Simpendi Mume wangu baada ya kutambulisha Mtoto wa nje.

"Dada pamoja na wadau weninge ushauri wenu ni muhimu kwangu. Mimi nina miaka 22, nimeolewa miaka miwili sasa. Tatizo ni kuwa simpendi hata kidogo mume wangu.

Siku za mwanzo tulivyokutana hakuniambia kuwa ana mtoto. Baada ya wiki mbili akaniambia ana mtoto tangu hapo mapenzi yakapotea sikuwa na haja ya mwanaume wa namna hiyo kwani sipendi watoto wa nje hata kama nimemkuta.

Nimejitahidi labda nitampenda lakini mpaka leo wapi, sioni hata dalili sijui hata nifanyeje na nipo kwenye ndoa nitaachana nae vipi au nifanyeje? Asanteni jamani kiroho safi"


Dinah anasema: Pole kwa unayokabiliana nayo, mimi binafsi sipendi watoto wa nje ya ndoa au kabla ya ndoa ( wa ujana) lakini kutokana na maisha tunayoishi hivi sasa ni nadra sana kukutana na kijana wa miaka 25-32 ambae hana mtoto....wengi wanazaa iwe kwa uzembe na kutojali, kutegeshewa (PMU) au kusingiziwa.    

Sidhani kama humpendi mumeo, nadhani unahasira nae kwa vile unahisi amekudanganya, hilo moja.  Pili, ni hofu uliyonayo kuhusiana na hisia zake juu ya Mwanamke aliezaa nae na labda usumbufu utakao upata kutoka kwa mwanamke huyo hapo baadae.    

Baadhi ya watu wanaweza kudhani kuwa una roho mbaya lakini ni ukweli usioepukika kuwa kunapokuwa na Mwanamke mwenye mtoto lakini mpenzi wako hasemi mpaka baada ya kufunga ndoa....inakusanya maswali mengi yanayojenga hasira kuu.    

Kutokana na maelezo yako umegusia kuwa hupendi watoto wa nje, inawezekana kabisa umewahi kuliweka hilo wazi kwa Mume kabla ya ndoa hali iliyopelekea yeye kuogopa kukuambia kuwa anamtoto akihofia utamuacha.    

Maswali muhimu unayopaswa kumuuliza mumeo ambayo yanaweza kukusaidia kumsamehe, kujiwekea "sheria", kuanza upya na kusonga mbele na maisha yenu.    

1)-Hisia zake kwa Ex wake (mama wa mtoto) na je mtoto alizaliwa kwenye mazingira gani (ndoa, uhusiano kabla ya ndoa au usiku mmoja aka bahati mbaya).  

2)-Mtoto anaumri gani? anaishi wapi? na nani?  

3)-Je! kuna mawasiliano yeyote kati yao?     Jinsi atakavyokujibu ndivyo itakavyokusaidia kusonga mbele (unaweza kurudi kwangu kwa ushauri zaidi ukipata majibu ambayo ni tata kwako).  

Pia majibu ya mumeo kwa mswali hayo yatanisaidia mimi na Wachangiaji wengine(perhaps) kukuelekeza namna ya kuweka sheria ili mtoto aendelee kuwasilina na Baba yake (hana makosa) lakini  wakati huohuo Ex wa mumeo (mama mtoto) akae mbali na ndoa/familia yenu mtakayoianzisha.   

**Alafu mwenyewe mdogo masikini...anyway! Nakutakia kila la kheri,
Mapendo tele.....    

Comments

Anonymous said…
Huyo mtoto anaweza kuwa baraka kwako bibi, wewe huwezi kujua kama Mungu atakujaalia mtoto, na akikujaalia huwezi kujua utaishi naye hadi lini..wengi tu wamelea watoto wa namna hii na kujizolea baraka tele na baadaye watu wa kuwasaidia uzeeni....
Mtoto hana kosa lolote huna sababu yoyote ya kumchukia mtoto, muombe Mwenyezi Muonge akuondolee chuki hiyo kwa watoto ni mbaya sana na ni laana
Anonymous said…
habari? na pole na majukumu ya kuelimisha jamii mimi ni mwanaume wa miaka 30 ila na tatizo la kuwa na mboo ndogo kiasi nafikia hatu ya kuhisi simrizishi mpenzi wangu nifanyeje jamani niondokane na hili tatizo