A-demand tuachane mara kwa mara!

Habari dada....
Nipo kwenye mahusiano kwa muda wa miezi minne sasa, lakini kila tunapogombana mwenzangu ana'demand tuachane.



Nikijitahidi kuongea nae anasema anataka kua peke ake. Tatizo ananipenda na mie nampenda pia ....na leo hii ndio kanikazia kweli anataka tuachane.



Kinachosikitisha tuanaachana bado
tunapendana na hakuna sababu ya msingi ya sisi kuachana.... So hii
hali inamaanisha nini....???


********************

Dinah anasema: Habari ni njema, nashukuru. Kwani wewe na huyo Binti mnaumri gani?


Alafu huwa mnagombana kuhusu nini hasa? Maana jambo laweza kuwa dogo lakini kwa mwenzio ni kubwa.



Miezi minne ni michache sana ku-declare "Uhusiano" unless otherwise huwa mnaonana kila siku ya Mungu au mnaishi pamoja.



Tuseme mmekuwa mkitoka (date) kwa miezi minne, inawezekana anakupenda ile ya ku-like na sio ya ku-Love hivyo hayupo tayari kuwa serious yaani kuwa kwenye UHUSIANO na wewe.




Vilevile Miezi hiyo 4 ni michache sana kuwa mnagombana-gombana.



Huenda mwenzio anataka kufurahia uanamke wake kwanza baada ya kutoka kuwa Binti wa fulani, anataka kuwa mwanamke mwenye maamuzi yake na uhuru wa kufanya atakalo alafu baadae ndio a-settle na kuwa serious kwenye uhusiano, hilo Moja.




Pili, kama Binti ni wakubwa kiasi say 25-29 basi nitasema "anatikisa kiberiti" ili kuona reaction yako je? Utambembeleza? Utamhakikishia kuwa unampenda kiasi gani na kumahidi er... pengine Ndoa hapo baadae.




Tatu, pengine ni Homono tu, unajua baadhi ya wanawake huwa zinawasumbua sana hasa wakikaribia Hedhi huwa na hasira/mkali, anachukia kila kitu/mtu n.k.



Nne, inawezekana kabisa ni utoto tu unamsumbua....


Nyongeza: Issue ya kuaminiana kwenye kutoka/mahusiano imekuwa pana na tata siku hizi kutokana na mitandao ya Kijamii.


Tuone wengine watakuambia nini....
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Akati mwingine mtu unagundua kuna mambo muhimu maishani zaidi ya uhusiano wa kimapenzi ambao unajua kabisa hauna future. Bora kuachana nae kuliko kupotezeana muda. Nionavyo mimi.
Anonymous said…
Hakupendi angekuwa anakypenda asingekuwa anakwsmbia tuachane mara kw mara