Saturday, 8 March 2014

Nampenda, ila ananifanyia Visa!

Hi dinah!
I am a big fan of your blog napenda ushauri unaotoa kwa sababu unajenga na unaelimisha hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nikuandikie ili wewe na wadau wengine wa blog hii wanisaidie

Dinah me ni msichana, and am at my early 20's and niko kwenye mahusiao kwa muda wa miaka mitatu sasa i trully love this guy (i mean i'm so madly in love) at first ilikuwa kama a passing fantancy 2 but this time round imekuwa so serious that i feel like i wanna be his saa yoyote ile(hiswife) lol.

But the problem it's self comes here.. This guy is so ignorance nw days, i might text him but he replies late au hajibu kabisaaa he goes silent for over a week and forth(this is really killing me) what runs kwenye akili yangu ni kwa nini ananifanyia hivi?

Hana hisia na mimi tena? Ana msichana mwingine au what exactly is going on.

Dinah this guy never seezes to amaze me coz when i talk to him kuhusu ku end this relation hataki hata kusikia and yet bado ana nifanyia visa.

Nashindwa cha kuamua hadi dakika hii coz bado nampenda as i said before i am willing to do anything yes! Anything so as to save this relation but nashindwa coz cjui nianzie wap and ukizingatia he's my first guy plz dinah nisaidie..

Thanks in advance dada dinah and wadau!


**********


Dinah anasema: ah! Hii ndio sababu ya mimi kuendelea ku-blog, ahsante sana kwa ushirikiano na Ushabiki kwa Blog yangu.


Upo in your early 20's ambayo ni kati ya 21-24 baada ya hapo ni Middle then late inaanzia 28.

Umekuwa kwenye uhusiano na Jamaa kwa miaka Mitatu, nae pia atakuwa kwenye 20's (I guess).

Sidhani kama uhusiano wenu unahitaji kuokolewa kwani hakuna kitu kinachoashiria kuwa kuna matatizo makubwa...kutokana na umri wenu na urefu wa uhusiano wenu.

Kuna umri fulani (mara nyingi kati ya 24-30) baadhi ya wanaume huamua kuweka mapenzi pembeni na kuwekeza muda mwingi kwenye "kurekebisha" maisha.

Hiyo haina maana kuwa hakupendi/hana hisia nawe (kutokana na maelezo yako) bali hana muda.....inawezekana anatumia muda kukutana na watu anaodhani kuwa watamsaidia kuweka sawa mambo kimaisha/maendeleo.

By the time kafika nyumbani anakuwa hoi, ili usilazimishe kwenda au kukutana nae....anaona ni bora akujibu late au akae kimya which is wrong na hapo ndio Nguzo ya Mawasiliano inapoingia.

Achana na vitisho vya "kama ni hivyo tuachane basi" sort of thing....kama nia yako ni hiyo ni vema kutopetezeana mida.


Siku ukipata muda na kukutana nae ana kwa ana, ongea nae kuhusu mambo yanayokukera kuu ni "kuchuniwa" kwa wiki nzima.

Mwambie Mpenzi najua maisha/masomo yanakupeleka mbio na wakati mwingine unaona mie ni msumbufu....nasumbua kwa vile nakupenda.

Ongeza, huwa napata hofu unapokaa kimya kwa muda mrefu kwani sijui kama ni mzima au unatatizo, naomba tuboreshe mawasiliano yetu.

Mengine ongezea mwenyewe kulingana na unavyomjua mpenzi wako na jinsi alivyo serious na Uhusiano wenu.

Bila shaka nae atajieleza na kuweka wazi kitu kinachomfanya wakati mwingine akae kimya....

Baada ya maongezi hayo, jitahidi kupunguza mawasiliano, yaani usimtumie text wala kumpigia simu kwa siku 3, then msalimie kisha Uchune tena.


Hakikisha unapowasiliana nae unapunguza maswali au ulalamishi....


NYONGEZA: Tatizo kuu la mabinti wengi kwenye 20's ni haraka, too demanding, lazimisha mambo, kutegemea mengi kutoka kwa mwanaume na sio mchango wako (mwanamke) kwenye uhusiano husika .

Tatizo lingine ni kale kaimani ka' "mwanaume wangu wa kwanza" hawezi kunitenda na siku moja atanioa!

Ukitunza Bikira fanya hivyo kwa ajili yako binafsi na sio kwa ajili ya mwanaume au kama mtego wa kuolewa na atakae kuwa wa kwanza kwako.

Kwavile ni mpenzi wako wa kwanza haina maana kuwa ndio atakuwa mumeo.....Ukwanza/Bikira haina maana kwa mwanaume zaidi ya kuongezea kiburi Ego yake.

Pamoja na kusema hivyo, anza kumchunguza nyendo zake ili kujua ukweli (hii ni risk, akikubamba unalo).


Haya, tuone wengine watakushauri vipi.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

3 comments:

Anonymous said...

Mahusiano katika umri mdogo ni kusumbuana tu. Muachane kila mtu awe single atafute maisha alafu mkifikisha miaka 30 ndio muanze mambo ya mapenzi.

Anonymous said...

"If u love him or her, fight for him or her".... Well, thats what many tends to say.... But, this is what i'm gonna tel u, love should always be a two way traffic and not otherwise, any ways i know it sucks to be in your shoes coz i can say that, i'm experiencing almost the same thing at the moment coz i'm so damn crazy for this girl but wow, ananipasua kichwa mbaya..... I think sometimes when our loved ones know how much we love them, they tend to use it kama fimbo ya kutuchapia wenyewe.... Umh, like Dinah said, mchunie for a few days without calling or texting him and tell u what?? I did the same to my girl coz i didn't text her or call her since on saturday na nimemtafuta just this evening(thats 3days) umh, to my suprise, she told me shf missed me!!.. I must admit, i wasn't easy doing that, but, i was worth it coz like u, i'm madly in love with her and i swear niko tayari to marry her even now coz nauhakika i truly love her...... But then again, akiendelea kunizingua, i will definitely walk away coz najua if she can't love me, somebody else will surely do!!! The same goes to u, if he can't love u, somebody else will!!!

@Dinah, u are doing an incredible job and i love u for that coz i have been a regular visitor to ur blog for quiet sometime time now..... Any ways, keep it up!!! Blessings.....
Pande za Arachuga!

Anonymous said...

pole ,ila cha msingi usipende kumlaum sana pindi unaongea nae sometimes usimuulize kabisa kile kilichokukera kwa muda huo ila baada ya kuona ametulia ndio ufanye kuongea naye u'l save