Sunday, 13 May 2012

Ndani ya Wiki mbili kesha "move on" na jamaa kwenye WhatsApp!

Habari yako dada Dinah,

Mimi ni kijana Mtanzania, nina jambo ambalo ningependa ushauri wako. Jambo lenyewe ni kwamba nina mpenzi wangu ambaye tuligombana na tukakaa kama wiki mbili hivi hatuelewani...ndani ya hizo wiki mbili akafanya ngono na mwanaume mwingine.

Sasa baadae, baada ya hizo wiki mbili tulikuja kuelewana tukasameheana yale yaliyotugombanisha. Hapo bado sikuwa najua kama alifanya ngono na mtu huyo mwingine.

Sasa baada ya hapo tukarudiana na kuendelea na uhusiano kama mwanzo, Mpenzi alikuwa anatumia simu ya Blackberry ambayo baadae alinipa mimi niitumie kwasababu yeye tayari alishapata simu nyingine ambayo sio Blackberry lakini anaipenda zaidi. Nikaichukua ile simu nikaweka line yangu ya vodacom.

Cha kushangaza, baada ya siku kama mbili tatu hivi napokea Message kutoka kwa mtu ambaye walikuwa wakiwasiliana kupitia WhatsApp, hiyo message ilikuwa ya kimapenzi...then muda mfupi nikapokea picha mbili ambazo huyo jamaa alizituma.

Hizo picha zilionyesha walipiga wakiwa wote, moja wamelaliana yeye mpenzi akiwa amejifunga khanga moja tu, na nyingine wanakipeana busu yeye akiwa amemkalia huyo jamaa...

Nikaamua kumuuliza taratibu kwanza kabla hata ya kumuonyesha hizo picha, nikamuuliza kama anazijua namba za huyo jamaa nilimuonyesha maana kwenye whatsApp namba ya alietuma inaonekana, akasema anamjua.

Nikamuuliza wakoje naye, akasema ni rafiki tu japokuwa jamaa anamfuatilia mara nyingi kwani amekuwa akimtaka...akakataa kabisa kusema ukweli.

Baadae nikawa mkali na kumwambia tuachane kabisaa aendelee na huyo jamaa yake! Akawa mkali, hapo bado sijamuonyesha zile picha, akawa analia machozi kabisa kila siku ananibembeleza nimsamehe kwakuwa hakuwahi kuniambia kuwa huyo jamaa huwa wanatongozana japo bado hajamkubali.

Ndio siku moja nikamwambia upo tayari kusema ukweli ili nikusamehe?..akasema ndio! basi nikamwambia tukutane sehemu tuongee....ukweli ni kwamba hakuna alichokisema kipya zaidi ya kusisitizia kuwa huyo jamaa yeye ndiyo anaemfuatili (kumtongoza) lakini yeye hamtaki na wala hawajawahi kukaa au kukutana faragha popote.

Nikamuuliza je? nikikuonyesha ushahidi kwamba yule ni bwana yako, nimfanye nini?...akanijibu niachane naye nisimsikilize tena na akasema yeye atakuwa Malaya na hafai...

Mmh nikaguna kidogo, nikamuuliza tena kama kuna jambo ambalo amefanya nae halafu hajaniambia basi aseme lakini wapi...akang'ang'ania msimamo wake.

Ndipo nikamuonyesha hizo picha mbili. Alitahamaki, akaanza kulia na kuoba msamaha tena kwa kunipigia magoti, ila moyo wangu ulishakufa ganzi nilipomuona anajiamini baada ya kupinga maswali yote niliomuuliza wakati ni uongo ambao hata yeye alikuwa akiujua kuwa ni uongo.

Kwasababu baada ya kumuonyesha zile picha tu alianza kulia na kuomba samahani nisifanye yale aliyojiapiza, wakati nilitegemea angezikana zile picha au angalau abishe bishe kidogo lakini alizikubali pale pale na kuanza kulia na kuomba samahani akinisihi nisifanye yale aliyojiapiza...

Hapo mimi nilinyanyuka na kuondoka zangu nikimwambia tusijuane tena...aendelee na huyo jamaa yake...

Hivi ninavyoongea mpaka sasa bado hatuna mawasiliano mazuri, mimi ndio sitaki kuwa naye tena japo roho inaniuma lakini nikimuangalia nasikia hasira sana.

Nimejaribu kumuuliza maswali kadha wa kadha kwamba kwanini na ilikuwaje ndani ya muda mfupi vile alifikia umbali wote huo wa kufanya ngono na mtu mwingine?

Akanijibu eti frustration tu..ndio zimemchanganya akajikuta kafanya hivyo...Mh akilini kweli mimi hainiiingii...Frustration?...Sasa swali langu mimi kwako na hata wadau wengine wanisaidie mawazo.

Je! sio kwamba huyo mtu alikuwa naye muda mrefu tu?...au ni kweli inawezekana ndani ya hizo wiki mbili ndio wamekubaliana na kutiana kweli?...

Na je! ni vyema mimi kumkubali na kumsamehe turudiane kama mwanzo?....je! Inawezekana ndio tabia yake?, kwasababu nijuavyo mimi, mwanamke yeyote anaweza akatongozwa karibu kila siku na watu tofauti, lakini kukubali ndani ya muda mfupi hivyo kumvulia mtu chupi na kufanya naye mapenzi sio rahisi tena ukiwa katika kipindi kibaya umegombana na mpenzi wako ambaye leo au kesho unaomba akusamehe ili mrudiane?

Pamoja na maswali hayo ukweli ni kwamba nimemchukia sana yule dada.

Sasa dada Dinah na Wadau wengine naombeni ushauri...nini cha kufanya hapo?

Natanguliza shukrani zangu, Ahsanteni"
------------------

29 comments:

Anonymous said...

hayo ni matokeo mazuri ya
mabadiliko ya tekinolojia!....hiyo ni tahadhari umepewa..

Anonymous said...

ndugu yangu huyo jamaa alikua nae kitambo tu..halafu kama ulivyosema moyo umeshaingia ganzi na chuki hapo hakutakua na mapenzi tena bali utakua unalazimisha na hiyo itakufanya uzidi kuumia..once ulishachukua maamuzi ni bora uangalie mbele..

Anonymous said...

Pole. Ila mimi binafsi nakushauri achana naye coz anaweza kuja kukuua huyo. Sio mwaminifu huyo, usigeuke nyuma hata kama unampenda, hustahili kula mifupa bali steki, sasa tulia na kaa peke yako kwa muda mrefu then utapata kilicho bora. Huyo watamgonga hata kwa buku browangu. Tc

Anonymous said...

Jembe kwanza pole xana kwa matatzo,ila kuhusu kumsamehe uyu demu wako jarbu kusahau:
kwanza nimuongo,hakupendi,hawezi akakusalti ndani ya wiki mbili jembe,
nakama haukumwonyesha hzo pcha angeendelea kukuambia hana mahuciano nae,na bado jamaa angeendelea kula mzgo taratbu uku bla wew kujua,achana nae malaya uyo,fnd mwngne

Anonymous said...

Huyo demu siyo muaminifu achana naye kabisa kwa week2 ametembea na mwanaume mwingine hiyo inaonyesha alikuwa na mahusiano na huyo mwanaume mwingine kwa mda mrefu so alikuwa anawachanganya wote wawili bila wewe kujua na pia huwezi jua anaweza akawa na mwingine wa 3 na 4 pia siyo mwaminifu na sikuhizi magonjwa mengi sana haina aja ya kuwa naye atakuuwa bure stay away from her, unaumia lakini wewe mwanaume hata ukimuoa huyo hatakuwa mwaminifu kwenye ndoa huo ndio ushauri wangu kwako

Anonymous said...

MWACHE HUYO DEMU SIYO MWAMINIFU HAKUFAI ATAKUUWA BURE KAKA

Anonymous said...

pole kwa yaliyo kukuta.ila kila mtu akiwa na matatizo,ana njia zake za kukabiliana na matatizo.inawezekana ni kweli frustration zake zilimfanya afanye hivyo.jee kwa nini hakutaka kuendelea nae huyo jamaa?na akuchagua wewe?inawezekana ni kweli yalikuwa ya mpito kwake.kuna wengine wakiu dhiwa wanaishia kunywa pombe.wasiwasi wangu hata ukirudiana nae,hautomuamini tena.maana anajua kujikausha akiongopa kitu.maybe aliogopa akikueleza ukweli ungemuacha

manka said...

pole kwa yaliyokupata ..mimi mwenyewe nimeshakua kwenye hio situation niligombana na bf wangu akanikashif na kunitolea maneno machafu ambayo hata hayaendani na kosa nililofanya

nikiwa na bf wangu kulikua na jamaa alionesha kunipenda kweli na kunijali hata kuliko bf wangu

basi mm kutokana na hasira na upweke na nikikumbuka kashfa na maneno machafu aliyonitolea huyo bf wangu nikahisi kama kuchanganyikiwa na tayari tulikua tumepanga kuoana mwakani

kwa wakati huo yule jamma aliekua akinipenda alikua karibu sana na mm kuniuliza siku hizi naona haupo sawa, kuna tatizo gani ila mm sikumwambia chochote na alikua akinipigi sim mara kwa mara kunijulia hali kunitoa out weekend

wakati huo mi nasubiri kama bf wangu labda atabadilisha mawazo wiki ya kwanza ikapita ya pili ikapita na jamaa anatake good care of me kuliko hata bf wangu na wala sikuwahi kufanya mapenzi nae

nikikaa nae anasismka anadindisha mboo hata masaa mawili mpaka namuonea huruma nilipoona kimya kimezidi kwa bf wangu wiki ya 3 nikaamua kumove on na yule jamaa
ananipenda nampenda mpaka naona raha duniani kuliko hata nilipokua na bf wangu..

baada ya miezi miwili ndo bf wangu eti ananitumia meseji ya nimekusamehe naomba tuonane tuendelee na mapenz yetu..nikamjibu kumuuliza ulivyokaa kimya mda wote ulitegemea me nifanyeje nlikua nikimpigia sim hapokei wala mesej hajibu

mpaka sasa nipo na huyo jamaa tumeoana na maisha yanaenda vizuri yy amebaki na chuki moyoni hata nikimsalimia ananipita

ushauri wangu kwa huyu kaka ni kwamba kama kweli unampenda huyo dada na una uhakika na yy anakupenda sioni shida ya ww kutokumsamehe.kwa mm naweza kua na mwanaume nikafanya nae romance nikambusu na wala nisikubali aniingizie uboo wake..labda hizo zilikua ni picha tu na wala hawakufanya mapenz i can tel u kua na uamuzi mapeme usiseme mara unamwacha mara unampenda utakuja kujuta utakapomwona na mtu mwingine tene wanafuraha kuliko hata akiwa na ww
life is too short kaka hamna anaetaka kukaa kujiumiza kumwaza mtu ambae hamjali

Gerry said...

pole kaka kwa matatizo ,hayo yalishanikuta hata mimi.kwa upande wangu ninaweza kukushauri yafuatayo:

1.sioni logic ya yeye kusema frustrations ndo zimepelekea yeye kufanya aliyoyafanya,its seems uhusiano walikua nao hata kama haukuwa strong as u but lazima kuna namna flani walikuwa wanarelate,so uaminifu ni mdogo hapo,

2.Pili, msichana angekuwa muungwana angesema ukwel,truth sometimes heals and sets u free,ukiambiwa ukwel unajua how will u handle the issue kama ni kusamehe au laa,lakin uongo hupoteza uaminifu, so ni vigumu kuendelea kuamini kama hata ukimsamehe hatofanya aliyoyafanya,

so pima maamuzi yako kwa kuangalia nini ulitarajia toka kwake na vigezo vyako vingine ni hayo tu

lady h said...

huyo hakufai kabisa kaka cose hapo hata hamjaingia kwenye ndoa then anasema frastration, for only 2 weeks jaman huyo kiboko! Tafuta mwingine, ila na ww kama huwa unamcheat msamehe manake mkuki kwa nguruwe kwa binadam mchungu! POLE SANA

Anonymous said...

Pole mdau

manjaumdogo said...

mimi mawazo yangu nikama ifuatavyo nikiwa kama mwanamke ni vigumusana mtu kutoka kwenye relation hapohapo akaingia kwenye relation nyingine while ile alikua akiipenda kawaida lazima atahangaika kurudisha ile hapo nilazima jamaa walikua na mahusiano so alikua na wewe pamoja na huyo na tatizo lingine nikwamba mwanamke si mkweli hata kukushauri uwenaye tena ni issue kwani sidhani kama atakua ameachananaue kwani kama angekua mtu mwenye uelewa na jamaa alikua akiwasilianannaye kwa watsapp

Lazima wakati umemuuliza kwamba huyumtu unamfahamu angewezakuwasiliana na yule jamaa akamwambia asitume tena sasa naona umesema jamaa aliendelea kutuma duh hapa ni pagumu mwambie akuwekewazi kama bado unampenda na akukutanishe na jamaa na amwambie ukweli so utagundua kama jamaa alikutana naye for shot time ama laa

haya nimawazo yangu thanks

Anonymous said...

Duh! huyo ni muongo sana hafahi wiki mbili ni chache sana, ajatulia huyo hakufahi. Jiulize sasa hakiwa mke ukimkosea je atatoka na mtu mwingine na bila haya uhusiano wa muda mchache tu keshapiga picha huyo msichana kakuweka kwenye list yake tu lakini hakupendi

Rehema said...

Kwako Ndugu yangu,

Mimi ni mwanamke kwa kweli nimesoma maelezo yako yanasikitisha sanaaaaa.

Sina haja ya kueleza maelezo mangi ila kwa ufupi tu huyo Mwanamke hafai kwa sababu kuu kwanza kwa kipindi cha mda mfupi kama huyo yeye tayari kaishatembea na mtu ni HATARI SANA. Mtu yeyete unapokorofishana na mwenzio inatakiwa huwe na subira kwanza sio haraka haraka kama hiyo. Kweli anasikitisha sana, eti frustration! hajui maana ya frustration. Frastrution inakuja kama mtu ulikuwa na mpenzi wako kwa mda mrefu sanaaaa au mke wako au mme wako, kisha yakatokea mambo ya kugombana inaweza ikamtia mtu kuchanganyikiwa na hata hiyo frustration haiwezi kuja haraka haraka kiasi hicho inachukua mda ndio mtu unaona afanye nini?

Basi kama hivyo anatisha huyo inawezekana alikuwa tayari na huyo mwanaume mda mrefu au inawezekana katika kipindi hicho cha mda mfupi ndio akafanya naye mapenzi.

Na pia Kaka yangu ujaribu kutafakari kwa nini huyo Mwanamke alikupa simu yake wakati anajua huyo mwanamke aliyefanya naye mapenzi yupo na number zake? huwo ni ujinga sana. Inawezekana alifanya makusudi ili kukuumiza wewe au aachane na wewe, sasa tena kule alikofanya mambo hayo pia mambo sio mazuri sana kama wewe haijulikani hapo.

Mwambie atulie uhuni aufahi na tamaa haina faida sana sana unajisumbua tu mwili wako na kupoteza mda kwa mambo ya ajabu. Wanawake ni walewale na wanaume ni walewale. Uzuri wa mtu na utamu wa mwanamke kule chini ni kujituliza kwani unapoangaika na wanaume hovyo hovyo hata huku uchi unakuwa sio mtamu maana unapanuliwa na haina tofauti ya mboo, lakini unapokua na mtu mmoja tu yaani uchi wako unabakia kuwa swafiiiii. Wee angalia ukikaa week moja bila kufanya unakuwa safii lakini ukifanya leo kisha jioni tena hakuna utamu kwa kweli.

LEO HAFANYE NA MWINGINE KESHO KUTWA AFANYE NA WEWE SASA MAMBO GANI HAYO? AMEPOTEZA UAMINIFU.

Lakimboria said...

dah!kama yeye alivyo sema ni malaya wa kutupa na hafahi,Hapo Hamna mjadala huyo ni kicheche Brotha.
wanawake jombaaa...wana tatizo moja husahaau kabisa kwa mda mfupi halafu akishafanya ufuska akiona jamaaa hajamridhisha kama wewe unavyo mridhishando'anakukumbuka...na kuamua kurudiana na wewe.
Huyo ni kigeugeu hafahi anajirahisisha mno'find mwanamke mwingine mwenye maarifa.
wana HIPHOP tunakwambia MWANAMKE MZURI APATE UFAHAMU YOOO.

Kwako Kaka,

Nimesoma maelezo yako kwa kweli inasikitisha sana. Sina haja ya kueleza maelezo mengi ila kwa ufupi tu huyo mwanamke hafai kwa sababu kuu kwa mda mfupi kama huwo umegombana naye basi tayari yeye kaisha tembea na mwanaume mwingine basi ni hatari. Na kisingizio ni frustration; frustration inakuja yaani mtu uchanganyikiwe kweli kweli kwa mfano kama una mtu kwa mda mrefu sana au mke wako au mme wako kisha mkorofishane inaweza ikatokea lakini hata kutokea kwenyewe si kwa mda mfupi kama huwo yaani mpaka mtu usote kweli kweli ndio inaweza ikatokea hivyo. Mtu unapokorofishana na mwenzako inatakiwa kwanza subira na kushukuru Mungu yaliyotokea kisha unatulia. Lakini ghafla tu umegombana basi wewe mwanaume yupo wapi tayari unafanya naye mapenzi anatisha kwa kweli. Na frastrulation nyingine inakuwa kama uko na mpenzi wako lakini yeye hapendi mfanye sex na kila ukimuomba yeye hataki basi mtu unashindwa ufanyeje maana itakutuma kama mwenzie hakupendi ndio unaweza ukafanya hivyo. Na hivyo hiyvo pia sio kwa mda mfupi kiasi cha namna hicho. Tafikiri ana Jini la mahaba Bwana? Kumbe sio ni kuendekeza uhuni na tamaaa tuu.

Kwa mtazamo wangu mimi sikubaliano na hilo jambo mwambie ajaribu kutulia ina maana mkikorofisha tena hatafanya hivyo hivyo au mkija kuoana pia mkikorofisha hatafanya hivyo hivyo na ndoa ina raha yake na pia ina karaha yake kubwa sanaa. Itakuwa basi hatari:

Hivyo hivyo kaka yangu mpenzi jaribu pia kuangalia hilo swala itakuwaje yeye hakupe hiyo simu yake utumie wakati anajua yupo mwanaume alifanya naye hayo mambo ya ajabu, wakati anajua anafahamu hiyo number, ukute alifanya makusudi ili kukuonyesha tu wewe kukuumiza au kuachana na wewe, na kwa bahati mbaya pengine kajilaumu pengine huyo mwanaume hakufikii wewe kwa upendo au mapenzi au vyovyote vile anavyoona yeye. Ndio maana yeye sasa anajuta.(Hapo mbele nilisema mambo ya ajabu maana week mbili tu jamaa tayari frusration mmmmm).

Na kama kuhusu huyo jamaa inawezekana alikuwa anamfahamu siku nyingi na ndio kalikuwa kamtindo kake kufanya naye sex huku yupo na wewe AU inawezeka pia katika mda wa week mbili ndio alikumbana na huyo jamaa ndio akafanya hivyo.

Kijana tafuta mtu mtulivu na mvumilivu. Uvumilivu ni jambo la maana sana kama mwanamke anauvumilivu hataendeshaje maisha kwa mtindo wa frustration.

Ahsante

mandy said...

dah.pole sana kaka huyo msichana ni muongo ila me kwa ninavyojua wanaume wengi hua hawawez kusamehe sa aliona angekwambia ukwel kabisa usingemsamehe hata iweje lakin kumbe tayar ulikuwa na ushahid...kukudanganya kwake inawezekana isiwe kama ndo tabia yake ilivyo ya kutembea na wanaume ila inawezekana bali uoga wa kwamba ungeweza kumuacha..kosa lake kubwa ni yeye kupiga picha kama hizo na huyo mwanaume alikuwa anafikiria nini hapo..yeye ndo anajua
pia kwa kusema frustration do zilimsababisha akatembea na mwanaume mwngine inawezekana ni kwel wanawake wengi wana tabia hiyo hasa wakiona kuna hali ya tofauti kwa mpenz wake inawezekana alihis unamwanamke mwingine au vyovyote ili kutuliza akil yake akaona ni sawa na yeye kuwa na mwanaume mwingine kama kukukomoa vile lakin kumbe anaharibu..
fikiria sana kabla hujachukua uamuzi wa kumuacha au kuendelea nae

Anonymous said...

malaya tu huyo hkn k2 hapo

Anonymous said...

Mmmmm dada Dinah, hii kali, lakini kiukweli huyo bi dada aseme ukweli tuu...huyo jamaa mwingine alie move nae kipindi ambacho amegombana na mpenzi wake hawezi akawa mtu mpya, lazima atakuwa alikuwa nae siku nyingi nyuma kabla hata hawajagombana. Na pia ninavyoelewa mimi, msichana akigombana na mpenzi wake ambae anampenda kweli hawezi ndani ya muda mfupi hivyo eti akamsahau akampenda mtu mwingine..hilo haliwezekani kabisa..huyo atakuwa anamahusiano naye kwa muda mrefu au kama kweli ndani ya muda mfupi hivyo ameweza kuanzisha mahusiano na mtu mpya na wakafikia kufanya mapenzi basi hakuwa anampenda mshikaji waliegombana naye, au atakuwa malaya...yani ndio tabia yake...
So ninachomshauri mshikaji yeye aendelee na maisha yake tuu...japo roho inamuuma lakini lazima akubali ukweli tena mapema maana baadae huwezi jua kwa akili hiyo ya huyo dada atafanya nini ambacho ndio kitamuumiza zaidi, yaani hafai na wala hilo hawezi kudanganya kwa kweli...natamani ningeweza kupata contacts za jamaa hata email tuu angalau niwe nawasiliana naye....
kweli inauma sana....lakini ndio maisha wakati mwingine inakubidi uchukue hatua au ufanye maamuzi magumu ili maisha yaendelee...ila huyo dada hafai, huwezi kugombana na mpenzi wako ndani ya muda mfupi hivyo eti unaenda kwa mwanaume mwingine unafanya naye mapenzi...kisingizio eti frustration...jamani frustration si ndio zinazomfanya mtu ashindwe kuduu...maana pale unakuwa haupo normal huna feeling zozote za kimapenzi na kwasababu umegombana na unayempenda basi mtu utakayekuwa unamuwaza akilini ni huyo huyo unayempenda ambaye mmegombana na si mwingine, mwingine yeyote akija huwezi hata kusikiliza achilia mbali kumkubalia...aisee huyo itakuwa ndio tabia yake, au lazima huyo jamaa aliemove naye alikuwa naye hata kabla ugomvi wao....
Jamaa nampa tano, aachane naye kabisaa...mungu atamjalia atasahau yote hayo...kwani kila jambo hapa duniani ni la kupita tuu...asiumie sana kwasababu huyo dada hafai...wiki mbili ni chache sana kufanya maamuzi kama hayo...
pole sana jamaa yangu...

Anonymous said...

Hi
Mimi ni mvulana napenda sana wanawake kwa umbile na kwa matukio siwezi kujiziwia kuwafikir kindanai na kinje, nikimuona mwnamke mzuri yaani kaumbika basi na simamisha na huona aibu, nifanye nini hata niache tabia hii.

Anonymous said...

hUYO DADA HAKUFAI KWA SABABU ULIMSIHI KWA APENZI ANGEKUWA MWAMINIFU KWAKO ANGEKUBALI KOSA NA KUKUOMBA RADHI KABLA YA KUFIKA HAPO ACHANA NAYE ATAKUWA MWOINGO SIKU ZOTE NA LABDA BADO ANAO WENGI ILA TU HUJAPATA USHAHIDI TAFUTA POLEPOLE UTAPATA MWAMINIFU

Anonymous said...

hapo inawezekana ni stress bt huyo dada ilibidi akuambie ukweli coz jinsi ulivyokua unamuuliza ni dhahiri kwamba unajua nn kimetokea,nahis alishakua nae hata wakati mpo sema mlipo gombana ndo akatake advantage zaid

Anonymous said...

Achana na hiyo mambo! Huyo c mwanamke kaka! Mimi nlkuwa na grl wangu tunafanya biashara tena vjana wadogo wenye mafanikio makubwa, kiumri ninamiaka 25 na yeye 23 wote wachaga lkn c mwaminifu kwani nlkuta anatoka na mfanyakaz wangu wa moja ya maduka yangu ckuamin na kwa kuwa tulkuwa na malengo nlimfukuza kijana huyo na kumrudisha kwao Mosh baada ya muda nkaja kugundua kamrudisha nakampangia nyumba Mikochen kwa siri. Bob kiufupi achana nae kabsa na uwaze maendeleo kwanza achana na hawa kuku wapo wengi wanatfa mwanaume mwaminifu wa kuish nae wanakosa. Call me Mimi