Thursday, 12 April 2012

Safari ya Ughaibuni imebadili Mume wangu!

Habari za kazi dada Dinah, mimi nina matatizo na ndoa yangu niliyofunga mwaka 2009 mwezi 4 Kanisa la Romani Katoliki.


Mwaka 2010 nikapata post ya kwenda nje ya nchi kwa mkataba wa miaka 2 , baada ya kuondoka nilikuwa napata likizo ya siku 21 au wiki moja. Chakusikitisha tangu mwaka jana mume wangu alianza kubadilika.


Nikirudi likizo mara ananiambia nenda kwenu ukawatembelee. Naweza kukaa wiki nzima lakini anafanya sex na mimi mara 1 tu mpaka naondoka.


Mwaka jana mwezi wa kumi na mbili nilipata taarifa kuwa amezaa na mwanamke wa pale mtaani kwetu na mtoto anamiezi 3.


Mwezi wa kwanza tarehe 12 alikwenda kumtabulisha kwao kijijini pamoja na mtoto na pia hapo hapo ana mwanamke mwingine anamimba anakaribia kujifungua na hao wanawake wote huwa anawaleta pale kwenye nyumba kwetu wanalala kitandani kwangu!


Mimi nategemea kumaliza huu mkataba mwezi wa sita mwaka huu, nimejaribu kuongea na mume wangu na amenitamkia kuwa hanitaki tena.


Nimeongea na wazazi wake mpaka sasa sijapata jibu lolote, roho inaniuma sana kwani nilipokuja huku tulikubaliana vizuri.

Sasa hivi nikienda likizo anafunga chumba hataki nionane naye, nikipiga simu ananikatia,nikituma sms hajibu, naomba ushauri wako dada maji yamenifika shingoni dada.

****************************

Dinah anasema: Pole sana kwa matatizo unayokabiliana nayo. Sina hakika ni kitugani hasa kilipelekea ninyi wawili kufunga ndoa...kwani si ndoa zote zinafungwa chini ya misingi ya mapenzi...wapo wanafunga kwa ajili ya kuanzisha familia? Kurahisisha maisha(pesa), Umri, Mkumbo, kuondoa mkosi n.k


Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa hamkuwa na muda wa kuzungumza au kuwasiliana kama pea na pengine hamkuweka au hamkuwa na nia/mipango inayofanana ya kimaisha hapo baadae.


Inaonyesha mumeo alitaka sana kuanza familia na wewe ulitaka career vyote ni vizuri na ni muhimu ila vimekutana wakati mbaya na labda kwavile hamkujadili haya mwanzoni kabisa mwa uhusiano wenu kabla ya ndoa.


Hongera kwa jitihada zako za kutaka kurudisha ndoa yako, hakika inauma lakini suala zito kama hili huwezi kulizungumza wakati wewe mwenyewe uko mbali.


Ni vema kuzungumza na mumeo na wakati huohuo kujaribu kuwasiliana na aliewafungisha ndoa Kanisani au wale waliowapa Semina kabla hamjafunga ndoa.


Natambua Ndoa za Kikatoliki zina hatua zake, basi ni vema ukijaribu kuzifuata mara utakaporejea nyumbani.


Umejaribu kuzungumza na wazazi wake ambao kwao kidogo inaweza kuwa ngumu kufanya chochote kwani hujui mtoto wao(mumeo) amekuzungumziaje kabla ya kutambulisha mwanamke mwingine na mtoto.

Muombe Mungu akutie nguvu kipindi hiki uko mbali kikazi lakini pia shukuru kuwa mumeo anakukwepa kwenye kufanya mapenzi...:uwezi jua anakuepusha mangapi.


Maneno yangu sio sheria, lakini nashindwa kujizuia kusema haya:-

Mwanaume aliekosa uaminifu kwa mkewe na kungonoka na wanawake ovyo na hata kuwapa ujauzito hafai kuwa Mume.


Unaweza kushawishika kupigania penzi lako na hata kushika mimba ili umpe mumeo mtoto so that ndoa iokolewe lakini baadae ikakuongezea matatizo zaidi.


Hatua mliyofikia sidhani kama kuna umuhimu wa "kupigania penzi" ni vema kuanza maisha yako upya.


Kisheria unaweza kumtaliki mumeo lakini Kikristo huwezi kufanya hivyo. Sasa kwasababu imani yako ya Dini inakataza Talaka haina maana uendelee kuishi mpweke ndani ya ndoa.

Tusikilize wengine watasemaje...
Pole na kila la kheri!!
------------------

17 comments:

Anonymous said...

Dada apa tunaona unalaumu zaidi mmeo kwa maana unazungumzia upande mmoja wa shilingi je kwa upande wako uko ulipo uko safi?

Anonymous said...

umemwelezea vizuri lakini sijui ni kanisa lipi hilo halikubali talaka. Mimi sio mkatoliki lakini nafahamu watu wengi wenye talaka katika kanisa hilo..na moja ya kuruhusiwa na kuwa kama mtu alificha ugonjwa mkubwa bila kumwambia mwenzake, kutoka nje ya ndoa inaweza kukupatia talak. Inachukua muda mrefu sana baada ya councellings na kila kitu lakini ni bora ufuate hiyo njia halafu uwe peke yako na baadaye upate mtu atakayekupenda na kukheshimu wewe. Kweli ushukuru Mungu sana hakukuletea mengine. It could be worse.Just imagine sasa hivi ungejua ana mtoto nje na wewe una ugonjwa?

Anonymous said...

Dada yangu wewe si wakwanza hata mimi yamenikuta makubwa kushi

Anonymous said...

Dads yangu acha kuumiza kichwa

Anonymous said...

pole sana dada yangu kwa mkasa huo uliokufika kwani naelewa uchungu wake kwa undani.

inaelekea kwa namna fulani mumeo alikubali uende ughaibuni either kwa wewe kulalamika sana, nae akakosa uwezo wa kukuzuia na kwa wakati huo bado ndoa yenu ilikua mbichi sana ambapo alikuhitaji kupita kiasi.

kwa kusema hili sio kwamba nakubaliana na ushenzi alioufanya...lah no, amefanya makosa makubwa hasa kuzaa na mwanamke mwingine, kumtambulisha kwao wakati akijua kua ndoa yenu haijavunjika na bado kumpa mimba mwanamke mwingine kwa hili sidhani kama anayosababu yoyote ya kukueleza kwani ni umalaya na uhuni.

yapo mengi ninayoweza kukueleza ila kwanza tuliza akili zako kwa kila njia unayoweza and then umalize mkataba wako na urudi nyumbani

jiweke katika mazingira ya kujiamini na kua na msimamo thabiti kwani hata kama bado unampenda huyo mtu, yakupasa ukumbuke kua kwa sasa atakua na watoto wawili wenye mama tofati, unaweza ukampenda yeye na kumsamehe ila itakapokuja ishu ya hao watoto waweza ichukia ndoa yako daima.

ukiwa jasiri na msimamo utagundua pia msimamo wake na hivyo itakusaidia zaidi kufanya maamuzi kulioko kung'ang'ania penzi mfu.

njia zote muhimu zikishindikana as you want mpe talaka na uanze maisha yako mapya. kila kitu kinawezekana hata kwenye bible kumeandikwa "waweza mtaliki mkeo kwa uzinzi tu" so the same alichokifanya huyo ni uzinzi mkubwa sana and as per your wishes waweza mtaliki.

ila mengineyo angalia upande wako pia coz sometimes matatizo yanapotokea kama hayo waweza kuta mnahusika kwa pamoja kwa namna moja ama nyingine kuyasababisha.

Eddy

Anonymous said...

Mi naunga mkono ushauri wa dinah....haina haja ya kupigania penzi la mtu ambaye tayari ameshazalisha mwanamke nja na mwingine ana mimba atakuletea magonjwa tu bure na ameshakutamkia wazi hakutaki tena. Ni bora ukirudi uendele tu maisha yako kama wewe vitu vinatokea kwa sababu kwa hiyo huwezi jua mungu anamakusudi gani na wewe inawezekana anakuepushia makubwa zaidi. Utapata tu akupendae kiukweli. Pole sana

Anonymous said...

Dada, japo mimi ni mwanasheria kabla ya kuzungumza kisheria kwanza naamini Mungu yupo so namshauri huyu Dada kwanza amuombe Mungu ikiwa ni pamoja na kufunga NOVENA, atampa njia ya kutokea. Ni kweli ndoa za kikristo hazivunjiki, lakin kuna mazingira yanayoruhusu hivyo, endapo mmoja wao atakuwa mzinifu, basi hapo ndoa inaweza kufika mwisho, nina mfano wa jirani yangu hapo napoishi, yeye ni mchungaji maarufu tu! na anahubiri sana, alimtaliki mke wake sababu ya uzinifu. Hata nimesikia japo sina uhakika yule muhubiri maarufu marekani na duniani Ben Hin amemtaliki mke wake na kuoa mwingine japo sijajua sababu. Dada mimi ni mwanaume na huu ulimwengu kuna mambo inabidi ufanye maamuzi magumu wakati mwingine, wanawake wengi viruka njia hebu fikiria kawapa mimba wawili na hao wanawake wana wapenzi wa nje japo mmoja kila mmoja, na hao wapenzi wa nje nao wanawapenzi wa kuzugia japo mmoja kila mmoja, unaona mtandao huo wa ngono, sasa ukimwi umekosekanika hapo, kuwa firm focus on issues na hata kama akikubali kurudiana na wewe mkapime msiwe mnajirahisi kina dada nyie ni wa thamani sana, japo mmefunga ndoa isiwe kigezo cha wewe kuteswa, Mungu alisema tiini mamlaka iliyopo ndoa ya kikristo huwa inavunjwa kwa sheria za nchi, japo wateja wangu wakija ofisini huwa nawashauri sana wapatane na ikishindikana no way out, maana inaonekana bado mdogo utakufa na ukimwi bure dada na inaelekea familia nayo haikutaki maana ni jamb o kubwa sana na baba mke angeingilia kati kama ni mtu smart. Utakuja wekewa sumu bure. Ni hayo tu, its mi Izoo wa mjengoni, Dodoma.

Anonymous said...

Dada jikaza na uchukue maamuzi magumu, huwezi ukamnang'ania mtu katika mimba wasichana wawili, mbona kwa uzinzi ndoa inavunjika na utampata mwingine anayekupenda kupita kiasi mpaka utashangaa.

Anonymous said...

aliyosema dada dina,ni kweli kabisa cha msingi tafuta msingi mwingine ili upate furaha na amani ktk maisha yako ya wawili kwangu mie sioni haja ya kuendelea na huyo mzinzi au bwanahewa!tafuta kwingine ni hayo tu chagua kunyoa au kusuka.

Anonymous said...

samahani kwa maelezo yangu,ila ukirudi jaribu tena kwa mara ya mwisho.kama hakuna usulisho,mshukuru mungu,anza maisha kivyako.na ikibidi omba talaka mahakamani.hizi ndoa nyengine za kusema hakuna kuachana kwa upande mwengine zinadhalilisha.iweje wewe utulie,mwenzako ahangaike nje.ukilalamika unaambiwa vumilia.raha ya ndoa ni furaha.utaishije ndani ya ndoa ambayo haina furaha yoyote?na mara nyingi,lawama zinaangukiwa kwa mwanamke.huyo mumeo hajatulioa,na hatotulia.iweje akamu introduce m.ke mwengine mwengine na wakati anajulikana ana mke?inashangaza kwa kweli

Dondola said...

Haha nacheka lakini najua ni jambo baya na sio zuri na linaumiza...ukweli unabaki pale pale kama alivyoongea dada Dina, kwamba inawezekana misingi ya ndoa yenu haikuwa dhabiti...na mpaka mkafikia kufunga ndoa hamkuwa mmejipa muda wa kutosha kujuana vizuri..yaani mlifunga ndoa yenu kwa misukumo mingine tuu, possible wewe ndio ulimpenda yeye hakukupenda kwa dhati na alikuwa na mipango mingine ndani ya kichwa chake..
Kingine, hakuna mahali katika maandishi matakatifu katika dini yoyote inakulazimisha uishi na mtu kama huyo wakati hatari unaijua...japo lengo la kuoana ni kuishi pamoja milele kwa raha na shida lakini kiliwekwa kikomo...kwahiyo sheria inayobana ni ya kanisa tuu lakini kwa mungu una haki zote mamii....unaweza kutemana naye tuu ukaanza maisha mapya tena mungu akayakubali na kuyapokea...sio hayo mnayoishi sasa ambayo sidhani hata kama anayapenda...kwanza ni hatari, pili ni magumu utaendelea kuumia tuu, tatu jamaa ameshasema hakutaki, shukuru mungu kwamba amefunguka moja kwa moja japo inauma lakini ukweli ndio mzuri...sasa ukiendelea kung'ang'ania yanayofuata ni majuto..utatamani bora ungejiengua mapema...
Mapenzi yanauma lakini amini hapo huna chako, kubali hasara yaishe uanze upya wangu....

Anonymous said...

pole sana ndugu yangu, hayo mambo yanaumiza sana maana hata mimi yamenipata. kwa kweli yanafana. mimi pia naishi miji tofauti na mume wangu, kazaa na wanawake watatu wote mimba zimepatikana kupitia kitanda changu! mwanamke mmoja housegirl, mwingine rafiki yangu jirani yangu na mwingine wanafanya kazi ofisi moja. Inaumiza sana lkn muombe Mungu akupe faraja, usichukue maamuzi ya haraka ya kumuacha, fuata maelekezo ya dada dinah, njia ya mazungumzo. Lkn kama mwenyewe kasema hakutaki basi usilazimishe mapenzi. mimi mwenzio bado tunaishi pamoja na mume wangu, tuligombana akatubu na kulia sana na kuniahidi kuwa amekoma. na kweli naona mabadiliko kwake na anipenda sana. sio siri mambo hayo yanatesa sana, hususani kwa sisi ambao hatuna tabia ya umalaya. Kwa wanawake waliozoea ku share hilo sio issue.pole my dia, Mungu atakufariji.

emu-three said...

Hapo ndipo unapoona usemi wa ndoa ndoana....lakini ni vyema ukalizungumza na wazee wa pande zote mbili, ili yote yawekwe hadharani, na ikiwezekana wawepo wakuu wenu wa dini, ili waone jinsi gani ndoa hiyo itakavyokuwa...maana hapo kutokana na imani yenu kuna mambo yakuwaza;
-Imani yenu hairuhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja
-Imani yenu haijui kutalikiana,kuachana...imani zote haziPENDEZEWI NA HILO,ILA IKIBIDI ...
Kwahiyo ndio maana naona kamainawezekana, mkutane wazazi wa pande zote na hawo wakuu wa dini zenu, ili wajadiliane..na hatima itajulikana. Ndio ushauri wangu huo
Tupo pamoja ndugu yangu muda sijaongea hapa kijiweni, lakini tupo pamoja

Anonymous said...

Pole sana rafiki. Mimi niko nje nafanya PhD itakayonichukua miaka 4. Lakini mume wangu anapenda nisome; japo najua kuna vishawishi viiingi wana ndoa wanapokuwa mbali na mimi naona hii elimu ni muhimu kwangu, kwake na kwa watoto wetu. Inawezekana kabisa mume wangu anacheat nikiwa mbali (kwani wanaume ni very weak) lakini najua ananipenda saana and that is all I need from him at leat now that I am far.

Kuhusu wewe mpenzi, nakushauri uachane na huyo mwanaume. Kwa sababu amna watoto hence wewe huko mre free to move on. Pili mumeo hakupendi na amekutamkia wazi.

Wanaume ni wengi na huyo si wa mwisho. Wewe mchukulie kama ilikuwa mistake wewe kuolewa nae. Na wala usijutie kuwa wewe ni sababu ya ndoa yako kuvunjika kwa kuwa umeenda kufanya kazi mbali kwani wewe si wa kwanza na si wa mwisho kufanya hivyo.

Mwache ahangaike na hao wanawake zake. Huyo ni malaya maana kama suala lingekuwa wewe huko mbali basi angekuwa na mmoja; sasa iweje kazalisha wanawake wawili???

Hata ungekuwepo huyo bwana angekupa za uso live. Mwache utanambia baada ya miaka mitano jinsi dunia itakavyomfunza adabu; wakati huo wewe akha maisha yanakunyookea ukiwa Mrs fulani na watoto juu.

Anonymous said...

kweli inaumiza sana maana hata mimi yameshanikuta kama yanayokukuta, na pengine ya kwangu yakawa ni makubwa zaidi.hivyo ukae ukijua kuwa wewe sio wa kwanza kukutwa na hayo. pole sana.fuata maelekezo ya dada dinah, ikibidi kuacha mahusiano usisite, kwani mapenzi hayalazimishwi, ukilazimisha utaumiaaaaa!

Oluwakemi said...

Mama rudi home funga vilago vyako anza life yako peke yako, he is NOT worth it

Oluwakemi said...

mamaa, waambie ndugu zako wakutafutie nyumba huku bongo, maliza mkataba wako huko, rudi home move out, that man WILL KILL YOU.