Friday, 16 May 2014

Kisirani sehemu ya Pili

Acha Uvivu: Kabla hujalala panga kwa kuandika nini kinatakiwa kufanywa siku inayofuata.


Kitu cha kwanza kiwe Mazoezi, natambua sio utaratibu wengi lakini amini nakwambia....Mazoezi huondoa Uvivu/Uchovu, huitaji kwenda Gym, hapo hapo chumbani kwako kunatosha kabisa kuruka-ruka na kufanya push-ups na sit-ups. Kwavile huna mtoto itakuwa rahisi kwako.

Kwa kufuata mpangilio wa vitu ulivyoandika chini jitahidi uvifanye vyote kwa muda uliojiwekea....Mf; kabla ya saa Sita Mchana usafi uwe umemalizika.

Huna mtoto na wala huna ajira hivyo sidhani kama unahitaji Msaidizi, kama uanae muachishe kazi ili ufanye kazi zote humo ndani kama "ajira" yako.


Kisirani/Hasira/Ukali:

Jifunze kujizuia, unaweza kujizuia kwa aina nyingi....ila hizi hutoa matokeo mazuri. Ikiwa kama unamuaini Mungu, Ongea nae, Muombe akupe Amani Moyoni kwani hutaki kujisikia unavyojisikia.


Jifunze kusikiliza na kufikiria kwa wakati mmoja hali itakayokuzuia ku-snap na kutoa majibu kwa hasira.....kama hasira zimekukamata jizuie na utoe jibu fupi bila kufoka au kuonyesha hasira Usoni...

Kama issue inahitaji maelezo marefu, omba muda kujibu, nenda chumbani na ufikirie kilichosemwa kisha rudi na ujaribu kutoa jibu bila kufoka au kukasirika.

Au kila unapohisi hasira zikianza kuja bana/Uma Meno au kunja ngumi, huku umefumba macho na ujikakamue bila ku-move wala kuongea......au hit something kama ukuta au meza....ukiumia utajiona mjinga so hutorudia tena.Au kila unapokuwa na kisirani, usikae na kuanza kujionea huruma....inuka na hasira zako, nenda kachukue Masufuria masafi na uyasugue kwa kutumia Mchanga mpaka yang'ae.


Ukimaliza bila kupumzika....safisha nyumba yako na hakikisha ni safi na imependeza. Nyumba ikiwa safi kutokana na jasho lako hakika utapata Amani Moyoni na utatabasamu(kisirani nje).


Tamaa/Wivu:

Ni hisia ambayo hujificha au mhusika mwenyewe huificha kwa vile ni aibu kusema kuwa unamuonea wivu (as in envy) au tamani maisha ya rafiki yako/ndugu yako/jirani n.k.


Wengi huificha hisia hii kwa kujifanya marafiki, kwa kuonyesha furaha kwa mafanikio yako lakini kumbe Moyoni wanatamani wangekuwa wao (wanajenga chuki).

"Envy" inasababishwa na kutoridhika kwako na maisha uliyonayo au chochote ulicho nacho unadhani hakitoshi na unataka zaidi.....unapoteza Muda mwingi kufananisha maisha yako na ya watu wengine....unafuatilia maisha ya watu au mtu alafu unaishia kuumia au kukasirika/chukia.

Ifunze nafsi yako kuridhika na ulichonacho.....Kila unapoamka asubuhi ukiwa na afya njema, jione kuwa unabahati kwani wenzako muda huo ndio wanavuta Pumzi ya mwisho.


Thamini maisha uliyonayo na yaone kuwa ni unique na hayapaswi kufanana na maisha ya watu wengine kwani wewe na wao ni watu tofauti na muhimu hawana umuhimu kwako.


Andika vitu au mambo uliyonayo maishani mwako ambayo unadhani ulitamani kuwa navyo na sasa unavyo.


Mf:Afya njema (huna magonjwa), Elimu, Ndoa, Mahali pa kuishi n.k. kisha jiulize...ulifanya nini kufanikisha yote hayo na je ni Muhimu kwako?

Kisha andika vitu ambavyo unatamani kuwa navyo sasa na kwanini? Je ni kwasababu unataka kuwa sawa na fulani au kumshinda?.....unapata faida gani kujilinganisha au kushindana na huyo fulani? Je, ni muhimu kwako kuliko Ndoa yako?


Kujiamini; Uzuri hauna uhusiano na kujiamini au kutojiamini. Mimi si Mzuri lakini najiamini asikuambie mtu hihihihihihi. Anyway....


Kujiamini kunatokana au kunasababishwa na malezi ambayo yalikuwa Chanya kutoka kwa wazazi au walezi.

Kama watu hao walikuwa ni watu wa kukukandamiza, simanga au kukufanya ujihisi huna umuhimu au "not good enough" kwenye lolote then hali ya kujiamini hupotea kwa sababu umeaminishwa kuwa wewe si "good enough".


Sasa ukiendelea na Kisirani/Hasira, Uvivu na mengineyo hata mumeo atakuona kuwa si "good enough" kama mke....hivyo ni muhimu kurekebisha hayo hapo juu ili kupata au kurudisha hali ya kujiamini.

Anza kuwa Chanya (Positive) na fikiria kitu cha kufanya kila siku ili uhisi kufanikiwa. Mf; jitolee kusaidia wengine....tembelea Hospitali/Wodi ya watoto na Usaidie kwa lolote linalohitajika na wewe unauwezo wa kufanikisha.

Sio lazima usaidie Wodi nzima, unaweza saidia mtoto mmoja kwa kitu kidogo kama Dawa ya kupunguza maumivu.....utakuwa umefanikiwa kufanya jambo "chanya" la kuondoa maumivu ya mtoto husika....ni mfano tu.

Itumie Elimu yako kusaidia wengine, umesema hufanyi kazi, Unaonaje kama ukiitumia Elimu yako kujitolea kufundisha watoto kusoma vitabu(soma nao).....watoto hao wakijenga utamaduni wa kujisomea Vitabu utakuwa umefanikisha jambo ambalo ni Chanya.

Kufanya hivyo pia kutakupa nafasi ya kukutana na watu mbalimbali na hivyo taratibu kuanza kujenga hali ya kujiamini na kuondoa Uoga/Aibu ya kukutana au kuwa mbele ya Watu.

Kila unapopata Changamoto, usikasirike au kujiona kuwa umeangushwa na badala yake tafuta namna ya kukabiliana na changamoto hiyo ili ushinde ki chanya zaidi.


Toka na mumeo mara kwa mara bila kujumuika na Marafiki bali ninyi wawili kama wapenzi, hakikisha mnakaa mahali ambapo sio "romantic" yaani penye mwanga mdogo.


Kaeni mahali ambapo watu wengine wanawaona kwa uwazi....sina maana kuwa ujionyeshe la hasha! Bali utakuwa mbele za watu wengine na hiyo itasaidia kukujengea hali ya kujiamini.

Ngoja niachie wengine wajazilizie niliporuka au kosea.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

3 comments:

Anonymous said...

Asante sana..dada kwa ushàur mzur, kwan hata nami nasumbuliwa na tabia kama hîi lkn hasa ile ya kuchukia/kakasirika bila sababu,ila pia leo nimegundua kuwa sababu ya mm kuwa ivi... apo miaka ya nyuma nikiwa mdogo niliishi kwa mateso xana na manyanyaso wakati nalelewa na kusomeshwa na mjomba wangu....ivyo mkewe alikuwa akinitesa sana.... nashukuru kwa elimu unayoitoa dada.

Anonymous said...

Ushauri mzuri sana Dada dina nimekupenda

Anonymous said...

Nimejifunza xna kwenye UKALI + hasira... Hongera D