Sunday, 15 January 2012

Wivu

Mambo vipi!

Hebu leo tulizungumzie hili suala la Wivu, natambua watu wengi wanaamini kuwa Wivu ni chanzo cha kufarakana na kutokuelewana. Baadhi huamua kuficha hisia hizo za wivu kwa vile wanaogopa kuachwa na wenza wao.

Vijana wa sasa ndio wanaongoza kwa kupinga hisia hizi za wivu, lakini tukirudi nyuma enzi zile za Hayati Bibi yangu kumfanya mtu akuonyeshe wivu ilikuwa ni sehemu ya mapenzi na ikiwa mpenzi wako hakuonyeshi wivu ni dalili kuwa humvutii tena (namna ya kumfanya mume awe na wivu ni somo kwenye kufundwa).

Pia wapo wanaopenda kuweka "Wivu" kama ubora wa hali ya chini sana kwenye uhusiano wa kimapenzi na hata ndoa. Ukifuatilia kwa ukaribu utagundua kuwa sehemu kubwa ya watu wanaopinga hisia za Wivu kwenye uhusiano ni ama wanawapenzi zaidi ya mmoja au hawajui Wivu ni nini? kama sio wanachanganya wivu na kuwa "obsessed"(kwa kiswahili ni?).


Inashangaza unapomkuta mtu anataka mpenzi wake awe mlevi wa penzi lake (addicted) lakini hataki mpenzi huyo awe na wivu juu yake....hapo huwa najiuliza ikiwa unamkolezea mwenza wako mapenzi motomoto kiasi kwamba unakuwa "tiba" yake na bila tiba hiyo hajiwezi tena, kwanini asiumie kihisia ikiwa haupo karibu yake au umechelewa kurudii nyumbani?


Wivu ni hisia kama ilivyo penzi, hupangi au kuchagua bali inatokea tu. Wivu mara zote uhusisha mtu wa watatu, inaweza kuwa jirani, rafiki, mfanyakazi, mpenzi wa zamani n.k.

Wivu hauna tafsiri wala sababu kama ilivyo kwenye hisia za kimapenzi, anaekupenda siku zote huwa hana sababu ya kukupenda bali hutokea tu anakupenda, japokuwa kukupenda huko kunaweza kuongezeka siku hadi siku kutokana na matendo mema au mapenzi unayompa n.k basi hata wivu ni hivyo hivyo na huongezeka kutokana na matendo mema na mapenzi unayotoa.

Wivu unaweza kuwa maumivu ya hisia (mtu unakonda tu...lol), hasira, Uoga, hofu, na huzuni. Vilevile wivu unaweza kujionyesha kwa mhusika kuwa mfuatiliaji, muuliza maswali, uhakiki wa muda/mahali au kutaka kujua maisha ya mpenzi wako ya kimapenzi kabla yako.

Wivu unahimarisha uhusiano na kukufanya uhisi/ujue kuwa mwenza wako anakujali, inakufanya wewe mpenzi kuona namna gani unamrusha roho japokuwa mmekuwa pamoja kwa miaka mingi.

Wivu mzuri nii ule unaokwenda sambamba na na mapenzi na kujaribu kumsukuma mtu wa 3 ambae labda humuamini mbele ya mpenzi wako kutokana na mazoea yao.

*Kuna ila hali ya kutomuamini mpenzi kwa vile tayari amewahi kukutenda, au umewahi kumfuma na mtu mwingine "wakidukuana", hali hiyo sio Wivu kama wengi ambavyo huita bali ni kutomuamini mwenza wako.

Pia kuna ila hali ya "umilikishi" kwamba kwa vile tu ni mpenzi wako basi hutaki awe karibu na mtu yeyote....yaani ni marufuku hata kwenda kwao, shughuli zote za kutoka unazifanya wewe kwa vile unahofia watu wengine watamuona na kumtamani....wengi huita wivu, lakini kiukweli sio wivu ni kuwa "obsessed".

Kila la kheri.

*Samahani L inagoma-goma kwani mwanangu kaing'oa hivyo nahitaji kubonyeza kwa nguvu na mie nasahau kutokana na mwendo wa haraka wa kuchapa.....

20 comments:

abyss said...

It's quite clear for those ambao wako kwenye mahusiano..Inakuwa jambo baya mno kuput neno 'uaminifu' sehemu nyeti kama hii..
Maana yangu ni hii..
-Kuwa ni GF/BF or wife/hb pasipo walau kuonyeshana a piece of wivu is direct show that 'there is no true love in somehow' becouse inamaanisha kwamba no one anayemjali mwenzake or kuumia kumwona mpenzi wake kuwa na 'kirambas' mwingine..
Dada Dinah kiukweli kabisa 'bibie wangu' akipea mkono na jidume lolote na wasipoachia mikono kwa muda kidogo,huwa ninachafukwa vibaya...Ni sawa ninamwamini but kuwa na doubt mara nyingi muhimu kwa maana wapo wanaoweza kushawishika..
'regards to all'

Anonymous said...

Dada Dina, nakubaliana na wewe kabisa, wivu ni mojawapo ya ishara za upendo.....ila siku hizi, ulaghai na kutokujiamini vinafanya watu wasionyeshe wivu kwa wenza wao ili wasionekane insecure....mimi nafurahi pale partner wangu anapoonyesha hisia za wivu over me, na mie nikiwa na hisia hizo huwa sichelewi kuzionyesha.....

Pia kama mtu upo katika mahusiano, ni vizuri kuhakikisha kuwa ukaribu wako na marafiki zako wa jinsia nyingine unapungua kupita ukaribu wako na mweza wako, kuna mipaka ambayo rafiki anatakiwa aiheshimu katika mahusiano yako...kupiga simu usiku wa manane kutuma sms zenye sexual content si uungwana!!!!

Amos Bwire said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

Wivu mwingine ni wa kitoto sana haufai kuuiga.

Wivu uwe wa maendeleo lakini isiwe kila unapomuona mume/mkeo anaongea na mtu fulani basi kiroho juujuu na maswali juu yake kibao.Please bear in your mind that "Humans beings are social beings. Unapokosa imani na mpenzio.mume/mkeo ni dalili za kwamba una kasoro fulani hivi.Kuna rafiki yangu anaulizwa na mkeo kila saa anapigiwa simu uko wapi, ukona nani?unafanya nini na mambo kibao kiasi cha kuleta kero. Juzi aliamua kumwambia ikiwezekana awe anafuatana naye kila aendako.

Naamini kama kweli kuna upendo wa kweli kati ya watu wawili basi wivu wa maendeleo utakuwepo ule ambao unakaa na mpenzio.mumeo.mkeo mnaona mambo ya watu mema na yenye tija katika mahusiano ambayo mnaweza kuyafanya pia mkijiweza.lakini ya kuulizana ulikuwa unaongea na nani sijui ulimpa nani ride nk ni upuuzi tu.

Namshukuru mke wangu hana mambo ya kijinga hayo.Na siku moja aliniambia kuwa wewe ni mtu wa watu wengi, nami nimekukuta ukiwa ulikuwa na watu wengi uliosoma nao mashuleni, vyuoni, nk,hivyo sina muda wa kuchunguza nani na nani unawasiliana nao kwani umuhimu wangu ni kuangalia mambo yetu tunayoweza kuyapanga pamoja kwa ajili ya afya ya ndoa yetu na maendeleo yetu ya kimaisha.Na aksema sitaki kujianzishia magonjwa yasiyo na sababu bure.

Hajawahi kugusa simu yangu wala nini, hata nikiiacha siku nzima hapo chumbani itaita hatapokea.Kinachompa ujasiri huo ni vile anavyoniamini na kunipenda na anavyojilinda kwa nafsi yake pia.Kwa kweli namheshimu sana kwa hayo na niko muwazi kwake kwa jambo lolote.

Nina picha nyingi za marafiki zangu toka huko nyuma waume na wanawake wengi wao aliisha wajua na hana taabu nao hata nikiongea nao.Imesaidia sana kumjali na kumheshimu sana kupita kiasi.

Si rahisi kumzuia ndege kupita juu ya kichwa chako, lakini ni rahisi kumzuia ndege asijenge kiota juu ya kichwa chako.

Anonymous said...

Kaka Amos, kama mwanamke, nahisi mke wako alipatwa na wivu kwa sababu haukumuuliza....

Anonymous said...

Dina naomba siku moja moja huwa unatuwekea familia yako bwana kila siku maandishi tuu.

Anonymous said...

sio kweli mdau hapo juu sio lazima mtu anapokuonesha wivu ndo et ana true love.no nakataa kabisa.mtu anaweza kukuonesha wivu kumbe wala hana mapenzi ya kweli anakuzuga tuu wala usidanganyike mwanamke mwenzangu niulize mimi yaliyonikuta mama yangu.mtu anayeitwa mwanaume sio mtu kabisa sio wa kuwaamini.

Anonymous said...

dada dinah me naomba unipe mbinu ya kumfanya bf wangu awe na wivu juu yangu na aweze ku express huo wivu wake kama ulivyosema kuwa bibi yako alisema suala ya wivu lilikuwa likifundwa unyagoni..mimi nina mwanaume wangu ambaye tuna miaka miwili sasa kwenye mahusiano yetu ila hakika nakuambia ni mara mbili tu ashawahi kunionesha kuwa ana wivu na mimi..ingawaje kiukweli ni miongoni mwa wale wanaume ambao kuexpress feelings zao kwa kuongea ni wazito kidogo! sasa cjui ni hilo tuuu au kuna lingine...mimi niko tayari kujifunza hiiizoo mbinu za bibi yako nijaribu nione kama labda atabadilika...

Anonymous said...

dada dinah me naomba unipe mbinu ya kumfanya bf wangu awe na wivu juu yangu na aweze ku express huo wivu wake kama ulivyosema kuwa bibi yako alisema suala ya wivu lilikuwa likifundwa unyagoni..mimi nina mwanaume wangu ambaye tuna miaka miwili sasa kwenye mahusiano yetu ila hakika nakuambia ni mara mbili tu ashawahi kunionesha kuwa ana wivu na mimi..ingawaje kiukweli ni miongoni mwa wale wanaume ambao kuexpress feelings zao kwa kuongea ni wazito kidogo! sasa cjui ni hilo tuuu au kuna lingine...mimi niko tayari kujifunza hiiizoo mbinu za bibi yako nijaribu nione kama labda atabadilika...

jolie said...

Mada nzuri sana.. Binafsi asiye na wivu kwa mpenzie basi Malaya ! Wivu turn me on kusema ukweli,nchi yangu imetawaliwa na wafaransa, tuna mtindo wakusalimiana kwa huge na kisses za mashavu. Mpenzi wangu ni WA Tz akiiona nawasalimia watu kwa njia hiyo utaskia .. Kwani lazima umuhuge tyt hivyo ? Ananinunia..hahaha, basi ananiturn on namuomba msamaha after that Nampa kitu roho ya penda.. Jamani wivu unaraha yake! Ndio nimesema asiye na wivu kwa ampendaye basi Malaya for sure.

jolie said...

Mada nzuri sana.. Binafsi asiye na wivu kwa mpenzie basi Malaya ! Wivu turn me on kusema ukweli,nchi yangu imetawaliwa na wafaransa, tuna mtindo wakusalimiana kwa huge na kisses za mashavu. Mpenzi wangu ni WA Tz akiiona nawasalimia watu kwa njia hiyo utaskia .. Kwani lazima umuhuge tyt hivyo ? Ananinunia..hahaha, basi ananiturn on namuomba msamaha after that Nampa kitu roho ya penda.. Jamani wivu unaraha yake! Ndio nimesema asiye na wivu kwa ampendaye basi Malaya for sure.

Hemedi said...

Dina, wivu ni hisia ya kawaida kwa binaadamu (na hata baadhi ya wanyama). Katika mahusiano na mtu ambaye mnapendana naye kwa dhati lazima lazima kutakuwa na kiwango fulani cha wivu. Hata hivyo tatizo linaanza pale ambapo wivu unakosa mantiki kabisa ("irrational") na kumtawala mtu katika kila hali ("obsession"). Kwa mfano, jamaa yangu alimuona gf wake ametoka nje na kurudi ndani baada ya dakika moja, akafoka "umetoka kutazama nini?" Gf: "Nilikuwa natema mate". Jamaa: "Hebu nionyeshe hayo mate uliyotema". Bahati nzuri mate yalikuwa hayajakauka. Mimi nilikuwa na gf ambaye alikuwa ana wivu mpaka akawa anakera. Siku moja nimechelewa kutoka kazini, nilipoingia akawa amenuna. Nilpotaka tu kuingia bafu akacharuka: "ngoja niinuse chupi yako! kazi gani hiyo mpaka saa 3 usiku". Kwa kuwa nilikuwa nimechoka nikamruhusu ainuse chupi yangu. Sikukaa naye sana kwa kuwa, kama wanavyosema wanasaikolojia "obsessive jealuosy is a sign of insecurity". Au unakuta watu wengine hawataki kabisa mume/mke awatazame watu wengine (whatever happened to the saying "Macho hayana pazia?"). Kwa kifupi, "a healthy dose of jealousy can be good for a relationship" lakini wivu ukivuka mpaka na ukiwa hauna mantiki basi unaweza kuleta maafa katika uhusiano.

Anonymous said...

Mi naona swala la wivu kwa mtu unaempenda ni la muhimu sana, neno kumpenda mtu kutoka moyoni si mchezo jamani.

Anonymous said...

dina swala la wivu kiukweli nimuhimu tena sana tuu haswa kwa maisha yakileo.Isipokua usizidi.kwa mm mwenzenu ninawivu kwa ma huby kanakwamba huwa naona kama nazidisha!!nisaidieni kwa hili kwan imekua ikileta shida sana haswa pale unapohoji kitu ama kutaka weka wazo kwamba hilituliangalie kwan laweza athiri uhusiano wetu,mwenzangu nikununa nakupanic!!nisaidieni jamani kwan inaumiza akili kana kwamba kila ninacho hoji inakua kero kwa ma huby!!maoni yenu katika namna yakucontrol wivu!!

Anonymous said...

dina swala la wivu kiukweli nimuhimu tena sana tuu haswa kwa maisha yakileo.Isipokua usizidi.kwa mm mwenzenu ninawivu kwa ma huby kanakwamba huwa naona kama nazidisha!!nisaidieni kwa hili kwan imekua ikileta shida sana haswa pale unapohoji kitu ama kutaka weka wazo kwamba hilituliangalie kwan laweza athiri uhusiano wetu,mwenzangu nikununa nakupanic!!nisaidieni jamani kwan inaumiza akili kana kwamba kila ninacho hoji inakua kero kwa ma huby!!maoni yenu katika namna yakucontrol wivu!!

Anonymous said...

Im sooo happy u r back Dinah.umesaidia sana kudumisha ndoa yangu hadi hiii leo tuko pamoja<Mungu akupe maisha marefu I luv U .

Anonymous said...

Dinah naomba nisaidie natafuta mama mtu mzima mwenye busara na hekima(kungwi)anifundishe kukata kiuno vizuri zaidi na kwa ustadi.kwani mume wangu anapenda sana akikatikiwa kiuno wakati wa kungonoka,shukrani na kazi njema.

Anonymous said...

...kuna watu hawajui kubembeleza means hawaoneshi wivu sana lakini doesnt mean hawana true love..pia kuna watu wanaonesha wivu sana na bado wanacheat ni dizain ya watu wasiolizika na kutosheka..unakuta mwanamke anawivu sana na mumewe lakini anatombwa nje na yeye..upuuziii!
..pia kuna watu sio kwamba wana wivu ila ni kwamba hawajiamini na wanahisi penzi lao lipo cuz wamelazimishia hao unaweza dhani wana wivu na wanakupenda kumbe walaaa...wanaangalia life security tu na sio love..

so mtu kuwa na wivu na wewe muangalie kwa jicho la tatu haimaaniishi anakupenda sana na anatrue love au hacheat ..anaweza kuwa na wivu wa kuzuga tu ili kuwa na wewe for his/her own reasons..hasa wanawake wanazo sana hizi...


Gluv
gluv100@yahoo.com

6pistolz said...

thumbs up dinah....
,,,wivu wa wastani hudumisha mapenzi,,,
,,,i like it

Anonymous said...

UMeongea vzr sana kaka,,big up kwako