Wednesday, 2 April 2014

Nifanye nini ili harufu iishe...

Pole na kazi za kuelimisha jamii na hongera pia. Mimi ni mfuatiliaji
mzuri wa uelimishaji wako kwenye mtandao na ninatatzo ambalo
linanikosesha raha na marafik.


Ninaumri wa miaka 19 toka nizaliwe sijawahi kufanya mapenzi ila tatizo langu ni huwa natoa harufu sana sehemu za siri.

Nimeenda Hospitali mpaka nimechoka, na kujisafisha najisafisha kila siku
sijui tatizo ni nini?

Nakosa raha na marafki wananikimbia na kunisema, hata wanaume wanaponitaka kimapenzi nawakatalia kukwepa aibu.

Natamani kuwa na mpenzi ila
nashindwa, dada natumai utanisaidia kwa ushauri kuhusu tatizo langu ili niwe na furaha kama wenzangu.


Asante


*********

Dinah anasema: Shukurani kwa ushirikiano na ahsante sana.

Pole sana Mrembo, hao marafiki gani wanakukimbia na kukusema badala ya kukusaidia angalau hata kwa ushauri au kutafuta ushauri kwa niaba yako?!! The shenzi type.

Kwenda hospitali na kupewa dawa au ushauri na Daktari wa Jumla (GP) haisaidii sio Daktari Maalum kwa ajili ya tatizo lako.

Unapaswa kwenda kumuona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kike/Wanawake ili ufanyiwe uchunguzi yakinifu na kupatiwa matibabu.

Magonjwa ya sirini (wengi huita zinaa) kwa wanawake sio lazima yasababishwe na kufanya Zinaa au kufanya Ngono.

Kutokana na maumbile yetu yalivyo, kutokuvaa Chupi tu kunaweza kukusababishia maradhi Ukeni.

Kuvaa chupi kunasaidia lakini ni muhimu kujua aina au material ya Chupi husika, ni vema uvae za Pamba au zenye kijitambaa cha pamba pale kati (panapoziba uke).

Kuchangia kamba ya kuanikia nguo, vifaa unavyotumia bafuni/chooni, sabuni unayotumia wakati wa kuoga n.k. pia inaweza kukusababishia maradhi ya Zinaa kutoka kwa watu wengine.

Wakati mwingine mabadiliko ya Homono wakati wa Ukuaji (Kubalehe) kwa wanawake kunaweza kusababisha maambukizo...."Vimelea" rafiki vinavyotunza Uke hu-attack mwili kwamba vinakuwa adui.

Ukipatiwa matibabu anza kuwa muangalifu sana, hakikisha unanawa na safi na kujikausha kila unapokwenda kukojoa.

Tumia maji yaliyochemshwa vema na kupoa/mji ya kunywa kunawa kila unapomaliza kukojoa.

Kama unachangia kamba ya kuanikia nguo hakikisha unazipiga pasi ili kuua wadudu.

Hata kama unaochangia nao ni ndugu zako wa damu, hakikisha unachukua hatua mbili mbele ili kujilinda.

Undugu/Ujirani mwema sio sababu ya wao kuwa salama na sio lazima wakuambie kuwa wanagonjwa au walikuwa na gonjwa la zinaa.

Tafuta kifaa chako pekeyako kwa ajili ya matumizi ya kuoga au kujisafisha baada ya kutumia Choo.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

2 comments:

Anonymous said...

Pole na kazi Dina... kwanza samahani nmeshindwa kutuma swali langu moja kwa moja.... ndio maana nmepita huku kwenye comments. . Mimi ni mwanamke wa miaka 28.. nmeolewa miaka 2 iliyopita.. Jana wakati tunafanya mapenzi na mume wangu umentokea hali ambayo haijawahi kunitokea .. kabla hatujaanza nlienda choon kukojoa.. lakin cha kishangaza wakati tunaendelea nlisikia raha ya ajabu halafu nkawa nasikia kama mkojo nliashindwa kujizuia nkauachia ulitoka kodogo lakin kwa kasi halaf nlisikia raha mpaka miguu ikatetemeka na nkapiga kelele za ajab bila kujijua.. je inaweza kua ndio ku squirt au ni tatizo....

Anonymous said...

Msomage topic zilizopita kabla hujaja kuharibu swali la mwenzio. Badala ya kumpa ushauri unakuja na raha zako za kukojoa.Dinah alielezea hilo kitambo. Angalia hii topic http://dinahicious.blogspot.co.uk/2008/12/kukojoa-kwa-mwanamke-ndio-kukoje.html?m=1Muulizaji Wanawake tunamatatizo mengi kabla ya kufanya ngono, wakati wa kufanya ngono, kuzaa na kufikia kikomo cha hedhi au uzee. Kwahiyo huitaji kushiriki ngono kupata ugonjwa ukeni au sehemu za uzazi. Ndio maana tunamadaktari bingwa wa wanawake, nenda kamuone akusaidie.