Friday, 18 July 2014

Mimba ya Mume wa Mtu, Mama hanielewi.

Shikamoo Dada, pole na majukumu. Mimi in msichana mwenye umri wa miaka 22, naishi marekani na familia yangu nikimaanisha mama na ndugu Dada yangu. Nafanya kazi kama server kwenye restaurant maarufu hapa nchini.

Tatizo langu nilijishirikisha kwenye mapenzi na Boss wangu ambae pia ni mume wa MTU ni baba mwenye umri sawa na baba yangu japo muonekano wake na umri ni tofauti anaonekana mdogo.

Tokea tumeanza mapenzi ni muda usiopungua  miezi minane.  Familia hawakumkubali lakini kutokana na kuona ni furaha yangu ikabidi wajilazimishe hivyo hivyo. 

Wiki iliyopita nilikuwa naumwa hali iliyofika hadi kuhisi kizungu zungu na kutaka kuanguka kazini ndipo boyfriend wangu aliponipeleka Hospital, baada ya siku tatu nikaambiawa nina matatizo ya upungufu wa damu  nisipokuwa makini Anaemia inaninyemelea na kingine ni kwamba nina Ujauzito.

Hapo ndio nilipochanganyikiwa zaidi. Maana Mimba ni ya mume wa mtu japo mwenye yupo willing kuilea ila anahofia mkewe akijua sitakuwa na amani. Pili kuitoa huku inaruhusiwa kisheria ila anahofia nitaharibikiwa Kisaikolojia.


Ukija kwetu mama hajafurahia hata kidogo kwani miezi mitatu iliyopita Dada yangu alipata mimba hali iliofikia kutibuana na mama na kuamua kuhama nyumbani kwenda kwa bwana wake kwa maana alikataa kuitoa.

Sababu ikiwa ameshatoa mimba mbili kabla hivyo kuitoa ya sasa hataki kabisa. Hivyo kahama in kufanya mama kuchanganyikiwa na kunionya Mimi nisije nikafanya kama Dada yangu.


Hapa sasa hivi niko na mawazo mpaka nawaza mabaya. Kuitoa naogopa nitakufa ama kitu kibaya kitatokea. Pia nawaza kama nikiitoa Dada yangu akizaa nitazidi kuumia maana mtoto wake atakuwa ukumbusho wa kwangu.

Pia naanza Chuo Fall (September ) so kusoma na Ujauzito sijui kama nitaweza. Kiufupi Dada yangu nipo kwenye dimbwi la mawazo.

Dada yangu kaniambia nitulie kwanza na kufikiri nini nataka. Lakini still naona wazimu unataka kunijia. Silali vizuri, mama yangu haongei na Mimi. Ndipo nimeona  nikwandikie wewe labda msaada wako wa mawazo  unaweza kunikwamua katika hili dimbwi la mawazo.

nitafurahi kusikia majibu yako either kwa email au blog yako.

Ahsante.


************


Dinah anasema: Marhaba mrembo, pole kwa yote ila ungekuwa karibu ningekusema mpaka Mimba itoke....(Natania)! Ila kwanini? Jamani kwanini at 22 unachanyanga maisha yako kizembe hivyo?!!!

As if mume wa mtu haikutosha ku-mess up maisha yako, ukaamua kujiachia kabisa na kushika Mimba!! Mama hakukufundisha namna ya kujikinga dhidi ya Mimba?

Haijalishi muonekano wake wala umri wake, Mume wa mtu ni Mume wa mtu tu hukupaswa kumpanulia Miguu...end OFF!....well limetokea, let's deal with it.

Wewe sio Dada yako so option ya kutoa Mimba achana nayo na mimi sikushauri uitoe kwasababu siamini katika kutoa Mimba bali naamini katika kuzuia kushika Mimba.

Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa ulikuwa unataka kuzaa na mume wa mtu alikuwa easy target, hivyo hakuna cha "tulia uangalie unachokitaka".....unamtaka mtoto then keep him/her....utamtunzaje? Ulipaswa kujiuliza kabla hujafanya Ngono bila Kinga.

Kuna uwezekano mkubwa huyo Boss Mume wa Mtu boyfriend wako ama akakuachisha kazi ili kulinda Ndoa yake, kama alivyokuonya kuwa Mkewe akijua utakiona cha MTEMA KUNI. Hilo moja.

Pili, akasema yupo willing kumtunza mtoto, hiyo sio guarantee ya yeye kufanya hivyo bila mkewe kujua hivyo anaweza kuamua kukuchunia tu ili aendelee kulea familia yake.

Muhimu ni wewe mwenyewe ku-sort things out na Mama yako ili angalau uwe na mahali pa kuishi kwa Muda na ujiandae kuwa a single mother (kwa UK is a bonus maana single mother wanamisaada kibao kifedha hihihihihi sorry).

Kama nia ipo na umekamia unaweza kabisa kusoma ukiwa Mjamzito(kama mimba haitosumbua), lakini kama hujiamini kuweza kufanya hivo basi badilisha mipango na uanze shule Next Sept utakapo kuwa umejifungua (Mungu akijaalia).


Sasa mrembo fanya hivi; Umekwisha haribu na matokeo unayo, hakuna haja ya kuwaza na kuwazua ufanye nini (too late), Simama kama mwanamke na angalia mipango ya Chuoni ili ubadilishe mwaka/tarehe ya kuanza.

Angalia Mkataba wako wa kazi unakulinda vipi au unalinda vipi Wajawazito na Wazazi (waliojifungua)....soma Sheria za Kazi za hapo ulipo ili ukifukuzwa kazi uweze ku-sue Boss wako(sio bf) kuwa kakufukuza kazi kwa sababu ya Ujauzito....sijui US sheria zilivyo ila nadhani hazitofautiani sana na za hapa (UK).


Usimwambie mtu yeyote kuhusu mipango yako ya ku-sue ikitokea umefukuzwa kazi(iwe between mimi Dinah na wewe).

Nimejaribu kuwa mpole ili nisikufanye ujione mpweke, lakini nina hasira sana na wewe, zaidi ya Mama yako.


Kua mwanamke Imara, Soma, piga kazi, lea mwanao.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

2 comments:

Anonymous said...

Pole Mdogo wangu kwa yaliyo, sikusapoti kwa ulichokifanya ila ni nafasi ya changamoto pekee. Kumbuka kupata mimba sio mwisho Wa dunia , sikiliza aliyokuambia Dada Dina na uyafuate kama yanaendana na situation yako. Ni hivi Mimi pia Niko marekani weka contact yako ya email nikutafute kwa kuwa unahutaji MTU Wa kuongea nae . Elewa Hiki kipindi si cha kujilaumu Bali Wa kusolve hiyo issue. Mimi sikuruhusu utoe huo ujauzito kabisa. Huwezi jua Je kama mungu amekupangia kiumbe hicho hicho. Mfano mzuri unamuona Dada happiness magese anavyoteseka, na si kwamba anapenda no, anatamani sana kuwa na Mtoto ila ndio hivyo afya haimruhusu hebu nipe contact zako nikutafute . Kila la heri!

Anonymous said...

pole sana kwa tatizo lako mrembo.. ua my age mate & nami nliwahi pata tatizo kama lako bt unfortunatly mimba'angu ikatoka ktk wiki ya 6 kwa 7bu ya stress.. unahitaji kuwa makini sana, stress, frustation + anaemia vitaleta matokeo mabaya sana kwako na kwa mimba yako.. unahitaji ku2lia na kuangalia unajisaidiaje pia rejesha uhusiano na mama hyo itakupa amani then achana na mume wa m2 coz hana future na wewe.. unaweza postpone chuo ukaanza mwakani km tatizo la anaemia halitojitokeza tena, kula sana matunda na mboga za kijani(kila siku kama utaweza).. epuka sana kutumia vinywaji vyenye preservatives, natural juices zitakuwa best option kwako.
KUMBUKA: USITUMIE DAWA PASIPO USHAURI WA DAKTARI..