Nampenda ila ni Kicheche, nimtulizeje?

Habari Dada, 27 ni umri wangu, Mwaka 2010 nilianza mahusiano na binti mmoja akiwa Form 3 mwenye umri wa miaka 17. Nilimpenda sana tangu the first day namuona, kipindi hicho nilikuwa College. Kimaisha kwao hali si nzuri, kutokana na mapenzi yangu kwake niliweza kumsaidia Ada.

Kuna wakati hata kuiba chakula home kama Mchele, Unga na vitu vingine vingi ili asitaabike. Pia nilimsaidia kimasomo kama kufatilia shuleni kwao ambako nilijifanya ni Kaka'ke. Kutokana na shule kuwa mbali na anapoishi ilibidi ahame na kukaa kwa family friend wao.

Ukweli alikuwa hapendi Shule, kwani mara nyingi maudhurio yake hayakuridhisha. Alifika Form Four ila hakumaliza. Huyu mtu akahama pale alipokuwa akiishi akaenda kwa marafiki zake maeneo flani ya M'nyamala, sikupenda akae maana sifa za huko si nzuri.

Nilimsihi sana Arudi kwao hakutaka hata mzazi(single parent-mama)yake hamsikilizi mpaka leo. Kipindi hicho mimi nikamaliza Chuo. Nikaamua kufuatilia Skuli kwao nikaambiwa amefukuzwa, Baada ya hapo sikujua namna ya kumsaidia maana sikuwa na hela ya Shule ya Private, ninamuonea huruma sana.

Ananilaumu kuwa mimi ndio nimemfanya aache shule maana baada ya kuwa kafukuzwa alikuwa akija home analala hata siku tatu. Wakati huo mimi nilikuwa Jobless so nilichukulia advantage, baada ya muda nikamwambia baadae tuachane ili mimi nitafute kazi. Alilia sana ila baada ya wiki nikamuambia turudiane akakubali na baada ya wiki moja akanitosa na kunitukana matusi sijapata kuona. Nilichanganyikiwa na nililia kama mtoto mdogo hapo tukiwa na mwaka mmoja.

Kwa kweli alikuwa mtu wangu wa karibu sana. Nikapata kazi mkoani ambako nipo mpaka sasa. Nikamtext nikamwambia nimepata kazi mkoa flani nimefanikiwa interview. baada ya Wiki yaani mwezi tangu tuachane akanikpigia simu akidai kuwa mamake anaumwa ananiomba hela kwa huruma nikamtumia via mpesa.

Tukaanza tena mahusiano, ila alikuwa amebadilika sana. Siku nilimkuta na simu ambayo si yake akadai ni ya bf wake wa zamani. Niliongea na yule kijana na aliniambia huyo demu muhuni na anapenda sana kufanyiwa kinyume.

Sikujali nikaendelea nae, siku mmoja aliniomba nimuingilie kinyume na maumbile, hapo ndio nikajua jamaa alisema ukweli lakini sikukataa nilifanya.

Baada ya muda nilimuida aje huku Mkoani nilipopata Kazi ili apaone kwangu, Huku mkoani nilipopata kazi na alikaa miezi minne lakini tulikuwa tukigombana kila siku. Mara atoke mchana arudi saa tisa usiku, analewa, analeta Mashangingi nyumbani kwwangu. Nikamwambia arudi tu kwao ila nilimuonea huruma. Hiyo ilikuwa October mwaka jana, sikujua alipoenda. November nikamuona kwenye baa moja maarufu alikuwa amekaa na Mzee mmoja nikasalimiana nae akaondoka mida hiyo hiyo.

Nachukia mambo yake lakini sijui kanipa nini? Nampenda sana, nikaanza kumtafuta tena ila niliishia kutukanwa tu. December 31 mwaka jana akanipigia na kuanza kuomba turudiane, tukarudiana. Feb 2013 alienda mkoa flani jirani na napoishi na rafiki yake, alivyokuwa akirudi alipitia kwangu baada ya nimemdanganya nimenunulia vitu fulani vya ndani so akakasirika alivyoona sikuwa mkweli, hata hivyo tulitoka.

Siku mbili baada ya birthday yake tukavamiwa na vibaka ambao walitishia kumbaka mbele yangu. Waliiba pochi simu na kila kitu na walituumiza sana. So nikaona kama mkosi au labda ni jamaa alishawahi kuwa nao nilipoachana nae wametufanyia revenge.

Kaondoka Wiki iliyopita na sasa hanitaki tena. ILA NASHANGAA SIJUI KWA NINI MIMI HUUMIA SANA KULIKO YEYE. Alishawahi nishika na wanawake nje ila nahisi (sina uhakika lakini )yeye ni malaya zaidi coz kwao hawajali anaishi wapi. Nampenda nifanyeje?lengo atulie nimuoe ila elimu hana na hataki kusoma. Nifanyeje, nifanyeje?


Dinah anasema: Kaka mapenzi matamu lakini yanaumiza. Nashukuru kwa kuelezea Hadithi yote kwa kina lakini jibu lake ni fupi sana.
Huyo Binti ni bado ni Mtoto (hajakuwa kiakili), anatumia matatizo ya kifedha kwenye familia yake kama tiketi ya kutangatanga na Dunia. Inasikitisha lakini ndio amechangua mtindo huo wa Maisha.

Pia inaelekea anakutumia kiuchumi lakini hana mapenzi na wewe. Mambo ya kuachana na kurudiana kila baada ya Wiki mbili ni kupotezeana mida tu.

Futa mawasiliano yake na acha kumtafuta tena. Songa mbele, weka maisha yako sawa.
Muda ukifika utakutana na Binti mwenye tabia njema na atakae kupenda zaidi ya unavyompenda au kama unavyo Mpenda.

Hakikisha umeangalia afya yako(Kapime) ili uanze maisha mapya ukiwa unajua ulipo(Status) yako.
Wachangiaji wengine wataongezea....


Kila la kheri. Mapendo tele kwako!!

Comments

emuthree said…
Hapo kwa uoni wangu hakuna `future' hapo labda kwa kiingereza wanaita `infatuation'ni mapenzi ya `Ujana' mnahitajia `kukua' na kwa tabia aliyo nayo, ambayo umesema na wewe unayo, hamtaweza kufanikiwa kuwa marafiki wa kweli.
Kaeni, na mpeani muda, mfikirie kwa undani, kama kweli mnahitajiana. Na mnahitajiana kwa vipi?
Urafiki wa kweli ni ule wa kuwa mkweli kwa mwenzako,(uaminifu) ni muhimu sana,

Pili `ngono' ni hatari, mtapata magonjwa, na itafikia sehemu mumeshamua kuona, mkapata hata mtoto, mkapima mkaonekana mumeathirika,nini faida yake...

Achana naye, kaa panga maisha, ondoa mawazo juu yake,...nina uhakika utapata mwenza mwema, lkn na wewe uwe mwema pia!
Amina K said…
pole sana kaka angu. ila nahisi unachompendea labda alivyokupa ngono kinyume na maumbile sijui ulijisikiaje ndo mana labda ukiwaza hicho unashindwa muacha, ila huo unaofaynya wewe ni utumwa. angalia maisha yako na magonjwa yalotuzunguka. jiulize huyo mwanamke kama hayupo na wewe anafanywa na wanaume wangani? na inavyoelekea hata condom hamtumii, oMG, ACHANA NAE ATAKUUA MBONA WASICHANA WAPO WENGI TUU.