"Hanitamani" sababu ya ku-Flirt Mitandaoni...

Habari dada, mimi ni kijana wa kiume na nina umri wa miaka 30 nina mke wa miaka 28 na mtoto wa miaka 3.


Kwenye ndoa yetu na Mke wangu kuna vitu vya hapa na pale ambavyo vinaniumiza kichwa kutoka kwa mwenzangu ambavyo ni; mara nyingi sana mimi ndiye naomba kufanya nae mapenzi sikumbuki mara ya mwisho ni lini yeye amenianza.

Mara nyingine tunakaa mpaka mwezi mzima kila nikimwomba anasema hajisikii, pia mara nyingi sana tukifanya mapenzi Uke unakuwa mkavu matayarisho tunayafanya ya kutosha tu.

Mke wangu anapenda sana kuchat kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba nishawahi kufumania mpaka chat za kimapenzi akaniomba msamaha!!

Nina mpenda Mke wangu naomba msaada kutatua hayo mambo.


***********


Dinah anasema: Habari ni njema kabisa, ahsante! Shukurani kwa ushirikiano.


Hivi mpaka karne hii mtu na mkewe wanaombana kufanya mapenzi? Kumuomba mpenzi wako kufanya mapenzi huoni inaweza kukata "stimu" eti? (Labda ni mimi tu).

Si wanawake wote wanapenda kuombwa tendo, wengi hupenda iwe spontaneously....kwamba yupo jikoni, unamnyemelea kwa nyuma kisha unaaza kunshika maeneo apendayo ambayo yatamfanya ajisikie kupendwa na nyege at the same time...kwa mfano:


Au mpo chumbani kisha unamnyanyua na kumuweka kitandani kisha unaufanyia mwili wake "shughuli" ili ajihisi kupendwa, kuvutia na wakati huohuo Nyege na mengineyo....sio "mama Kadala nipe haki yangu"....au "mke wangu naomba basi leo" au unaama usiku wa manane na kumgeuza tu kisha uingie kama yeye ni chombo cha kuondolea hamu zako n.k.


Pia ni vema utambue kuwa sio wote wenye kupenda "kulianzisha", hii ni kutokana na kuaminishwa kuwa mwanamke kumuanza mwanaume kitandani ni Umalaya* lazma Mwanaume akuanze kisha mwanamke kutoa ushirikiano (inategemea na Mazingira aliyokulia). Pia wanawake hulianzisha mara kadhaa kwa mwezi pale anapotaka Tendo(anapevusha kushika Mimba), hawezi kulianzisha kila siku mpaka umnyegeshe kwanza. Zingatia mzunguuko wake wa Ngono.


Ikiwa unapenda Mkeo "alianzishe" basi ni vema kuzungumza nae na kumwambia "najisikia kupendwa ikiwa mke wangu unaonyesha kunitaka kingono, unanipa dalili kuwa unanihitaji kimwili"....kwa mfano!


Nadhani kuna uwezekano Mkeo alikuwa ana-cheat kihisia (hashiriki kimwili) na hao anaochat nao lakini kitendo cha kuchat maswala ya kimapenzi/ngono (flirtation) kunaweza kumfanya Mtu akose hamu na Mume/Mke wake kwani yule au wale anaochat nao wanaonyesha kujua kumridhisha mwanamke/mwanaume kuliko Mume/Mke wake.


Hali hiyo hupelekea mhusika kutaka kufanyiwa yale anayoambiwa au chat about na watu hao lakini anashindwa kumuambia mwenza wake na hivyo anaishia kukukwepa. Jitahidi kuwa mbunifu kwenye ufanyaji mapenzi na muulize anataka kufanyiwa nini na kisha boresha...sio kurudia yake yale kila siku, Mkeo anakuwa-bored....hasa kama ni mama wa nyumbani.


Hali hiyo ikiendelea basi Mume/Mke hupoteza kabisa hamu/matamanio na mwenza wake na hivyo kutegemea kuridhika na chat za hao anao-flirt nao kwenye mitandao.

Baada ya kugundua kuwa ana-cheat (flirting online/via texts IS CHEATING) na yeye kuomba radhi, wewe kama Mumewe ulipaswa kuweka "rules" kwenye Uhusiano wenu au kumpiga marufuku kabisa kujihusisha na Mitandoa na aweke muda wake na attention yake kwenye maisha yake halisia ambayo ni familia yake(wewe na Mtoto).


Badilisha au boresha namna ya kumtaka mkeo kimapenzi, badala ya kuomba....tumia vitendo kama nilivyogusia hapo awali. Pia ni vema wewe na mkeo mkawa wazi kingono ili kila mmoja wenu aweze kumridhisha mwenzio bila kujali nani "kalianzisha".


Kufanya mapenzi sio Mashindano, sio Kazi, hivyo sio lazima yeye afanye jambo kwa vile wewe unafanya kila siku.....ukianza kulinganisha ni wazi utakuwa unachukulia suala zima la kufanya mapenzi kama Kazi au Mashindano.


Kwenye Ndoa/Uhusiano wenu kuna ukosefu wa Uaminifu, Ushirikiano na Mawasiliano.....ili msipoteze Ndoa yenu ni Muhimu mkaboresha hayo mapema.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments