Thursday, 30 January 2014

Kunatatizo nikioa Shemeji yangu!

Mambo vip dada Dinah. Pole sana na shughuli za kila siku. Mimi ni
Mwanaume mwenye miaka 25 nipo mwanza.Nimemaliza Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) mwaka jana (2013). Kwa sasa naishi na Kaka yangu, Shemeji (mke
wa kaka) pamoja na mdogo wake Shemeji, wa kike.
Kwa sasa tumetokea kupendana sana sana na Shemeji (mdogo wake Mke wa Kaka). Mapenzi yetu ni siri sana kwa sababu Kaka hajui wala Mke wake hajui chochote.Tumeshapanga mambo mengi ambayo tutafanya hapo baadae. Naomba ushauri, hivi kuna tatizo nikimuoa shemej yangu?!
*************************Dinah anasema: Ahsante na Shukurani kwa Ushirikiano. Well huyo Binti sio Shemeji yako bali ni Shemeji ya Kaka yako. Huyo Binti ni mdogo wa shemeji yako au niseme ni Shemeji ya Kaka yako. Huna uhusiano wowote hapo.Kinachofanya Ndugu wa pande mbili tofauti zilizofunga ndoa kutopendana ni Heshima au Uoga (inategemea na Kabila na Mazingira).


Enzi za Bibi yangu, Mwanaume akiwa anajiweza kiuchumi na kuchumbia familia nyingine, Baba Mkwe alikuwa anatoa Binti yake mwingine kama zawadi/Nyongeza.


Hivyo Mwanaume anaoa Dada na Mdogo wake....hehehehe, My point is:- Hakuna tatizo lolote Kiimani na Kitamaduni kuoa Mdogo wa Shemeji yako.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

5 comments:

Anonymous said...

Da Dina mzima,
Tunashukur jinsi unavotujuza mambo endelea na moyo huo huo BIG UP!!
Niko nje kidogo ya hiyo topic, nna swali kidogo, hivii, eti ni kweli ukitaka kuconceive haraka usiwe unasafisha kitoko kwa bibi?? eti uache ule utoko mwiingi sperms zitapita kirahisi? nimeisikia ikanistua kidogo kwani kunawa biwa kujisafisha humo ndani mmmh.mimi binafsi imenishinda.
Tafadhali nisaidie.
Mama D.

Anonymous said...

Khabar za leo da Dinah?
Asante sana kwa mafundisho yako mazuri.
Nje ya topic kidooogo,
Naomba kujua hili nimesikia kuwa eti ukitaka kushika mimba kwa haraka basi usisafishe kitoko, ukiache kiwe kama ukoko huko kwani sperms ndio zitapita kwa urahisi eti, Je lina ukweli ndani yake? na sisi tulozoea kujiswafi huko kikamilifu ina maana ndio kinatuchelewesha kushika ujauzito?
natanguliza shukran.

Dinah said...


Anny wa 03:33pm, Mie mzima namshukuru Mungu. Kazi ya Utoko ni kusafisha na kulinda Uke wako sio kusafirisha Mbegu.


Pia Utoko ni mzito na unajitokeza ili kutoka nje ya uke na sio kukutana na mbegu kurudi ndani yaani Utoko na Sperms haufanyi kazi pamoja.


Ute ule kama maji unaoteleza, ule unaojitokea unapokuwa na nyege au ukifika kileleni.....enhee ule ndio maalum kabisa kusaidia mbegu kufika zinakotakiwa kufika ili kutengeneza mtoto.

Natumai nimekujibu vema, ahsante.

Dinah said...

Annoy yule yule hehehehe swali moja umerudia mara mbili kwa namna tofauti. Bahati yako wanangu wamelala.


Tunaojiswafi hekoo! hakuna uhusiano wa kujiswafi (kutoa Utoko) na kushika Mbimba haraka. Mie nimeshika mimba chap-chap mbona.


Muhimu ni kufika kileeni kwanza (mwanamke unafika kwanza) kisha mwanaume anakufuata hivyo basi kuna kuwa na ute wa kutosha kusafirisha Mbegu.


Akiisha kukojolea inua kiuno sambamba na makalio na miguu juu kwa dakika kama 5 hivi kisha ndio uende kuoga/nawa.


Hakikisha hamfanyi kila siku bali kila baada ya siku moja au mbili ili akikojoa amwage shahawa za kutosha.

Kila la kheri!

Anonymous said...

Asante sana da Dinah nimekuelewa vema..nliona shida kutonawa..kumbe haihusu...
Barikiwa sana..and kisses to your lovely kids.
Mama D.