Yeye 40s with 2 Kids, Mimi 27 anataka ndoa! Je nikubali?

Habari Dada Dinah!
Naomba ushauri wako lakini naomba usinitaje jina langu.


Awali nilikuwa na uhusiano na kijana mmoja ulidumu kama miaka saba hivi. Hatukuweza kuwa pamoja kwa sababu mwenzangu alikuwa anasoma hivyo tulivumiliana kwa shida na raha.

Kwa kweli kaka huyo nilimpenda kupita maelezo lakini alikuwa na tabia zake nyingi ambazo nilizivumilia nikitegemea kuwa ipo siku atakuja kubadilika na hata hivyo niliziona kama ni ndogo kwani penzi la dhati lilitawala juu yake.


Mimi nilianza kazi huku mwenzangu akiwa bado anasoma, hivyo nilikuwa nikimsaidia kwa vitu vidogo vidogo na hata kumnunulia zawadi hasa kila siku yake ya kuzaliwa. Hivyo vyote sikuvihesabu kwani nilikuwa natoa kwa mtu nimpendae.


Kuna kipindi alianzisha biashara mbalimbali na kuna wakati alihitaji msaada wa pesa na mimi bila kinyongo nilitoa kwa moyo. Lakini zile biashara zilikuja kuisha kimya kimya na nikimuuliza anasema eti hajapata kitu chochote.


Yaani kwa kipindi chote hicho sikuona wala kupewa zawadi ya mafuta ya kupaka kama moja ya kifaida alichokuwa anapata katika biashara hizo.


Akaanza kuwa rafu kweli kwani alikuwa anafuga mindevu na nywele ndefu na kila nikimshauri ananiambia hii ndio life style yake na mimi siwezi kumuambia kitu na bangi alikuwa anavuta.


Hayo mambo yote niliyavumilia japo yalikuwa yaniuma sana hasa ukizingatia unamshauri mtu kitu na yeye anakipinga. Yaani ni mambo mengi alinifanyia kiasi kwamba nikasema enough is enough japo yeye hakutaka tuachane kwa kigezo kuwa amebadilika lakini sivyo.

Mapenzi yetu tulianza mwaka 2002 hadi mwaka 2009 nilipotosheka na vituko vyake. Niliamua kujikalia peke yangu bila mahusiano ya kimapenzi na mtu yoyote hadi leo.


Japo kwa kipindi chote hiki cha ukimya wangu huwa ananitumia meseji za kuomba msamaha kwa mambo yote aliyonitendea na kusema amebadilika na ikitokea nimemwambie mimi sitaki mahusiano tena na wewe basi atatuma meseji za kashfa na matusi kibao then anakuja kusema nimsamehe tena eti ni hasira ndizo zinamsababisha afanye hivyo.


Kwa kifupi Dada Dinah mimi kwake ni basi tena japo bado ananitumia meseji za kuniomba msamaha.

Sasa Dada kuna hili ambalo limenifanya niombe ushauri kwako, ni kwamba kuna Baba mmoja tulianza kufahamiana katika kazi niifanyayo japo nilianza kuona dalili za kunitaka kimapenzi lakini hakuwahi kuniambia hata siku moja.


Basi akawa anakuja kama kawaida kufanya kazi zake kunipigia simu kunisalimu. Ikatokea kipindi fulani akawa haonekani nina maana mkoa nilipo mimi yeye amekuja kusoma masters lakini makazi yake ni mkoa mwingine kabisa.

Siku moja akaniomba akutane na mimi na majibu yangu nikamwambia mimi sipendelei kutoka na mume wa mtu yaani kukaa nae sehemu. Akanijibu mimi nina watoto lakini sina mke nikamwambia mtu mzima kama wewe utawezaje kukaa bila mke? Akanijibu naomba utafute muda nikwambie maana ni story ndefu.

Basi tukaa akaniambia yeye ana watoto wawili wakike (darasa la saba) na wakiume (chekechea) na mkewe amefariki kama miezi minne iliyopita. Nikamwambie wanaume mara nyingi mnaweza kumuua mtu akiwa bado mzima.


Basi siku nyingine akaniletea mikanda ya video ya mazishi na nikagundua kweli amefiwa na mke.

Dhumuni lake kubwa anataka kunioa na sasa imepita kama mwaka mmoja tangu mkewe afariki. Nikamwambia swala la kupima amesema hamna shida twende tena mara tatu.


Yeye ni mwajiriwa wa Serikalini na tena ni Afisa Kitengo fulani huko mkoa anaofanyia kazi.

Dada Dinah, Mwanzoni nilikuwa najisemea mwenyewe kuwa mimi siwezi kuwa na mwanaume anayenizidi miaka saba na kuendelea maana nilikuwa nawaona ni rahisi sana kudanganya binti kwa upeo wangu.


Sasa huyu baba kiumri yeye amesema ana miaka 40 na kitu na mimi nina miaka 27 Je, hii ni sahihi kwa yeye kunioa mimi? na je kwa mtazamo wako huyu baba ana msimamo wa dhati kwangu?
*******************************


Dinah anasema: Habari ni njema tu, asante. Pole kwa kusumbuliwa na Ex, kuna Ex wengine wasumbufu sana. Hongera kwa kuwa na Msimamo ulionao mpaka sasa.


Kutokana na maelezo yako imeonyesha umakini na kutaka kujua "mzigo" alionao huyo Baba (Mjane). Inaonyesha anahitaji "mother figure" kwa ajili ya watoto wake na ndio maana amekuwa wazi tangu mwanzo.


Kitendo cha kuwa wazi na kukuonyesha mkanda wa mazishi ambao atakuwa kakuonyesha watoto wake na kuna maelezo yanayo-support maelezo yake kuwa ndio alikuwa Mfiwa, sioni tatizo hapo.


Umegusia kupima na yeye amekubali kufanya hivyo mkiwa wote nayo pia inatia moyo lakini hakikisha mnapima kweli Usiridhike na kukubali kwake haraka.


Pia ni vema wewe ukachagua pa kwenda kupima bila yeye kujua (kuna watu huonga Madaktari kutoa vyeti "fake").


Tofauti ya Umri sioni kuwa ni tatizo, kutokana na maelezo yako inaonyesha kabisa umekomaa na unajitegemea kiuchumi na kiakili (katika kufanya maamuzi).


Hayo hapo juu yakiwa sorted (ukiwa comfortable) kitakacho fuata ni kuendeleza uhusiano na kujuana zaidi, wewe uwajue wanae na wanae wakujue wewe na wakuzoee/kukubali.


Usiharakishe wala kulazimisha wakupende, kumbuka wamepoteza Mama yao mzazi hivyo wanaweza wakafurahi kuwa na "mama" au kukasirika kuwa umechukua nafasi ya mama yao....yote ni sawa tu, kuwa mvumilivu na muelevu.

Tuone nyongeza ya wachangiaji wengine.

Nakutakia kila la kheri!
------------------

Comments

Anonymous said…
mimi nina umri kama wewe nimewah kuwa na uhusiano na vijana ambao walinizidi kidogo umri bt hakuna malengo wala upendo wa dhati tuliofikia lakini sasa hivi niko na uhusiano na mwanaume mwenye miaka 36 aliwah kuoa na ana mtoto mmoja,aliponitongoza alinieleza ukweli na kwanini ndoa yake haikudumu,kwakweli hakuna uhusiano niliouona bora kama huu,anajua kucare na ni mwelewa sana,ananipenda na nimetokea kumpenda kuliko kawaida na yale mambo ya chumbani ooh ni mzuri ajabu kushinda ata vijana walionipotezea muda kwa sasa tunataraji kuoana siku za usoni.so usihofu fata hisia zako swala la umri its nothing.
Anonymous said…
Mie ninachomshauri huyu dada ni, kwanza asiwe na haraka, avulimie kama amedanganywa na huyo baba atajua kadiri wanazidi kukaa, hakuna linalo jificha, pili mapenzi hayajali umri. hawa serengeti boys ni vicheche sana.
emuthree said…
Tofauti ya umri sio kigezo, ilimradi mnaelewana....
Nikuambie kitu, mtu mzima anajali, na anapenda kikweli kweli, utaona hayo mwenyewe. Cha muhimu, jaribu kuwa naye karibu, muondoe katika huzuni kwa kumjali yale anayoyahitaji.

Hata hivyo,...nikupe kama angalizo, chonde chonde, hakikisha kuwa kama utamkubali, unawalea hawo watoto kama vile umewazaa mwenyewe,maana hawo watoto ndio jicho na kumbukumbu ya huyo baba kutoka kwa mkewe.

Ukiwalea vyema,basi ndio itakuwa njia ya yeye kumsahau mkewe wa zamani na kukuona wewe kama ni huyo aliyekuwa mkewe.
Ni hayo tu kidogo
Anonymous said…
Dada, unampenda huyo bwana? uko comfortable naye? Je unaweza kuwa mama wa watoto wawili?
Jiulize maswali haya kwa makini sana kama unaweyaweza yote kubali, mwanaume mkubwa kiumri aliyefiwa na mkewe hatakusumbua sana (IN MY OPINION)ukilinganisha na wanaume wa umri wako.
Ila usijilazimishe kuingia kwenye uhusiano kwa sababu ya stress za x au ndoa, kwani huyo x dawa yake ndogo tu, mchunie...akipiga usipokee akisms usijibu ataacha. Ndoa hujengwa juu ya upendo wa dhati na si vinginevyo... Kila la kheri
Anonymous said…
Jamaa ameonyesha kuwa ana nia sana na wewe na kiukweli kabisa asingependa kukukosa,MPE NAFASI.Tofauti ya umri sio kigezo cha kukosa FURAHA ambayo umeipoteza kwa miaka mingi.Maisha sasa hivi yamekuwa hayaeleweki kiasi kwamba watu wengi tunakosa MAPENZI NA FURAHA tunayoitegemea kuipata kutoka kwa tuwapendao kutokana na kukosekana kwa UAMINIFU NA MAPENZI ya DHATI.Nasisitiza kwa mara nyingine MPE NAFASI NA UJIPE NAFASI NA WEWE PIA UNAYOSTAHILI.
Mama B wa dar said…
my dear ni kweli kabisa alichokushauri da Dina. Age is not an issue kwani huyo ex wako inaonyesha ni kijana wa umri wako lakini amekubetray mno na mitabia yake ya kishenzi.

kwa huyo mbaba anaweza akawa ana mapenzi ya kweli kwa namna alivyojiexpress, kubwa sana ni kuhakikisha umepima ili kujua afya zenu kabla ya kufanya maamuzi. make sure hushiriki ngono kabla ya kujua status ya afya zenu.

otherwise kila lakheri na ujitahidi kuwapenda watoto wake ili kuwasahaulisha machungu ya kuondokewa na mama yao ikitokea umekubali kuolewa naye.
Anonymous said…
ni vizuri ukapima na ukajenga ukaribu kabla ya kuoana, mimi nimependa kwa ni muwazi, usikilize moyo wako kama umempenda juz go, umri si issu.
Anonymous said…
Pole sana dada kwa yote yaliyokupata kutokana na mpenzi wako. Mshauri wangu kuhusu huyo mchumba mwingine (40 years) mimi kwa muonekano wangu ni kwamba umri si tatizo lakini je Mke wake kafa kwa ugonjwa gani? kuona mkanda si tatizo kwani siku hizi watu walio wengi hawasemi kweli kwamba ndugu kafa na mgonjwa gani? Hivyo usiwe na haraka jaribu kumchunguza kwanza hata ikiwezekana uende mkoa alikotoka ujaribu kuulizia hata majirani upate jibu sahihi. Au kama dada dina alivyokushauri kuwa sehemu ya kupima uchague ww ni sasa kabisa asije akachagua yy akatoa rushwa. Kuhusu watoto utakaowakuta wapende sana kama unavyompenda huyo baba yao, kwani watoto ni malaika hawana kosa. wajali sana.

Nakutakia kila la heri katika mahusiano yenu. Katika yote mtangulize mungu kwani ndiye muweza wa yote Mungu akubariki.