Miaka 45, ila najisikia kama 20 Kingono.

Kwako dada Dinah.

Mimi ni baba mwenye umri wa miaka 45, Najihisi kuwa na nguvu nyingi za kiume kuliko hapo nyuma nilipokuwa na umri wa miaka
35.

Aidha mara nyingi nina tatizo la kuchoma mkojo na njia ya haja
kubwa wakati wa kukojoa, Niikienda kwa madaktari hunipima
Figo na kukuta ni nzima na hupewa dawa za kusafisha mkojo wakidai
eti mkojo ni mchafu kidogo.


Huwa nilisikiliza kipindi cha Daktari maarufu kinachorushwa na kituo kimoja cha TV Hapa nchini kwetu Tanzania
akieleza kuwa hali ya namna hiyo inasababishwa na accumulation ya Acid
nyingi mwilini.

SWALI:JE HALI YA KUSIMAMISHA SANA INATOKANA NA TATIZO HILO?
Nikipata nafuu ya kuchoma mkojo yaani vikipoa kidogo nasimamisha sana. Sina
tatizo lingine.

NAOMBA JIBU.


*************

Dinah anasema: Kwako Justini,

Umenifanya nicheke kwanza....hivi wewe na wengine wanaouliza maswali ya kitibabu mnajua kwamba Mimi sio Daktari wala Mtaalam wa matatizo ya kiafya?!! Hilo moja,

Pili, mimi ni mkimama(Mwanamke) hivyo sijui mengi kuhusu wakibaba. Natambua kuwa Mwanaume akifikia umri wa miaka 29-40 Nguvu za kiume hupungua na akigonga 41-49 zinarudi kama alivyokuwa in his 20s au zaidi.....alafu 50s nywiii....Viagra tiiiiime.


Hiyo ni kwa wanaume wenye afya njema nikiwa na maana hawana Mf: Kisukari, Ugonjwa wowote wa Moyo, HIV n.k


Pamoja na kusema hivyo inawezekana kabisa hiyo "nguvu nyingi" inatokana na Dawa ulizopewa kutibu tatizo lako, sote tunajua kuwa dawa huwa zina "side effect".

Nadhani ni vema kama utarudi tena kwa Daktari na kumuelezea hali hiyo ya ongezeko la Nguvu za Kiume ili akuangalie Moyo (msukumo wa Damu) na kukupa all clear.

Maana Msukumo wa Damu ambao unasababishwa na Moyo ndio husababisha Uume kusimama.

Kuhusu Uchafu wa Mkojo nadhani pamoja na Dawa ulizopewa pia ni vema ukinywa Maji kwa wingi, Maji ni tiba asilia ya kusafisha mkojo na uchafu mwingine mwilini.


Vilevile Maji ya Ukwaju bila Sukari kila asubuhi husaidia kusafisha Mkojo na kuzuia tatizo hilo lisijirudie (kunywa kila siku asubuhi).


Ni muhimu kuendelea kufuata ushauri wa Daktari wako, kutumia Dawa unazopewa mpaka tatizo liishe kabisa.

Lakini kama dawa zinakusababishia matatizo mengine basi sio mbaya kama ukibadilishiwa, usijefurahia kusimamisha sana kumbe Moyo unadhurika.

Kuhusu Acid Mwilini sijui lolote kuhusiana na hilo ila tangu nina Mume na mtoto wa Kiume nadhani itabidi nifanye uchunguzi ili kujifunza zaidi.


Tafadhali endelea kuwa karibu na Dakrati wako, kula vizuri na angalia afya yako mara kwa mara (Moyo, Mapafu, Figo, Pumbu n.k) maana pamoja na Glory ya kujisikia kama una miaka 20 unapofikia 40, umri huu ndio ambao matatizo ya kiafya hujitokeza kwa kasi.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Pole sana ndugu yangu kwa matatizo hayo. lakini kwa ushauri wangu ni utazame zaidi katika maumbile ya kiume, maoni yangu mimi binafsi nakushauri ukafanyiwe kipimo cha Serum -PSA ( prostatic specific Antigen) ambacho kitaonyesha kuwa prostate zako zimevimba au ziko kawaida na kama zimevimba basi lazima ufanyiwe uchunguzi zaidi wa kujua ni kwa sababu gani zimevimba inawezekana ni kwa sababu ya infection au tumor growth na je hiyo growth ni ya kawaida au uvimbe wa saratani. kwa hiyo ikikutokea hali kama uliyonayo na ukiongezea ya mkojo kutoka kidogo kidogo basi ni vema ukachunguzwe na dactari bingwa ya maradhi ya kiume (Urologist) na sio kila dactari au utaambiwa wewe ni mwanaume wa kikweli endelea kupiga kini kumbe unaharibikiwa. mara nyingi katika umri ulioutaja maradhi haya ndipo yanaposibu. na vilevile ukifuatia na tabia yako ya nyuma kwa kupenda kufanya ngono kwa wingi. Usidharau haya niliyokushauri,
Hautahasirika chochote ukipima mapema maana ikiwa ni negative ni bora kwako na kama Positive ni rahisi kuutibu kuliko kuchelewa. Nakutakia kheri.