Tuesday, 13 May 2014

Mke wa Pili, hanijali kwa hela wala penzi.

Habari dada Dinah, pole na kazi na hongera kwa kazi unayoifanya.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka kadhaa, nimeolewa ndoa ya mke wa pili na mume wa kiislamu huu ni mwaka wa pili sasa.


Tumezaa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka minne sasa. Cha kushangaza dada Dinah sitambuliki kwao mume wangu na wala mtoto wangu hajulikani.


Ndoa yetu ilikuwa ya siri hakukuwa na sherehe yoyote zaidi ya Sheikh tu na mashahidi aliokuwa amewatafuta huyo Sheikh.

Hela ya matumizi ni shida na hata haki ya Ndoa kama mke mimi siipati kwasababu halali kwangu na hata kuja ni kwa kubeep tu.

Sasa naomba ushauri huyu mwanaume ana malengo na mimi kweli au ananipotezea wakati na kunizibia rizki mimi.


***********

Dinah anasema: Nashukuru na ahsante kwa ushrikiano.


Sasa mrembo mbona jina lako la Kikristo ilikuaje ukakubali kufunga Ndoa ya Kiislamu achilia mbali kuwa mke wa pili kwa siri!!....Au ulilazimisha ndoa baada ya kuzaa na huyo Mume wa mtu?


Kutokana na maelezo yako nadhani wewe ni Kimada wa huyo Mume wa mtu, sio mke wa pili kwake kama ulivyojiaminisha.


Kufungishwa Ndoa na Shekhe haiweki uhalali wa Ndoa yako ikiwa taratibu nyingine hazikufuatwa. Pia kutokana na Ugumu wa Maisha wengine wala sio Mashekhe bali "wafanya biashara".


Sizijui sheria za Dini ya Kiislamu lakini nadhani kabla ya kufunga Ndoa Mke mkubwa na watoto wa ndoa ya kwanza hupewa taarifa na kuna sheria lazima zifuatwe.


Pia mume mtarajiwa huenda kwa mwanamke kuposa na kufuata taratibu zote muhimu za Uchumba.

Mara nyingi Wake wenza huishi nyumba moja au mahali pamoja, na ikitokea mahali hapatoshi au mke Mkubwa hataki ukae nae basi mke mdogo hutafutiwa mahali pengine.


Mume "wenu" hujigawa "sawa sawa" bila upendeleo kwa wake zake wote. Mke mdogo hujulikana kwenye familia nzima mpaka wale wa ndani ndani kule (wasio na uzito).


Sasa kama mwenzangu hayo yote hayapo na Ndoa ilifungwa kwa SIRI bado unaamini tu kuwa wewe ni Mke wake na sio Kimada?!!


Kwabahati mbaya sidhani kama kuna Sheria inayokulinda ili kupata "matunzo" kwa ajili ya mwanao. Huwezi kwenda Mahakmani wala Ustawi wa jamii kuomba msaada kisheria kwasababu huwezi kuthibitisha uhalali wa Ndoa yako.


Labda kama una Cheti cha Kuzaliwa chenye jina na sahihi ya Baba'ke mtoto, ila mzunguuko wake lazima ukate tamaa (kutokana na nature ya uhusiano wako na Mume wa mtu).


Usijutie kosa lako ila ujifunze kufunga miguu mbele ya wanaume wenye wake na familia zao in the future, Uislamu sio sababu ya kumkubali Mume wa mtu hata kama wanakuahidi Ndoa, kataa.


Kosa kubwa ulilofanya ni kuzaa na huyo mwanaume, matokeo yake mnamtesa mtoto ambae hakuomba kuzaliwa na mume wa mtu ambae sasa ni baba yake au wewe.

Hakupotezei Muda bali ameisha kupotezea Muda wako, hakuzibii rizki (hakuna mwanadamu anaweza kukuzibia rizki), nadhani kagundua familia yake na mkewe wanaumuhimu zaidi yako ndio maana anabeep au kuna Mke wa tatu wa siri huko kwingine.

Hama hapo ulipo, tafuta kazi au shughuli ya kukuingizia kipato.....mwanzo utakuwa Mgumu sana lakini ukisimama kama mwanamke na ukajitahidi utafanikiwa tu.


Baada ya kukaa sawa na mtoto kakua then unaweza anza kutoka tena, zingatia ulichojifunza kutokana na kosa lako la mwanzo.


Utakapo anza kutoka tena na mwanaume hakikisha hana familia na pia usikimbilie kuzaa, tumia kinga kwa faida yako na mtoto wako.

Mtoto akikua atamtafuta baba yake....(Kama atataka hilo litokee).

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

4 comments:

Anonymous said...

dada ushauri uliopewa sio mbaya ila Mie tu na Nakufahamisha kitu 1. Wewe ulipoolewa umeingia kwenye uislamu kwajili ya Mume au uislamu umeupenda kwa mapenzi ya dini? Msipende tu mwanaume na kuingia kwenye dini Kumbe huwapendi dini umependa Mume hayo pia hayafai, 2. Kama kweli umeingia kwenye dini fata wanaojuwa dini watakupa ushauri Mzuri sana kwa sheria za dini na mumeo mnavyoishi naye. Haya ninayo yajuwa Mie na dini ya kiislamu kwa mafunzo ya mtume Muhammad kumbuka mtume haabudiwi yeye ni mtume tu na ni mwalimu anayeaabudiwa ni mwenyezimungu so haya ni katika mafunzo mtume alifundisha Ummah wa kiislamu kuhusu Mke akiona anazulumiwa. 1. Kasema mwanaume lazima a hakikishe Mkewe hatuongelei wasioolewa hao kwenye zina Mwanaume Kama hamfikiishi mkewe mke anatakiwa a mfahamishe mumewe asikae kimya na Kama halijawezekana mke a kaona kwenye sex anazulumiwa hamfikishwi ikatokea Mume hamsaidiiki hata kwa dawa basi Mke Ana mawili Kubaki na Mume au Kama ataona anazulumiwa mahitaji anauhuru wakudai talaka nakujitoa kwenye ndoa mwanamke 2. Kuhusu wake wenza ndoa yako inaweza Kuwepo ila uliza bakwata vizuri ila tu Kiislamu Mume hajafanya haki amefanya Zulma 1. Anatakiwa ku kutoa kwa Baba yako mzazi mbili akufahamishe kwa wazazi wake na la 3. mwanaume sheria hata akiwa na wa 4 kila mmoja wenu anatakiwa aje kwenye nyumba kukaa siku tatu(3) mfululizo na kwa mwengine 3 asipofanya Hivyo kavunja ahadi za mungu na kakuzulumu na asipolala na wewe zaidi ya Miezi mitatu wakati yupo Hana tatizo pia anajipatia Zambi jengine wewe pia ukimtaka kimapenzi anatakiwa akupe Penzi labda Kama ametokea anaimwa , asipofanya hayo amevunja sheria za dini mengine nakushauri fata au tafuta ma sheikh Wenye elimu sio wa vichochoroni wakupe elimu wapo walimu wamesoma dini wakike watakusaidia, Jengine Kama kweli umependa na dini utafatilia ila Kama umependa Mume tu basi utapoteza wakati Pengine Huyo hata dini hajui yeye anaowa tu kwa Hamu zake labda wewe pia utapata kumsaidia kwa elimu, pia walimu waambie wakufundishe kutia Udhu Kabla kufanya sex na ukimaliza sex Mume na mke wanatakiwa kuoga janaba unajisafisha mwili tafuta namna ya kuoga Janaba utaelewa nini nimeongelea then ndio unakoga Kama kawaida lazima mke na Mume Hilo haki za Mke ni nyingi sana sijazimaliza anachompa Mke Kule na wewe anatakiwa kukupa watu wengi wanarukia wake wengi ila hawajui sheria za wake wengi mtume Kasema Kama unajijuwa huwezi baki na mmoja Kama utashindwa kuwafanyia haki wote. Akipewa gari Yule na wewe unatakiwa gari kwanza Mahari amekupa? Nenda Alhidaaya.com utajifunza mengi kuhusu haki ya Mke.

Anonymous said...

Jengine nimesahau kuhusu Pesa pia Mume sheria Mtume Kasema mwanaume ambaye atakuwa anaposafiri hajaiwachia familia yake kula Huyo kafanya Zulma kubwa haruhusiwi mwanaume kutoka kwenye makazi yake mpaka a hakikishe mke na watoto wapo Hali nzuri Huyu Mwanaume asiwe amekuowa kwa matamanio tu yake Kaeni vizuri mfahamishane elimu ndoa nyingi hazina elimu zina fikiria sex tu na ma uchafu jueni adabu za ndoa na sheria zinasemaje kwenye dini mkizifuata haya malalamiko yataisha. Na Pengine atabadilika ukimwambia dini inasema je .

Dinah said...

Annony wa 9:05am Nichukue nafasi hii kukushukuru sana kwa kuweka mambo kwenye mstari.


Umegusia vitu 2 muhimu. 1- Umebadili Dini kwa ajili ya mume au kuipenda Dini.


2-Mume anapaswa kuhakikisha mke na watoto wapo salama kamba "hajatoka"

Wengi hutumia "uislamu" bila kuujua Uislam kama Dini(Iman).

Hakika mie pia nimejifunza jambo pia. Ahsante sana.

Anonymous said...

Asante sana kwa ushauri,Mimi mtoa mada