Wednesday, 19 February 2014

Mimi ni mwanamke wa age 28 nimekuwa kwenye mahusiano miaka sita sasa. Nilikutana na kaka mmoja nikiwa chuo miaka sita iliyopita tukawa wapenzi na  aliniahidi kuwa tutaoana bahati mbaya tukapeana mimba kabla nikajifungua mtoto wakike sasa hivi anamiaka 5.

Katika mahusiano kumekuwa na ups and downs nyingi katika miaka yote nilikuwa namsisitiza atoe Mahari lakini wapi but mwaka juzi ndio alienda kujitambulisha rasmi na Mahari akatoa akaahidi tutafunga ndoa baada ya miezi tisa toka alipotoa Mahari. 

Lakini sasa umepita mwaka na ushee hamna kitu, kila nikimwambia ananiambia gharama ngoja nijipange.


Nikimshauri tufanye simple basi hataki na Kanisani kwenyewe kituo cha polisi sasa namuuliza hiyo ndoa tutafungia wapi kama Kanisani hauendi?


Mimi naenda ila ni dhehebu tofauti. Kinachoniumiza ni hivi sasa nina Ujauzito wa pili lakini mwenzangu ndio kazidi kubadilika nimemshika na sms za mapenzi mara tatu.

Ukifungua whatssap yake ndio utalia ni wanashushana kwa sms na video clips lakini namuona mwenzangu haoneshi mshituko kuwa amekosea. 

Mara ya kwanza aliniomba msamaha sana ila wakarudiana tena nimekuta sms tena za mwanamke mwingine nikachukua simu nikampigia huyo mwanamke cha ajabu na kipigo nikapigwa.

Sasa hivi ananiambia wameshaachana lakini bado huyo mwanamke huyo anapiga simu kwake nimetafuta njia yoyote ile ya kuiblock hiyo namba ya mwanamke lakini mwenzangu haoneshi ushirikiano anachukulia simple tu.

Imefikia  hatua wakiwa wanawasiliana anajirekodi kabisa, nimeona juzi nimeumia sana ili hali sasa ivi nina Mimba ya miezi saba.


Kila nikimuuliza ananiambia nimeshaachana naye. Huu ni mwaka wa tatu toka tumepata ajira yeye na mimi wote tunafanya kazi ila mie nipo Wilayani yeye Mkoani hivyo tupo mbali kidogo ingawa najitahidi kila weekend naenda lakini bado akaniambia hayo yote yanasababishwa na me kuwa mbali hivyo niwe naye karibu muda wote.


Sasa hapa nilipo sielewi niache kazi nimfuate ndio itakuwa suluhu au basi tuaachane tu nianzishe maisha mapya?


Najitahidi sana kumfanyia mazuri kumpa suprise kama zawadi mbalimbali lakini ndio hivo .


Kwa upande wa mapenzi ananipa vizuri kabisa tena bila kinyongo na huwa ananisifia sana pia kwa upande wangu kwani yeye ndiye aliyeniingiza kwenye Ulimwengu huu kwani mwanzoni nilikuwa mgeni sana maumivu kila tendo.


Hiyo yote ilikuwa kwasababu ya ubikira lakini siku hizi ameappriciate nafurahia naye nayeye anafurahia but tatizo ni hilo hapo juu sijui nimemkosea wapi.

Naomba ushauri wako mapema sana kwani nipo kwenye lindi kubwa sana la mawazo.

Asante

*****************************

Dinah anasema: Pole sana kwa yote unayokabiliana nayo. Kwanza kabisa USITHUBUTU KUACHA KAZI KUMFUATA huyo mwanaume...kamwe kamwe I beg you!


Humuhitaji Mwanaume bali Unamtaka mwanaume maishani mwako ili kukuongezea au kukupa furaha, kukupa ushirikiano, kusaidiana, kushauriana na pengine kuanzisha familia na kuitunza.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa wewe ni Mwanamke unaejiamini ila Miaka sita ya uhusiano wenu na yeye kuwa mwanaume wako wa kwanza ndio vinavyokufanya uendelee kuvumilia visivyovumilika.

Mwanaume hana Mapenzi ya kweli, hana Utu, hana Huruma wala Shukurani, iweje wewe ufanye yote hayo kwa ajili yake....mpaka kumsamehe alipokusaliti na kukupiga na bado anataka uache kazi kwa ajili yake!!


Hajasema wazi kuwa Uache kazi lakini aliposema uwe karibu nae inamaana hiyo, acha kazi unde huko aliko.


Kuachana/Talaka sio kitu ambacho huwa napenda kushauri, lakini kutokana na matendo ya huyu Bwana (Cheating haisaameheki kwangu) hakika nitakushauri uchukue hatua hiyo.

Hapo hajafunga ndoa na wewe hakuthamini wala kujali hisia zako, sasa "akimilikishwa" Kisheria si ndio utakoma kabisa!


Mmekutana wewe ukiwa na miaka 22, sina hakika na umri wake ila nahisi alikuwa Chini ya miaka 30....katika umri huu wanaume wengi huwa hawajatulia kichwani, hawako tayari kuoa japo wanadhani kuwa wapo tayari.


Huenda alidhani amekupenda lakini baadae(baada ya kukua, akagundua kuwa hakukupenda kivile bali alikutamani tu).


Wewe ulimpenda na huenda uliamini unapendwa au utapendwa zaidi kwa vile amekukuta Bikira (kiuweli hii haiongezi mapenzi zaidi ya kufurahisha Ego ya mwanaume).


Ikiwa mwanaume huyo ameshindwa kubadilika ndani ya Miaka mitatu tangu umsamehe ni wazi kuwa hatobadilika daima na utaishia maisha ya taabu kihisia.


Kabla ya uamuzi wowote Jiulize maswali haya:-

Nini muhimu katika Maisha yako? Kuolewa na huyo mwanaume na kuendelea kuishi maisha yaliyojawa na Hofu, huzuni, maumivu ya hisia na mawazo?


Au Kuishi kwa amani na furaha ukiwa peke yako na watoto wako?

Kumbuka happy mummy, happy kids. Lolote utakalo amua hakikisha watoto wanakuwa na uhusiano mzuri na Baba yao.


Tuone wengine watakushari nini....

Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...

7 comments:

Anonymous said...

Usiache kazi otherwise achana na huyo mwanaume coz ni waz hana mapenz ya dhat kwako,tulia utampata anayekujali.

Anonymous said...

Pole dada, mm kw mtazamo wng naona huyo bwana amekuumiza na atazidi kukumiza kw kuwa bado mapema na mungu labda anamakusudi yake ww usifunge ndoa na huyo jamaa we lea mimba yako ujifungue salama tena ushukuru Una kz yako, mi naona ungeachana nae tu lea watt wako 30yrs bado mdogo sn utapata mume alokipangia mungu na watt wako atawalea tu huyo bwana bado ajaamua kuoa na ht km akioa hiyo ndo itakiwa tabia yake

Anonymous said...

Mwanaume gani huyo hana hata huruma kwa mwenzie mwenye mimba? Hata kama hakupendi tena angezuga kipindi hiki mpaka ujifungue ndio aendeleze ufuska wake.

Muache na maisha yake, nenda ulee watoto wako na ipo siku utakutana na mwenye mapenzi na kujali kuliko huyu wa sasa.

Anonymous said...

Kimbia dada hakuna mapenzi hapo huyo loser anakunyanyasa kihisia na kimwili na ukiacha kazi umfuate atakunyanyasa kiuchumi pia. Utakosa pa kukimbilia na watoto wako na itakuwa too late. Kimbiaaa

Anonymous said...

Pole dada, umesema uache kazi au uachane nae. Jibu langu ni Muache yeye. Olewa na kazi yako, Wanaume wapo tele lakini Kazi za kutafuta na hazipatikani haraka kama wanaume.


Maisha ya siku hizi Wanawake tunaolewa na Kazi zetu wanaume ni luxury tu, hatuwahitaji ili kuishi lakini tunahitaji kipato au kazi ili kuishi.

Anonymous said...

Kisheria mnatambulika kama mke na mume kama mmeishi pamoja zaidi ya miaka miwili na kuzaa.
Kabla hujaachana nae weka sawa masuala ya Matunzo kwa watoto. Nenda Ustawi wa jamii kwa ushauri zaidi.

Anonymous said...

Miaka 28 mbona bado mdogo sana. Usijutie kupoteza miaka sita angalau umepata watoto. Lea wanao na huyo mdogo akifikisha miaka 3-4 jiweke sawa kimwili, upendeze, uvutie uanze kudate tena na utaolewa na atakaekupenda kama ndoa ni muhimu kwako.

Lakini mimi ningekushauri uwe single mum bila kuwapa watoto baba mwingine asijekukutesea watoto. Kuwa tu na uhusiano na kiserengeti maisha yaendelee.