Kufundwa, K kutoa/ingiza hewa na Kuruka hedhi(re-post from 2015)

Habari yako dada Dinah, habari ya kazi. Napenda sana kusoma makala zako maana zinanielimisha na kunijiza mengi. Hongera sana dada yangu.

Mimi ni msichana nitatimiza miaka 20 hivi karibuni, ninaomba unisaidie yafuatayo:

1-Nina tatizo, naweza kukaa nikasikia kama hewa inaingia ukeni ama kutoka. Mwanzoni nilidhani ni Mikao ya kufanya ngono maana nimewahi kuuliza nikaambiwa hivo.

Je hili tatizo linasababishwa na nini? kama ni mikao ya ngono kwasasa nina kama miezi 9 bila kushiriki ngono ila shida hii aihishi kabisa. Mara nyingine huwa nafikiri inasababishwa na kutokuvaa chupi maana mimi sipendi kabisa kuvaa chupi mara nyingi.

*******


Dinah anasema: Sidhani kama kutokuvaa chupi kunasababisha hewa kuingia kwani hata ukivaa chupi bado hewa itapenya kwenye chupi na kuufikia Uke. Ungekuwa umezaa ningesema labda ulegevu wa Misuli ya kike ambayo hujirudi kwa kufanya mazoezi ya Misuli hiyo muhimu. Pia mkao wa ngono uitwaji chumamboga au bong'oa au inama, au piga magoti kisha inama halafu Mkibaba anakuingilia Ukeni akiwa nyuma yako huingiza hewa....akiingia anaingia nayo na hivyo hewa kujaa ukeni.


Au pengine ni ufanyaji wa ngono kabla ya umri wa miaka 21 umelegeza misuli ya Uke wako, maana kama unamiaka 20 sasa ni wazi kuwa ulianza Ngono ukiwa mdogo si eti?!!Nakwavile bado mdogo au ulikuwa mdogo hukujua umuhimu wa kufanya mazoezi ya  kukaza Misuli ya uke.


Vilele kama ni mpenzi (wafanya mara kwa mara bila uangalifu) wa kufanya Ngono kinyume na Maumbile inaweza kusababisha muingiliano, si wajua maumbile yetu wanawake? Hizo sehemu mbili ni "majirani" wa karibu na hivyo kusababisha "jeraha" na hivyo ukawa unajamba kupitia Ukeni?

Niliwahi kusikia kuwa kuna uhusiano kati ya hewa Ukeni na ugonjwa wa Fistula, hivyo ni vema kama ukienda kumuona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wanawake kwa ushauri wa Kitaalam na pengine Tiba.

Kwasasa piga Endiketa(Mazoezi ya kukaza Misuli ya Uke) za kutosha.

***************





2-Je kwa uzoefu wako (ujuzi wako) kufundwa kuna umuhimu? kama kuna umuhimu nisaidie unambie faida zake.


******

Dinah anasema: Inategemea na mtu na Ufundwaji husika. Mie nimefundwa baada ya kuvunjwa Ungo na Elimu(ufundwaji) ukaendelea kutolewa karibu kila siku (a moment with Bibi) mpaka alipofariki.


Nimefundwa nikiwa simjui mwanaume na wala sikuwa tayari kuolewa actually nilikuwa Shuleni(Secondary)....tofauti kabisa na Ufundwaji wa sasa ambapo mtu anafundwa akiwa tayari kazaa na wengine wanafundwa na Wanaume (Mikorosho).


Kufundwa ni kupewa Elimu ya awali ya kukuandaa na Maisha ya baade kama Mke na Mama hivyo ni kuanzia Mwili wako,Mapenzi, Uhusiano, Ngono,Uzazi na baada ya Uzazi (natamani wangefunda na malezi ya watoto)

Faida za kufundwa nilivyofundwa mimi na wengine kama Mimi (kufuata Mila na Desturi) zipo nyingi sana nadhani itabidi iwe Topic maana maelezo ni marefu mno, ila kwa kifupi ni kuwa inakusaidia:

- kujua mwili wako.

-unajua jinsi ya kukabiliana na mambo ya kike bila kuhusisha watu baki.

-unaju anamna ya kujiheshimu na kujithamini kama mwanamke.

-unajua namna  ya kujiamini.

-unajua kuishi na mume na kuwa mke mwema bila kuwa mjinga.

-unajua namna ya kumpenda  na kumridhisha mumeo.

- unajua namna ya kutunza pesa.

- unajua namna ya kujitunza nakujipenda  kabla,wakati na baada ya Mimba/Uzazi na mengine mengi.


***********


3-Shida nyingine inanisumbua sana ni mzunguuko wa hedhi. Yaani naweza kukaa hata miezi 2-3 bila kuona hedhi yangu kwa kifupi zikitaka zinakuja kama hazitaki haziji. Je hili linaweza likasababisha mimi kushindwa kumimbika?


Nimeenda hata hospital Doctor kanambia eti siwezi kupewa dawa yoyote, ila eti siku nikitaka (nitakuwa tayari) kupata mtoto niende nipewe dawa. Nifafanulie hili maana nina ogopa.

Heri kwako dada na family yako.


********

Dinah anasema: Kwa umri wako mwili bado haujatulia (homono inbalance) baada ya kubalehe. Hilo moja. Pili, mawazo au hofu inaweza kusababisha Hedhi kuruka au kuchelewa.


Ukikua labda kuanzia mwakani ukigonga miaka 21 au pengine mpaka 24 hivi homono zitatulia na Hedhi itakuwa inakuja kila mwezi. Daktari wako yupo sahihi, hakuna dawa ya kusababisha Hedhi isipokuwa kama kungekuwa na tatizo la afya  na umri wako ni miaka 25+ linalosababisha ukosefu wa siku zako.


Ukiwa tayari kupata mtoto nadhani alimaanisha ukikua(ukiwa mkubwa na tayari kuzaa) then kama bado hupati Hedhi kwa wakati basi utafanyiwa uchunguzi hasa kwenye Ovari ili kuona kama kuna tatizo linakosababisha Hedhi kuruka..


Natumai utaridhika na Majibu yangu au wachangiaji wengine.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Dah mdogo angu wewe mbona bado mdogo sana,umri wako mwenzio nlikua naenda kusema kwa mama mwanaume akinisumbua nimejua mapenzi at 26 yrs old na najutia, huo umri unapaswa kuzingatia masomo dear instead of invorving in love affairs na uhakika unaweza hebu jicontrol bas mtoto mzuri ili baadae uje ufurahie ngono kutiwa at ur age dahh fanya mambo ya maendeleo au piga kitabu ka unasoma mpenzi...ila hakikisha unamuona dactari wa wanawake pia.