Wednesday, 25 June 2014

Penzi pasipo Penzi

Pole na kazi na Mungu akusaidie kwa kuendelea kutusaidia, nina miaka 24 na ni Mwanafunzi wa Chuo. Nimeanza  kujihusisha na masuala ya relation  nikiwa na miaka 22,nimekuwa na mahusiano na watu wawil tu!

Wa kwanza nilipokuwa nimemaliza Form 6 lakini sikumpenda na nilimwambia akanisubiri kama mwaka mzima nimpe jibu langu.

Wapili nikiwa nae mwaka wa kwanza naye sikumpenda na nilijitahidi lakini wapi na pia hakuwa mwaminifu katika mazingira fulani.


Sasa nimehisi kwa mara ya kwanza kumpenda mtu kutoka moyoni kabisa yaani hata nikilala nataja jina lake. Nimefanya kila juhudi kufikisha hisia zangu kwake lakini wapi!


Imefikia mahali nikawa kama nachanganyikiwa, lakini yeye hana hata mpango na mimi.


Nikamtumia rafiki yangu ambae anafahamiana na huyo Kijana ninaempenda kwa bahati nzuri nikapata namba yake. Ikapita miezi kadhaa nikijipanga nitaanzaje kuwasiliana nae.

Mwanzoni mwa mwaka nikamtafuta na tukawa tunawasiliana. Muda mwingine anaonyesha hisia za kunipenda lakini asilimia kubwa ndio hivyo anani-humiliate.

Hivi karibuni aliniita niende kwake! nilikuwa MP nikafika tukasalimiana tu nikageuza kurudi Chuoni. Baada ya hapo ndio kabisaa akakaa kimya hata hakuniuliza kama nimefika salama wala nini? kwa kuwa nampenda hata sikuona tatizo.

Nimekaa kama siku tatu hivi, nikamtext nikimwambia "ukimya wako unaniua" akanijibu "achana na mimi endelea na maisha yako", niliumwa wiki nzima nikiwaza hayo maneno napiga makelele napata maluweluwe.


Nikamwambia hali yangu lakini hata hakujibu. Baada ya kupona nimempigia simu lakini hapokei nikapiga kwa mtu mwingine anajibu "achana na mimi". Yaani naona kama nakufa.

Nikajitolea kwenda mpaka huko aliko lakini mtu wapi! Dada kinachoniuma mwanaume hana hata huruma.

Mpaka nimeshauriwa na Mwanasaikolojia sasa nimepona niko ok, ila nimefika mahali sitaki mpenzi wala mapenzi kutokana na kunyanyaswa kihisia.

Nikijiangalia mimi so mbaya wengi sana wananipenda wako tayari kunioa ila ninaempenda hana mpango na mimi nifanyaje?

Siko sahihi nimempenda sana na nampenda nifanyaje dada angu? Nimekulia malezi ya Kidini, sina uzoefu wa kumconvince hata.


***********

Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa ushirikiano, Mungu atusaidie sote.

Oh baby girl! Umri wako bado unatafuta kujitambua na kutambua hisia zako kama mwanamke. Ni umri unaochanganya sana wakati mwingine(kwa baadhi ya watu), lakini ni mpito tu.

Wanawake hatukuwa "programed" kukabiliana na "rejection" kama wanaume, ndio maana Mwanamke hawindi bali anawindwa....Mwanamke unapoamua kuwinda hakikisha hakuna kukataliwa kwa maana kwamba unauhakika na hisia za mwanaume husika kwako....sio kubahatisha kama wanaume wanavyofanya wakati mwingine.


Kuna namna/mbinu ya mwanamke "kumuwinda" mwanaume ili kujua kama ni single, kama ndio je "atakukubali" Kiswahili wanaita "kujitongozesha".


Kwamba unatumia mwili, Macho, maongezi(hutongozi bali unapiga interesting stories) n.k ili kufikisha ujumbe. Ukianza kuona dalili za jamaa kuingia "mtegoni" ndio unamtokea.....hii yote ni kujiepushia Maumivu ya kukataliwa.


Najua ni ngumu sana tena sana lakini inawezekana....itabidi umuache aende kwani kesha kuambia "achana na mimi, endelea na maisha yako" hayo ni strong words & serious, usikute tayari ana Mke au Mchumba.

Nadhani ni Kijana mwema kwani hakutumia nafasi uliyompa na kufanya ngono na wewe kisha kukuambia "achana na mimi, endelea na maisha yako"....ungejichukia, ungejiona Mchafu kuliko!!

Hakuna namna ya kumshawishi ili akukubali....lazima kuna sababu ya Msingi na muhimu kwake kwanini hataki kuwa na wewe, kama nilivyosema inawezekana na commitment kwa mtu wake.


Jitahidi kumuondoa akilini au ku-switch off kuwa hayupo, yaani ha-exist hapa Duniani ili uweze kuwa na amani na kuendelea na maisha yako na utapenda na kupendwa na mtu mwingine.

Itakuwa rahisi kwako kwasababu hujawahi kuwa na uhusiano nae lakini itachukua Muda. Muhimu ni kuifunza akili yako yako kuweza kudharau, kusahau na kukubali kuwa Penzi halilazimishwi.


Jipe muda wa kutosha ili uweze kuipa akili yako nafasi ya "kujifunza" niliyoyataja hapo juu. Inaweza kukuchukua Miezi Sita mpaka Mwaka hivi then utakuwa sawa, utakuwa tayari kupenda na kupenda.

Hope maelezo haya yatakupa mwanga na uelewa kiasi ili uweze ku-focus kwenye Masomo na mambo mengine Muhimu maishani zaidi ya mapenzi(kwa sasa).

Furahia maisha yako kama Mwanamke, heko kwa Ujasiri wako na Uwazi wako.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

1 comment:

Anonymous said...

Shikamo dada,ahsante kwa ushauri nitaufanyia kazi..ubarikiwe.