Monday, 24 March 2014

Hedhi kigeugeu, nashindwa kushika Mimba.

Jambo da Dinah first of all pole kwa kazi. Nimeijua blog yako for a long time now and it taught me a lot of stuff.


So dada swali langu is I have been in my marriage for long now bila kupata bahati ya mtoto na tatizo langu kuwa ni kwamba sijui kuhesabu mzunguuko wangu kwani tarehe zinabadilika sana.Hata sielewi kama ni tatizo au ni normal hii inashifanya nisijue ovulation days zangu.Mwezi wa Sept niliingia tarehe 7, October nikaingia 5, November it was 7, December was 15, January was 18 and February was 14.Tafadhali naomba unisaidie, nasubiri majibu yako. Thanks sana Mungu awe nawe and your family.

*************

Dinah anasema: Ahsante kwa kujali na shukurani kwa ushirikiano.


Uzoefu wangu ni wa mzunguuko wa kawaida wa siku 28, nikianza kuelezea na kutoa mahesabu hapa kuhusu mzunguuko wa kubadilika-badilika (siku 24-35) nitakuwa nakudanganya tu mdogo wangu.


Hata hivyo sidhani kama mzunguuko wako unafanya usishike mimba hasa kama mnafanya mapenzi zaidi ya mara 3 kila wiki...kwa mfano.Kumbuka Manii hudumu kwa siku tatu na hata zaidi (inategemea na afya yake) hivyo kama mnafanya mapenzi ya kutosha ndani ya Mzunguuko bila kujali tarehe ni wazi mimba itanasa tu.Unless otherwise kuwa na mambo mengine yanayoingilia au kuchangia kutoshika Mimba.Suala muhimu ni ku-relax maana stress huwa zinaingilia utungwaji wa mimba. Natambua kuwa unapokuwa unahitaji sana mtoto unajipa mawazo na pressure za hali ya juu hali ambayo hupaswi kuwa nayo wakati unajaribu for a baby. Hilo moja.Pili, angalia mtindo wa maisha yako, kama ni mwembamba sana mambo ya diet nini na nini....acha kama unafanya hivyo.....kula balanced diet sio Junk (chips, pizza, soda n.k)Tatu, Unene....kama mwili ni mkubwa pia inaweza kusumbua, fanya utaratibu wa kupungua kiasi.Ikiwa hujashika mimba baada ya Mwaka moja tangu ufanye mabadiliko basi wewe na mumeo muende kwa Daktari kwa Uchunguzi na Ushauri wa kitaalam.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

No comments: