Thursday, 31 July 2014

Haonyeshi kuumia baada ya kumuacha...

Habari dada dinah, pole na kazi pia hongera kwa kuelimisha
jamii.


Nimekua nikifatilia sana blog hii na kujifunza mengi, ila leo na
mie yamenikuta
(kabla ya yote kwanza naomba ulihifadhi jina langu).

Mimi ni Kijana wa Kiume mwenye miaka 22 nilivyoanza
chuo mwaka jana nilikutana na Msichana ambaye sijawahi ona!! inshort
nikampenda na nilichukua muda kumchunguza kama anatabia nzuri na
nikagundua kua anatabia nzuri na anafaa.


Tukaanza mahusiano ya kimapenzi na huu ni mwezi wa Sita ila
hatujawahi kufanya Ngono kwa sababu huwa anaogopa sana kwasababu hajawahi kuguswa.

Nimevumilia yote lakini sasa akaanza kuonyesha kutokunijali kama
mwanzo na hanitreat kama mpenzi ila kama rafiki nimemwambia
abadilike mara nyingi lakini hanielewi.


Mara ya mwisho wiki iliyopta
nikamuuliza mbona unanipa mapenzi nusu nusu akanambia kwasababu
haniamini! Nilishangaa coz najua anauhakika asilimia mia kua yupo peke
yake akaongea na mengine mengi yakuniudhi.

Some time anaenda kwa marafiki
zangu anakaa mpaka masaa mawili huko...pia fb na whatsapp
anachat muda mwingi na hufanya hivyo wakati nikiwa nae.

Kiukweli heshima yangu hanipi kama
mwanzo tena, sasa nimeamua kumuacha ili nipunguze hizi stress na maumivu coz nampenda mpaka nimepitiliza.

Tangu nimemuacha haonyeshi dalili za
kuumia wala kujali wakati mimi nazidi kuumia. Hii ni mara ya pili kumbuka niliamua kumwacha baada ya kuchoshwa na stress zake ila nampenda na natamani
hata arudi tena tuendelee na mapenzi. Nifanyaje???


Dinah anasema: Salama kabisan ahsante na shukurani kwa ushirikiano.

Dogo una asili ya u control freak eti! Kabla hujaanza uhusiano ukamchunguza kwanza, uliporidhika ndio ukaanzisha uhusiano nae.....ndani ya Miezi sita una demand msichana afanye mambo ka' Mkeo na umemuacha mara Mbili in 6months kwasababu hafanyi utakayo.

Unataka akuheshimu vipi? Ikiwa hakutukani mbele za watu au kukukebehi mbele ya ndugu, jamaa na marafiki as Gf atakuwa anakuheshimu....au unataka asikae na rafiki zako au asi-chat na rafiki zake kwenye Mitandao?


Ikiwa wewe unamiaka 22 ni wazi yeye ataluwa hivyo au mdogo zaidi, katika hali halisi Wasichana wadogo ndivyo walivyo....bado anajitambua, anajifunza mambo kama Binti anaeelekea kuwa Mwanamke, anapenda kuzungumza na marafiki na kujenga uzoefu na watu mbali mbali.


Nadhani ama umeaninishwa mambo kuhusu mahusiano ya kimapenzi ambayo ni tofauti na hali halisi ya Maisha au umejiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi bila kujua uhusiano wa kimapenzi ni nini hasa!


Huwezi kumtawala Binti wa watu kwa jinsi ulivyoelezea na yeye kuendelea kutaka kuwa na wewe kama Mpenzi wake.....inawezekana hapendezwi na tabia yako ndio maana ameamua akufanye uwe rafiki tu.

Nadhani timing ya wewe kumuacha ilikuwa mbaya, umemuacha wakati yeye tayari alikuwa kakuweka kwenye "friends zone" hivyo hakupata au hapati maumivu ya kuachwa kama mpenzi(hana habari).


Kama kweli unampenda na unapenda akurudie basi ni vema kubadilika kwanza halafu ndio ujaribu kumshawishi tena kwa kuomba msamaha na kumhakikishia kuwa hutokuwa ukimtawala.

Akikubali kurudiana na wewe unatakiwa ku-relax na kumuacha awe huru kuzungumza na wenzake iwe mitandaoni au vinginevyo ailimradi tu havuki mipaka.

Akikataa basi nadhani ni vema umuache aendelee kuwa yeye na kujifunza who she is kama msichana na wewe zingatia Masomo na huko Mbele utakutana na mwingine na kuanzisha uhusiano mwingine.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

3 comments:

Anonymous said...

Kijana miaka 22, na mwaka wa kwanza chuo, tayari umeishaanza kuchanganyikiwa na mambo ya mapenzi!! Mimi naona ni hatari sana kwani utapoteza mwelekeo wako wa maisha na masomo kwa ujumla. Mapenzi ni sumu kali sana katika maendeleo ya mtu siyo ya kuyaendekeza hasa katika uchanga wako ulio nao. Ndio maana hata unashindwa kuya-control. Kama Dina alivyokushauri jitahidi sana ujiepushe na hizo stress. Huyo msichana sidhani kama hakujali, nadhani yuko makini zaidi namna ya kuyakabili mapenzi.Na hapo yupo katika hatua za kujifunza na kuchunguza siri za mapenzi zikoje na mtu unayeqweza kujenga naye uhusiano anaweza kuwa ni mtu anayejua nini hasa katika angle hiyo.

Hebu sasa zingatia masomo achana na huyo binti ili naye apate nafasi ya kuyaangalia mambo yako ya msingi. Ipo siku wote mtakapojitambua mtakutana tena na mtayafaidi bvizuri mapenzi mkiwa mumejiridhisha kuwa mnajua kitu mnatafuta katika anga za mapenzi.

Anonymous said...

Wadada wa chuo ni watu wa kupenda starehe,mavazi, vipodozi na vyakula vizuri ndio maana wengi huishia kujiuza ili wakidhi matakwa yao.


wewe kijana umri 22 unajiingiza kwenye moto wa gesi utaweza?


bila shaka unahudumiwa na walezi/wazazi ambao pesa zao ndio unafanyia zinaa. ungekuwa karibu ningekutia bakora wewe dogo, utakufa na ukimwi hebu wahurumie wazazi wako.


mapenzi utayakuta na utayaacha.

Anonymous said...

Why lov? Dada dina, hiv na enzi zile baba zetu waliish hiv? Dogo achana nae kama ukimbembeleza akikataa. Dunian si kwamba yeye yupo kwa ajili ya kupendwa tu. Atapenda one day yes atakukumbuka. Wasichana wa chuo huwa wananamna fulan ya kutaka usawa na maisha ya kwenye movi ambayo baada ya chuo mtaan huwez kuyaona. Na kama anataka aheshimiwe kama mwanamke na jamii ya kiafrica, basi ni lazma ajiheshim na amheshim yule anaempenda wa kuelekea kuish pamoja. Acha utamadun wa mataifa ya magharib na wa kwenye movi wauishi wauwezao, Jikaze dogo, ipo siku utapata mwanamke halisi na mwenye maadili ya kitanzania. Kila la heli.