yako wa Damu.....sema ile "sisi damu moja hatuwezi gombana" huwa inaficha ukweli wa mambo kuonekana.

Hapo kwenye "uaduia wa ndugu" hata wewe Mume hutokuwa na namna ya kumfanya mkeo aone Uadui wa ndugu yake kwake kwasababu utaonekana wewe "mtu wa nje" unataka kuwaharibia Undugu wao, wanajuana na wameishi wote kwa miaka!, wewe umeishi na Mkeo kwa Mwaka na Nusu tu(vichwani mwao)....MUHIMU ni kumuacha yeye mwenyewe aje kugundua with time.(Usiwaingilie).


Nini cha kufanya:

1-Acha tabia ya kumuambia au kumueleza, kumbuka huyo sio Mtoto, sio Mdogo wako na sio Mwanao!


Jaribu kuwasiliana nae kwa kuzungumza nae. Mpe nafasi ya kujieleza na wewe usikilize....hoji kwa upendo nini hasa tatizo linalipolekea yeye kununa na kususa?


Mjipe nafasi ya kila mmoja wenu kumueleza mwenzio jinsi anavyojisikia....kwa mabaya na mazuri. Kitu gani kifanyike ili wote kwa pamoja muishi maisha ya amani na furaha bila mikwaruzano ya mara kwa mara kama Wanandoa?

Zungumzeni kama ninyi na sio "wewe", "mimi"......kumbuka kutokurudia issue ya Fungate na yeye kuomba Talaka (nadhani alilopoka tu kutokana na maumivu).

Zingatia issues za kununiana, kutowasiliana, kujibizana kwa ujeuri, kuitana majina mabaya...(wacha kuulizia pesa zimetumikaje....unless ulikuwa na shida nazo).


Vyovyote utakavyoongea na mkeo kumbuka kusisitiza Mapenzi yako kwake, umuhimu wake kwako na kwenye Ndoa yenu kama Familia.


2-Usihamie Hostel kwani kutakuongezea gharama, huyo ni Mkeo na kama huna mpango wa kumtaliki basi mpeleke kwenu (umemuoa ni wa kwenu sio kwao....."Mke ataacha kwao aende kwa Mumewe").

Lakini kama umefanya yote na hakuna mabadiliko na unadhani mapumziko a.k.a "trial" Talaka au "separation" itamfanya abadilike au ku-rethink basi mrudishe kwako kwa muda maalum.

Nadhani kabla ya yote niliyoyasema kuna taratibu Kidini na Kisheria(mmefunga Bomani), inategemea Mmefunga Ndoa wapi au chini ya Imani gani?.....sio lazima kuyafuata kwa mtiririko lakini ni vema kuzingatia kulingana na Maagizo ya Ndoa yenu chini ya Imani zenu.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments

Vince 69 said…
Pole sana kaka.
Kaka hapo hakuna tatizo...na "dawa ya moto ni maji" kwanini nasema hivyo??
Nionavyo mimi,mkeo anamatatizo ya kisaikolojia (japolkuwa sijui sana kubusu saikolojia,but i can view it from that vantage)Kumbuka ishu imeanza siku ulipovunja bikra yake.
Yawezekana akilini mwake,aliweka kwamba...bikra ni "kitu cha thamani sana kwa mwanamke", actually it is but pale unapompata mwenza wa maisha yako thamani yake inakuja pale unapokuwa uko tayeri kumpa nafasi ya kuitoa.
So dawa yake ni wewe kuwa positive towards her all the time. Kuwa mume na siyo kidume. Be polite, no matter anakuudhi vipi,muoneshe mapenzi no matter anakuignore vipi.
Tumia njia mbadala...mtoe out mpeleke sehemu anayoipenda...au andaa romantic dinner kwa ajili yake...alika rafiki yake au yako amabaye anamwenza wake na wanapendana. Wakiondoka mwonyeshe jinsi gani mnavyotakiwa kuwa kama wao na si kufarakana. Jaribu kuzungumzia na kukumbushia urafiki wenu zamani.
Mpe vitu ulivyotunza ambavyo amewahi kukupa ama kukutumia (kama vipo)
Kila binadamu anabreaking point yake, na i promise you "Itafika tu", na ataanza kuchange mwenyewe.
Zingatia sana masomo....ondoa hisia za postpone shule.
Hii ni vita ya kisaikolojia..usiipigane kihisia (hasira) wala kimwili (kumslap)
Pole sana,yupo pamoja!!
Anonymous said…
pole sana ndugu fanya kama mtoa comment wa kwanza alivyosdhauri, naamini atabadilika tu. Zingatia masomo.
Anonymous said…
Nawashuru sana wachangiaji wote wawili kwa busara na hekima zenu. Nimejifunza vya kutosha kupitia majibu ya Dinah na michango yenu kimawazo kwani ni jambo nililokuwa nikilitafuta ili niweze kuinusuru ndoa yangu ambayo bado ni changa. Nimeanza kuchange slowly how i handle my marriage. Thank you all in advance....