Tuesday, 1 April 2014

Ma' mtoto wa Pembeni Msumbufu, nifanyeje?

Mambo dada dinah,

Mimi ni kijana wa umri wa miaka 28 nina mke na mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka 3 sasa lakini pia nilizaa na mwanamke mwingine ambaye mwanae ni mwenye miaka 3 pia.
Huyu wa pili tuliiba tu na bahati nzuri akapata mimba ya mtoto huyo ila mimi
nimemwambia sipo tayari kuoa wanawake wawili na yeye ilikuwa si ahadi tuoane.
Nikimwambia aolewe anipe mwanangu hataki anataka aolewe na mimi. Mimi siwezi naomba ushauri nifanyaje? Kama matumizi natoa.


*************

Dinah anasema: Mambo poa kabisa, vipi wewe?


Uliibia na mwanamke mwingine nje ya ndoa bila Kinga alafu kashika Mimba unasema bahati nzuri?! Hiyo ni bahati mbaya tena MBAYA sana.
Bora Mkeo angekukuta na mtoto kuliko kumpelekea mtoto mwenye umri sawa na mwanae....! Wanaume Weusi kwa kusambaza umasikini (kuzaa ovyo) tu mnaongoza!!Ni rahisi kusema nipe mwanangu nawe uende kuolewa, lakini ukiweka hayo katika vitendo ni ngumu sana.
Sio rahisi kwa mama kuacha mtoto wake mdogo aende kulelewa na mama mwingine(subiri afikishe miaka 15 labda) ambapo mtoto ataamua mwenyewe kukaa na Baba yake au Mama yake.
Pia sio wanaume wengi ambao wanapenda kuoa wanawake ambao tayari wana mtoto/watoto. Most wanaume huwa abuse watoto husika kijinsia.Nenda Ustawi wa Jamii na ukaelezee issue yako nadhani wao wana-refer kesi yako Mahakamni kwa ajili ya Uamuzi kisheria kuwa utamtunza mwanao kwa kiasi cha pesa watakchokupangia kutokana na kipato chako(hakikisha mkeo anajua kama alikuwa hajui na uwe tayari kwa Vita).
Huyo mwanamke hawezi kukulazimisha umuoe ikiwa wewe mwenyewe hutaki kufanya hivyo kwa vile tayari umeoa.
Ikiwa anatumia mtoto kukutishia kuwa usipofunga ndoa nae atatoa siri au atakuharibia kazi....then itabidi ukamripoti Polisi.
Jifunze kumheshimu na kumthamini Mkeo. Unapotoka nje ya ndoa unaumiza Mkeo, mtoto/watoto wako na mtoto atakaezaliwa nje ya ndoa yenu.


Acha ubinafsi, Uzizi na kusambaza Umasikini.

Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...

4 comments:

Dinah said...

Uzinzi* na sio uzizi.

Anonymous said...

Ama wewe kijana ni mbinafsi sana tena bado hujakuwa na kuwa baba kiakili. je? ndugu yangu unajua maana ya kuwa baba? au unafikiri kupeleka matumizi tu JE? umesahau kitu kinachoitwa upendo, ulezi,(care) unafikiri mtoto wako anatambua maana ya pesa au matumizi. mtoto wako sasa hivi anataka kulelewa kwa upendo wa baba na mama na anategemea sana tena sana ushikiano wenu atakapokuwa either mgonjwa au apatapo shida. hivyo ndivyo ulezi unavyotakiwa. sio napeleka matumizi. matumizi unampa huyo mwanamke uliye lala nae sio mtoto. Je? huna huruma na mtoto uliye mzaa na huyo mwanamke? je? kama huyo mtoto ni wewe na baba yako akakuacha ulelewe na matumizi anayopeleka kwa hawara. je? ungali hisi vipi? Ushauri wangu Kama wewe ni muislamu basi unaruhusiwa kuowa wake wawili hivyo muowe. na kama wewe ni mkristo hivyo nenda kwa mchungaji na umuulize ufanye nini kuhusu mtoto uliye zaa kwa uzinzi na tamaa zako binafsi. pengine utapata jibu ukikosa kata uboo wako.

Anonymous said...

Mtoto sasa hivi bado mdogo sana sana mtamchanganya tu na maishu yenu ya kizembe kati yako wewe na huyo mwanamke, wote wakosaji kwa huyo mtoto wa nje na mkeo.

Kama alivyoshauri mwenzangu hapo juu mtoto anahitaji upendo na malezi ya wazazi wote wawili lakini kama wazazi walifanya zinaa bila kupendana na bahati mbaya mtoto kazaliwa hakuna haja ya kuoana hata kama angekuwa Muislamu maana mtatesana tu humo kwenye ndoa kwa vile hakuna mapenzi kati yenu.

Sio kila zinaa inayotoa Mimba ilikuwa na mapenzi nadani yake. Ushauri wangu ni wewe kumueleza mkeo ishu yote kisha uendelee na matunzo au kama vipi kata mguu kabisa alafu baada ya miaka 15 jitokeze alafu umueezee kilichokufanya uuchune.

Kuuchuna na kusubiri mtoto akue husaidia kumuondolea stress mtoto na confusion kwanini haupo na mama yake hii huwaumiza sana watoto sema kina baba huwa hawajali wanadhani watoto hawana hisia.

Ukijitokeza akiwa mkubwa na mwenye uelewa mzuri inakuwa rahisi kuanzisha uhusiano na wewe na pengine ndugu zake walioko kwenye ndoa.

Nasema hivyo kama kijana niliezaliwa kwa bahati mbaya nje ya Ndoa ya Baba yangu hivyo najua maumivu yake pale nilipokuwa namuona baba alafu simuoni tena mpaka baada ya miaka hata mitatu alafu anakuja tena kwa siku moja, simuoni tena mpaka baada ya miaka. Kwa mtoto inauma sana kuliko wazazi wanavyofikiria.

Tuache kuzaa ovyo na tutulie na wenza wetu.

Anonymous said...

Wee jamaa afadhali umetoa uzoefu wako ili wanaume na wanawake mashabiki wa usingo mother kuelewa kwamba unapojoachia kuzaa na mtu ambae huna mapenzi wala mpango wa kuishi nae anaeteseka ni mtoto sio nyie wapenda ngono chafu kana kwamba hakuna Kinga.