Monday, 26 March 2012

Baada ya Miaka 3 " Presha" ya Ngono imemzidi, mie siko tayari mpaka ndoa-Nifanyeje?

Hello dinah

Mimi ni mschana mwenye umri wa miaka 22 nimekua na matatizo sana katika safari yangu ya mapenzi kiasi kwamba naona kama sina bahati.

Nilianza mahusiano ya kimapenzi kipindi cha mwisho namaliza form 4 ila katika mahusiano yetu tulikubaliana mimi na mpenzi wangu tusifanye mapenzi mpaka pale tutakapo funga ndoa.

Mwezangu alishindwa kukaa nami bila kufanya mapenzi na badae tukachana. Baada ya kukaa kwa muda wa miezi mitatu nikapata mpenzi mwengine nae pia nilimpa mamuzi yangu kua sitafanya mapenzi nae mpaka pale tutakapo funga ndoa na akanikubalia tukawa tunaishi vizuri tu bila matatizo.

Tulipendana sana na kuvumiliana kwa muda wa miaka mitatu na bado mpaka sasa nipo nae ila cha ajabu sasa hivi amekuwa akiniomba tufanye mapenzi nikijaribu kumkumbusha tulivyokubaliana nyuma kabla ya kuanza uhusiano huu.

Ananiambia kuwa sasa hivi presha imezidi kua kubwa ni muda mrefu ajafanya mapenzi kwahiyo yeye kama mwanaume inamuathiri na hana pakukimbilia isipokua kwangu coz mimi ndo mpenzi wake napaswa kumsaidia.

Hili swala la yeye kuniomba kutaka kufanya mpenzi nami linafika miezi mitatu sasa mpaka sasa sijajua nini cha kufanya nampenda sana mpenzi wangu ila mimi bado sijajua nimsaidie vipi hali yakua kwa sasa siwezi kufanya mapenzi mpaka ndoa.

Dada dinah naomba unisaidie kufanya maamuzi sahihi, naamini mpenzi wangu ananipenda sana je kutaka kufanya mapenzi nami kwa sasa inamaana anipendi tena? nifanyeje?

------------------