Wednesday, 3 April 2013

Jinsi ya kuchagua jinsia ya mtoto

"Nina kukubali uwezo wako kiushauri na kiuzoefu,Umejaliwa!!..Mimi ni kijana wa kiume  mwenye umri wa miaka 27,nina mchumba wangu na tuko kwenye harakati za kufunga ndoa.


Tatizo langu ni hili: Napenda sana first born wangu awe wa kike;[tei tei.....],na ninasikia kuna namna fulani ya kuweza kupanga jinsia ya mtoto japo ni kwa majaliwa ya mungu.


NIFANYEJE???? Naomba unisaidie jamanii!! Wako B.Z"

*****************************

Dinah anasema: Ahsante, Nashukuru sana. Ni kweli kuna namna ya kuchagua Jinsia ya mtoto kabla Mimba haijatungwa lakini bado haijathibitishwa Kisayansi/Kitaalam.


Kupata mtoto wa Kike sio ngumu sana kama ilivyo kwa mtoto wa kiume + inategemea zaidi kwenye uwingi wa jinsia hiyo upande wako(familia ya mwanaume).


Mbegu zinazosababisha mtoto wa kike "hutembea" taratibu kuelekea kwenye Yai na huishi kwa masaa 72-Wiki....hivyo wewe na mkeo hamtahitaji kusubiri "tarehe" maalum.


Kama kwenu au kwa baba mdogo/ mkubwa kuna wanawake wengi basi unaweza ukafanikiwa kupata Binti bila taabu kabisa.

Ila epuka kufanya mapenzi tarehe ambazo mkeo ajae anakaribia kupevusha Yai....fanya mapenzi baada ya hedhi na wiki mbili baadae.


Mbegu zinazosababisha mtoto wa kiume zipo "faster" na hufa haraka, hivyo kama unataka mtoto wa kiume inabidi kutegea "tarehe" maalum ili Mbegu iliwahi yai likiwa njiani...


Japokuwa suala la mtoto wa kiume linategemea zaidi upande wa Mwanamke, ikiwa kwako kuna wanaume wengi au idadi sawa na wanawake, urahisi wa kupata mtoto wa kiume ni kubwa.


Sehemu ya maelezo yangu ni kutokana na uzoefu wangu binafsi, tulipotaka mtoto wa kwanza awe wa Kiume tulikuwa tunafanya kwa kufuata "tarehe" maalum + mikao maalum(hakuna kifo cha mende wala vijiko)!!


Mtoto wetu wa Pili ambae ni wa kike, hatukufuata "tarehe" maalum...

Kifamilia, idadi ya wanaume kwetu ni kubwa kuliko wanawake.

Wengine wataongezea...
Mapendo tele kwako...

1 comment:

Anonymous said...

Habari dada Dinah.. pole kwa kazi ya kuelimisha jamii nafurahia sana blog yako. Mimi naomba kutoka nje ya mada kidogo, naomba unisaidie maana nimetafuta jinsi ya kupost hili nikashindwa ikabidi niandike hapa. Ni msichana nina miaka 24 na natarajia kufunga ndoa mwezi wq pili mwakani. Nina kitu kinachonitatiza ambacho ni kuruka hedhi..yani nikiona siku zangu mwezi huu basi mwezi unaofata sitaona...kifupi naona hedhi mara 6 tu kwa mwaka. sasa mwaka huu imevurugika tena kdg ilivofika mwez wa tisa nimeona hedhi tareh 20..nikaja ona tena tareh 3 Nov then tareh 14 dec.. swali langu ni kwamba ni tarehe ipi ambayo naweza shika ujauzito?! Mana nakuwa sielewi kwasabab ya terehe kujichanganya na natamani sana kushika mimba. Au labda nitakuwa na tatizo kubwa ili nikawaone wataalam hosptal?! Ntashukuru sana dada yng ukinisaidia.

Angel from Arusha.