Wednesday, 3 April 2013

Jinsi ya kuchagua jinsia ya mtoto

"Nina kukubali uwezo wako kiushauri na kiuzoefu,Umejaliwa!!..Mimi ni kijana wa kiume  mwenye umri wa miaka 27,nina mchumba wangu na tuko kwenye harakati za kufunga ndoa.


Tatizo langu ni hili: Napenda sana first born wangu awe wa kike;[tei tei.....],na ninasikia kuna namna fulani ya kuweza kupanga jinsia ya mtoto japo ni kwa majaliwa ya mungu.


NIFANYEJE???? Naomba unisaidie jamanii!! Wako B.Z"

*****************************

Dinah anasema: Ahsante, Nashukuru sana. Ni kweli kuna namna ya kuchagua Jinsia ya mtoto kabla Mimba haijatungwa lakini bado haijathibitishwa Kisayansi/Kitaalam.


Kupata mtoto wa Kike sio ngumu sana kama ilivyo kwa mtoto wa kiume + inategemea zaidi kwenye uwingi wa jinsia hiyo upande wako(familia ya mwanaume).


Mbegu zinazosababisha mtoto wa kike "hutembea" taratibu kuelekea kwenye Yai na huishi kwa masaa 72-Wiki....hivyo wewe na mkeo hamtahitaji kusubiri "tarehe" maalum.


Kama kwenu au kwa baba mdogo/ mkubwa kuna wanawake wengi basi unaweza ukafanikiwa kupata Binti bila taabu kabisa.

Ila epuka kufanya mapenzi tarehe ambazo mkeo ajae anakaribia kupevusha Yai....fanya mapenzi baada ya hedhi na wiki mbili baadae.


Mbegu zinazosababisha mtoto wa kiume zipo "faster" na hufa haraka, hivyo kama unataka mtoto wa kiume inabidi kutegea "tarehe" maalum ili Mbegu iliwahi yai likiwa njiani...


Japokuwa suala la mtoto wa kiume linategemea zaidi upande wa Mwanamke, ikiwa kwako kuna wanaume wengi au idadi sawa na wanawake, urahisi wa kupata mtoto wa kiume ni kubwa.


Sehemu ya maelezo yangu ni kutokana na uzoefu wangu binafsi, tulipotaka mtoto wa kwanza awe wa Kiume tulikuwa tunafanya kwa kufuata "tarehe" maalum + mikao maalum(hakuna kifo cha mende wala vijiko)!!


Mtoto wetu wa Pili ambae ni wa kike, hatukufuata "tarehe" maalum...

Kifamilia, idadi ya wanaume kwetu ni kubwa kuliko wanawake.

Wengine wataongezea...
Mapendo tele kwako...
"Dinah,
Habari za kazi nimefurahi sana leo nimeingia kwenye blog yako umerudi ulingoni, na hongera sana.
 

Mimi naomba ushauri wako na wachangiajia wengine, najua wengine watanitukana au kunibeza ila mimi nitachukulia kama ushauri na kuchagua jema kwangu nisikuchoshe sana naomba nianze kama hivi:-
 

Mimi ni mwanamke wa miaka 32, nimeolewa na nina watoto wawili(2) kabla sijaolewa na mume wangu huyu nilikuwa na mpenzi wangu ambae kweli tulipendana sana ila tatizo likawa kuwa ameoa hivyo kunioa mimi ikashindikana.


Kwa kweli nilikuwa nampenda sana lakini kikwazo kikawa ana mke, ila kwenye maisha yake ya ndoa hakujaliwa kupata mtoto kabisa mpaka leo hii.


Yule mpenzi wangu (wa zamani) akawa ananipenda sana na akataka nimzalie watoto ila mimi nikamwambia sipo tayari kuvunja ndoa yako kwa sababu mke wako hazai, mpende tu hivyo hivyo maana ndoa ni upendo ila watoto ni maajiliwa.


Basi mimi nikapata mchumba aliyenipenda na kutaka kunioa na nikaolewa nae. Nikamwambia Mpenzi wangu(wa zamani) nikamwambia najua unanipenda ndio ila huwezi kunioa bora tu mimi niolewe na mtu mwingine.


Jamaa alikuwa mstaarabu akanikubalia nikafunga ndoa, Nimeishi na mume wangu kwa miaka 7 sasa, jamaa katafuta namba yangu akanipigia simu kuwa bado ananipenda na anaomba tuendelee na penzi letu kama zamani.


Yeye alikubali tu mimi niolewe ni jenge familia, kusema ukweli mimi pia nampenda sana maana ni mtu anaejali sana sio kwamba ana pesa laa! sasa amekuwa akinisumbua sana!


Nikamwambia mimi nipo kwenye ndoa sitaki kuharibu ndoa yangu ila bado jamaa ananisumbua nifanyeje ili nisiharibu ndoa yangu?


Wadau naombeni ushauri nimjibu nini ambacho hakitamuumiza akubaliane na mimi?

Wenu muathirika.

***********************************

Dinah Anasema: Njema tu, vipi weyee...mwambie huyo Mume wa mtu (your ex) akukomee kama alivyokoma....hihihihi natania!

Sasa Bibie umeweka wazi hisia zako kwa huyo Mume wa mtu kuwa unampenda, hujagusia hisia zako kwa mumeo baba wa watoto wenu! Inamaana humpendi, uliolewa tu kwa vile ulitaka ndoa au...au?


Kwanza Hongera kwa kutokuubali kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzio, uamuzi mzuri sana uliufanya.

Mwanaume huyo (mume wa mtu) hana heshima kabisa kwa mkewe, mwanaume anaemzungumzia matatizo ya mkewe kwa mtu ili afanikishe matakwa yake hafai kuwepo katika jamii.


Moja, jamaa(mume wa mtu) alikuwa akikutumia ili umzalie tu na sidhani kama alikuwa anakupenda zaidi ya mkewe.


Kama angekuwa anakupenda zaidi ya mkewe hakika asingeendelea kuishi kwenye ndoa, angetengana na mkewe (kama ni Mkristo) au angemtaliki via Sheria akiwa na sababu za msingi sio kutokuzaa pekee.


Uko sahihi kabisa, kuwa ndoa ni "Mapenzi" aka "Uamuzi" lakini watoto(uwezo wa kuzaa) ni majaaliwa.


Unahitaji msimamo, ulimpenda/mlipendana enzi hizo, mlifurahia mapenzi yenu "wizi", sasa uumeamua kusonga mbele na yeye anapaswa kusonga mbele na ndoa yake.


Kwavile ulikubali ku-cheat nae akiwa kwenye ndoa ni wazi anadhani kuwa utam-cheat mumeo pia ili muwe "Even".


Huitaji kumpa majibu au jibu yanayopelekea mswali zaidi! Badala ya kumwambia "mimi nimeolewa siwezi kuwa na wewe"...."mwambie sitaki kuwa na wewe, acha kunifuatafuata. Ukiendelea nakushitaki Polisi" (Sheria inakulinda)!!


Suala lingine ambalo ni muhimu ni wewe kuondoa "kiukweli nampenda maana anajali" Vipi kuhusu wanaoa? Vipi kuhusu Mumeo? Vipi kuhusu Ndoa yako ya Miaka Saba?


Acha kulinganisha, wanaume wanatofautiana, huenda mumeo sio kama huyo "mume wa mtu" lakini anaubora wake mwingine ambao umefanya uendelee kuwa nae kwa miaka yote Saba!


Futa Mawasiliano ya huyo Mume wa mtu, weka akili yako kwenye ndoa yako na maisha ya baadae ya watoto wako.

Wengine wataongezea....
Mapendo tele kwako...