Monday, 2 June 2014

Kutoka Mpenzi to Rafiki....

Nilikua na boyfriend wangu tulilkaa vizuri tu kama miezi mitano hivi lakini hakuwahi hata kunibusu wala kuongelea mambo ya Ngono.


Ni mtu wa Dini hivi, sa siku moja tukiwa out nikasema nimjaribu nikamwambia naomba nikukiss na nikihug, alishtuka akasema ni mapema, basi akanirudisha nyumbani.


Cha ajabu kuanzia siku hiyo akanichunia hapokei simu wala kujibu sms. Ikabd niwe mpole, baada ya miezi kama Nane hivi akaanza kunitumia sms za kunisalimia na mimi nikawa narespond bila kuonysha knyongo.

Baada ya Wiki mbili tangu mawasiliano yaanze upya akaanzisha topic ya utaniutani tu wakati tunachat maana ni kama rafiki sasa. Akasema kuwa anatamani kuwa na mtoto, na mie nikamjibu hata mimi natamani mtoto unaonaje ukinipa mmoja?


Duu si akauchuna tena hadi leo ni wiki mbili sasa kauchna. Kiukwel Dinah nampenda huyu jamaa na natamani anitangazie Ndoa ila sasa sielewi nitafanyaje maana ana misimamo yake ambayo inanipa vikwazo mie kumsogeza karibu kimapenzi.

***********


Dinah anasema: Hello there! uelezeaji wako mzuri (unavutia kusoma) hasa pale "duu si akauchuna tena".....usijali kichaa mie!


Nadhani kuna kutokuelewana kati yako wewe na huyo Kijana, kwamba yeye anataka urafiki ili mfahamiane kwanza kabla ya kujikita kwenye "Mapenzi ya Mwili" na wewe unataka kwenda moja kwa moja kwenye Mapenzi.

Katika hali halisi miezi Mitano ni muda mfupi (kama mnakutana mara mbili kwa wiki).....hasa ukizingatia ni MwanaDini.

Kitendo cha wewe "Mwanamke" kulianzisha kimemtisha....yeye ndio mwanaume na pengine alidhani kuwa umechukua nafasi yake.


Kumbuka sio wanaume wote ambao wanakubaliana na "usasa" wa wanawake....kwamba hata mwanamke anaweza "kulianzisha"(well mie na usasa wangu walaa nisingethubutu....hehehehe 1st time ni nafasi na mwanaume atiii).

Nadhani kujiamini kwako na kuomba Busu na Kubato kulimtisha na kuhisi "huyu mwanamke vipi" ikabidi ajipe muda.


Tangu unajua ni mpenda Dini, alipokuja na utani wake wa kutamani mtoto, ungemwambia...."Hata mimi natamani mtoto, lakini nasubiri mpaka nitakapofunga ndoa"....ingemrudishia imani. Jibu lako lilimtisha....ni kama vile unataka kuzaa kabla ya Ndoa wakati Imani yake hairuhusu....sijui umenielewa.


Pamoja na kuwa unampenda lakini usipokuwa Makini utakuwa unapoteza muda wako kusubiri Jamaa ambae huna uhakika kama atakuwa na wewe kimapenzi au la, na hata ukiwa nae utaweza kuishi maisha ya Kumpendeza huyo anaemuamini kama ni Mungu au Kanisa n.k?.

Kwasababu hakuna uhusiano ni vema ukamuambia wazi unavyojisikia....na ku-demand kujua msimamo wake kwako...je tuendelee na urafiki tu au mtegemee mapenzi out of urafiki?


Akijibu urafiki basi mchukulie kama rafiki na umuache kama alivyo na ufunge Mlango wa mapenzi kwake. Kisha ufungue mlango wa pili kwa ajili ya mtu mwingine utakaependana nae.


Tangu hamjaonana mkiwa watupu then mnaweza kabisa kuwa mafariki hata kama ukipata Kijana mwingine.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

4 comments:

Anonymous said...

Du wewe binti nimekupendaje japo sijakuona hata kwa sura?? Yaani binti muwazi na mwenye uhuru kiasi hicho mimi namzimia haswaaa. Huyo jamaa yako siyo dini wala nini, anakuzuga tu. Angekuwa mwenye dini angekuwa karibu nawe kukusomea kurani au bible kama kweli anakupenda asingekimbia miezi nane bila mawasiliano. Msome vizuri kuna kitu kinamzingira. Ikiwezekana hebu weka contacts zako hapa mimi niwasiliane nawe maana nimevutika sana nawe naona unaweza kuwa mke wa kunifaa.

Anonymous said...

subira yavuta heri my dia

Anonymous said...

Heee dada huyo jamaa gundu kabisa huyo haisimami kabisaaaaaa hebu chukua muda kumsoma vema. Mchangiaji hapo juu ameomba contacts zako hebu mpe uone kama anapenyeza hapo.

Anonymous said...

Hahahahahh Huyo Jamaa Mambo Yake Yanachekesha Kama Mr.Bean. Yan Anakataa Kutia!! Itakua Hadindi huyo Bila shaka