Wednesday, 4 January 2012

Siri ya Mafanikio kwenye uhusiano wako.

Sio pesa....Lol!!

Hakuna mtu asiependa kuwa na uhusiano wa kimapenzi mzuri na wenye afya, mimi binafsi napenda sana kuona watu wanapendana, huwa napata maumivu na wakati mwingine hasira ninaposikia au kupata kesi ya uhusiano au ndoa kuvunjika.


Wakati wa kufundwa mara zote niliambiwa kuwa ukizubaa mapenzi kati yako na mumeo hayatokuwa kama mtakavyoanza hivyo basi unahitaji kuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna kuzoeana bali kujuana.


Sasa kwa vile Mfundaji mwenyewe alikuwa ni Hayati Bibi yangu aliezaliwa na kukua enzi za Mfumo Dume aliwakilisha somo kwangu kwa kusema “hakikisha unakuwa mstari wa mbele” lakini kutokana na maisha yalivyo sasa mimi nitasema kwako HAKIKISHENI (wake kwa waume) kuwa hamzoeani na badala yake mnajuana kiundani zaidi.


Uhusiano huwa mtamu kweli kweli unapoanza, hakuna hata mmoja kati yenu anaekumbushwa na mwenzie kufanya mambo/jambo, unajikuta tu unafanya mambo mazuri-mazuri kwa mpenzi wako, uhusiano unaendelea mnafikia mahali mnakubaliana kuishi pamoja part time(mf: mwisho wa wiki tu) au full time kwavile inakuwa ngumu sana kupitisha siku nzima bila kumuona Asali wa Moyo na baadae
ndoa.


Baada ya kuishi pamoja au kufunga ndoa mmoja wenu au wote mnaanza kupunguza speed na hatimae inafikia mahali wote kwa pamoja mnajikuta mnadharau kufanya mambo mliokuwa mkifanyiana awali kwa sababu ya mapenzi......hatua hii ni mbaya sana na ndio huwa chanzo cha ugomvi au kutafuta mtu atakaekufanyia mambo bila kumkumbusha, hatua hii inaitwa KUZOEANA.


Baada ya kuzoeana na ku-miss hamasa, chachu ya mapenzi kutoka kwa mwenza wako, unaanza kulinganisha uhusiano wako na uhusiano wa watu wengine na kuanza kuona wivu na hata ku-wish kuwa mkeo au mumeo angekuwa kama yule au
tungekuwa kama wale n.k.


Sasa nini siri ya mafanikio kwenye uhusiano?


1-Usijisahau na hakikisha unarudisha uliyokuwa ukimfanyia mwenza wako miaka 4 iliyopita, kabla hamjafunga ndoa, yafanye tena sasa. Inawezekana
maisha yenu yamebadilika na sasa mmekuwa familia kwamba kuna watoto,
bado watoto hawakuzuii wewe mume/mke/mpenzi kuwa wapenzi. Ndio ni
baba na mama lakini pia ni Wapenzi.


2-Jipende ili uvutie, usipojipenda wewe mwenyewe na kuvutia itakuwa ngumu kwa
mwenzio kuvutiwa nawe. Kwavile tu mmefunga ndoa au mnaishi pamoja
haina maana ndio mwisho wa kuvutia.
3-Penda/pendezwa,
kukubaliana au kubali mchango wa mawazo yake kwenye jambo mnalotaka
kufanya, mshirikishe mwenza wako kabla ya kufanya uamuzi wowote,
peaneni matumaini na ushirikiano inapobidi....sio kila wakati wewe
ndio msemaji mkuu na muamuzi wa mwisho na yeye ni wa kupokea tu, hata
akichangia mawazo yake huyafanyii kazi(unadharau).


4-Muda, kazi na watoto huchukua muda mwingi na hivyo kutopata muda wa
kuzungumza na kuonyeshana mapenzi, hivyo kutenga muda wenu kama
wapenzi ni muhimu. Ninaposema muda wenu kama wapenzi sina maana ya
kufanya ngono kwani ngono inaweza kufanyika watoto wakiwa wamelala,
nazungumzia ule muda wa ninyi wawili kama ilivyokuwa mf: miaka 4
iliyopita kabala hamjafunga ndoa.


5-Mawasiliano kwa maana ya kuzungumza ni njia pekee ya kumwambia mwenza wako vile unavyojisikia, unataka nini, kwanini umefanya jambo fulani, usaidiwe
vipi, kwanini uko hivyo ulivyo n.k. Hii ni njia pekee ya kuwekana sawa na kuepuka maumivu ya kihisia ambayo yanaweza kukupa upweke ndani ya uhusiano/ndoa.

6-Kubali mabadiliko,
jinsi miaka inavyozidi kusonga ndivyo ambavyo tunabadilika/tunakua,
maisha yetu yanabadilika....japokuwa wakati mwingine mabadiliko hayo
hayaji kama tulivyotarajia bado hatuna budi kuyakubali na kwa pamoja
ku-adopt badala ya kulalamika na kufananisha.

*Mabadiliko yanaweza kuwa upungufu wa hamu ya kungonoka, kupendana zaidi, kuwa wazazi, kuishi maisha ya chini au ya juu kuiko ilivyokuwa hapo awai,
kuugua, ulemavu n.k


7-Kuzozana/gombana kwa maneno, kubishana sio ukorofi inategemea mnabishanaje na kuhusu nini? Katika hali halisi kubishana kwenye uhusiano kunahashiria afya ya uhusiano wenu....ikiwa kuna watu wanaishi pamoja kama wapenzi na hawajawahi kubishana basi ni either wanadanganya au mmoja wao anamuogopa mwenzie.


Pamoja na kuwa ninyi ni wapenzi bado mnatofautiana kijinsia, kimawazo,
kikazi, kipato, matumzi binafsi ya pesa, kimalezi na hata kasoro zenu
hazifanani....hivyo kubishana ni lazima ikiwa kunatofauti hizo na
nyingine ambazo unazijua.


Kubishana kunaweza kuwasaidia mmoja wenu kujirekebisha kwani itawawezesha
kutambua kosa lako ni lipi hasa kama mwenza wako sio mtu wa kukosoa
papo kwa hapo (kosa linapotokea), pia itakuwa nafasi nzuri ya kutambua au kugundua nini hasa mwenzako anafikiria kuhusu kosa/tendo ulilofanya au tabia yako na nini anataka kifanyike ili kuepuka mabishano ya mara kwa mara.


8-Shukuru, omba radhi ni maneno mafupi na pengine unaweza kudhani kuwa hayana umuhimu wowote, licha ya kwamba yanaashiria kuwa umelelewa katika maadili mema pia yanauzito na maana kubwa sana kwenye maisha yetu kuliko unavyofikiria.


Unapohisi kuwa umemuudhi mwenza wako, sio mpaka akununie kwa wiki moja au
akufokee ndio uombe radhi, akionyesha tu kuwa hajafurahia tendo lako
au maneno yako basi omba radhi.


Shukuru kwa kila jambo unalofanyiwa na mpenzi wako....unakumbuka wakati
mnaanza uhusiano akiku-check during the day unasema “asante mpenzi
kwa kunijulia hali”, sasa kwanini ushindwe kusema asante kwa chakula mpenzi?!!

Kila la kheri!

19 comments:

Anonymous said...

OWKEY DADA DINA BUT ME NAONA KAMA INAWEZEKANA KUNGEKUA NA LIKIZO KTK MAPENZI YANI KIPINDI FULANI MMOJA ANATOKA NYUMBANI THEN ANAENDA KWAO AU KOKOTE ILI KUMFANYA MMOJA AMMISI MWENZIE ME NAONA ITAONGEZA HAMU YA KUMPENDA MWENZIO

docha said...

Jamani Dinah,
Welcome back. Happy New Year. Tulikumiss sana sana na naona umeanza mwaka na siri ya mafanikio kwenye uhusiano. Hii ni nzuri sana na inatupa raha wadau wako. Mungu akubariki sana

ALFRED MWAKAPESA said...

Thank u Dinnah,
Ukweli uliyosema theoretically ni rahisi ngumu kuimplemnt kutokana ubinadamu unautufanya "hili nana aanze na kukubali kuwa chini au hali ya umeshindwa"Taasisi hii ni ngumu tumuachie mwenyewe MUUMBA

Anonymous said...

Asante Dinah,
Ugumu WA YOTE UNATOKANA NA UKWELI WE ARE LIVING ARTIFICIAL LIFE. ZAMANI HAKUKUWA NA TOFAUTI YA MAISHA BAINA YA FAMILIA AU KIJIJI NA UNAPOOA NYOTE MKO LEVEL MOJA NA MLINGANO WA MALEZI. LEO SI RAHISI BINTI ALIYEKULIA KWA WAZAZI WAKE NA MAISHA YAO AJE KWAKO ULIYELELEWA KIVYENU MKAMATCH.USHINDANI NI LAZIMA UJITOKEZE NA ASIPOKUWEPO WA KUSUCCUMB IMETOKA HIYO!!!!

Anonymous said...

wooo Dina karibu tena tulikumiss sana wadau. mada nzuri sana.please please tupe vitu maana wewe unamchango mkubwa sana katika mahusiano yetu ya kingono.

Anonymous said...

Mi naona ngono ya mara kwa mara ie daily ndio chanzo cha kuchokana na kuanza kuona mwenzako kama hana jipya au utamu wake umeisha hivi. Sex two days per week i hpe is enough to keep a relatnshp strong. Naona wapenzi wawe wanafurahia zaid ukaribu wao baadala ya kufurahia ngono tu!, mapenzi ya kufurahia ukaribu yanapendeza coz yanajenge mioyo iwe inawamis wenzetu hata mkitengana kwa saa moja tu. In short ngono ya mara kwa mara au kila cku ndio inayoua hisia za mapenzi na baadalayake inajenga mazoea kwa wanandoa. Ni maoni yangu. Its me Nazmuls

Anonymous said...

ZA MWAKA MPYA?SAMAHANI KWA KUTOKA NJE YA MADA HAPO JUU, MI NINA TATIZO KWENYE UKE PEMBENI KUNA VIPELE VIDOGO VIDOGO, NILIENDA HOSPITALI WAKANIPA DAWA IMEANDIKWA (CAUSTIC PENCIL AU SILVER NITRATE) YA KUPAKA.WAKANIAMBIA UGONJWA UNAITWA (WARTS), NIMEPAKA DAWA,VILE VIDOGO VIMEISHA ILA BADO VIKUBWA VINAZIDI KUKUWA, NAOMBA MSAADA WENU MANA VINANIHARIBIA MAENEO ILA HAVIUMI KABISA.NIMEJITAHIDI KUWAULIZA WATU TOFAUTI WANANIAMBIA NIENDE KWA WAGANGA WATANIKWANGUA NA KUPAKA DAWA

Anonymous said...

thanks kwa shule nzuri!!

watu wanajisahau sana...mwisho wa siku mtu anacheat


gluv

Dinah said...

Kaka Mwakapesa sio ngumu sema watu tunapenda kujiendekeza. Maisha yanabadilika bila sisi kutaka na ndio maana kwa sisi Wakristo tunapofunga ndoa huwa tunaapa kuendelea kuwa na wenza wetu kwa shida na raha....hii inamaanisha kukubali mabadiliko.

Umempenda mtu na mkakubaliana kuishi pamoja wote mkiwa wazima (bila kilema) na maisha mazuri.....Mara mwenza wako anapata ajali na kupata ulemavu....penzi ako itaisha na utamterekeza au utakubali mabadiliko na kuendelea kuishi nae?

Au ikitokea wote mmepoteza kazi au bishara hazijaenda vema na hakuna pesa, je mtaachana au mtakubali mabadiliko na kuendelea kuwa pamoja na kujitahidi kuinuka tena kama wapenzi?

Mimi kama Dinah na Mume wangu tumepitia mambo mengi magumu, tulikubali mabadiliko na kuendelea kuwa pamoja mpaka tulipoweka mambo safi na sasa tuko sawia kabisa.

Nilichokisema ni kutokana na uzoefu, hivyo sio ngumu kama unavyofikiria.

Dinah said...

Anonny wa 6:35:00 PM Heri ya mwaka mpya kwako pia mdada.

Ikiwa hiyo dawa imetibu na hatimae kuondoa vipele vidogo ni wazi kuwa ndio dawa unayotakiwa kuendelea kuitumia mpaka hivyo vikubwa viondoke pia.

Inawezekana vimechelewa kutondoka kutokana na ukubwa wake nje na ndani, ni vema kurudi tena kwa Daktari ili umueleze matokea ya Tiba uliyotumia na yeye atakushauri kama unahitaji kuendelea kutumia (pewa nyingine) au la.

Uvumilivu ni muhimu ili upone kabisa. Kila la kheri.

Dinah said...

Asanteni wote, Heri ya mwaka mpya kwenu pia. Nafurahi kuwa nanyi.

Dinah said...

Anony wa 4:41:00 PM hakika ngono mara 2 kwa wiki hiyo ipo kwenye kundi la mara kwa mara.

Kufanya ngono mara kwa mara hakukufanyi umchoke mwenzio unless other wise hakuna mapenzi ya dhati kati yenu na pia sio wabunifu/watundu.

Kuna namna nyingi sana za kungonoka hata kama mnangonoka kila usiku kwa mwaka mmoja bado hamuwezi kurudia yale yale, hivyo suala la kuchokana nadhani ni la individual.

Kama umejaaliwa uwezo wa kawaida au ule wa hali ya juu wa kungonoka huwezi kufanya ngono mara 2 kwa wiki(HAITOSHI)....Lol!

Asante kwa ushirikiano.

Dinah said...

Anony wa 1:20:00 hilo la likizo mbona lipo tangu enzi ila tofauti ni kuwa enzi hizo haikuwa ili mpenzi aku-miss bali ulienda kukumbushwa wajibu wako kama mwanamke, unakwenda nyumbani kwa Bibi au Shangazi mara 2 kwa mwaka.

Suala la kukumbukana kwenye uhisano linategemeana na mtindo wa maisha mlionao, uzito wa mapenzi yenu na mahitaji yenu ya kimwili na kihisia.

Mf: kama mna watoto na wote mnafanya kazi sidhani kama mtahitaji muda wa ku-miss-iana kwani huo muda wa kuwa pamoja tu hamna kwani wote mko busy, ninaposema kuwa pamoja sio kuishi nyumba moja bali kutumia muda mmoja kama wapenzi.

Pia ikiwa mnafanya kazi za shifts mmoja anafanyakazi usiku na mwingine asubuhi lazima mta-miss-iana tu.

Kuna watu wanaishi pamoja lakini wakiachana ile asubuhi kwenda kazini huwa wanakumbuka sana kama vile hawajaonana wiki nzima.

Asante kwa ushirikiano.

Anonymous said...

Asante sana dada kwa kutupa elimu, pia pole kwa hi kazi,mm ni mfuatiliaji wako ila kuna jambo naomba kuuliza, mimi ni mwanaume mwenye miaka 18, uume wangu una urefu wa inch 5 na mzunguko nch 4.1 ,je kwa hu umri wangu uume hu unaendelea kukua au ndo mwisho?, na je kuna umri mtu akifikia uume hauendelei kukua?
DAVID, arusha.

Anonymous said...

Anon wa 6:35 PM, Pole sana. Nakushauri uende kwa daktari bingwa wa ngozi. Pili, hebu fanya full blood picture ambayo itakupa picha kamili ya tatizo lako kwa kuwa wakati mwingine tatizo linaweza kuwa ndani ya system yako ya damu na si kwenye ngozi tu.

Anonymous said...

Anon wa 6:35 PM, Pole sana. Nakushauri uende kwa daktari bingwa wa ngozi. Pili, hebu fanya full blood picture ambayo itakupa picha kamili ya tatizo lako kwa kuwa wakati mwingine tatizo linaweza kuwa ndani ya system yako ya damu na si kwenye ngozi tu.

Anonymous said...

Anon wa 6:35 PM, Pole sana. Nakushauri uende kwa daktari bingwa wa ngozi. Pili, hebu fanya full blood picture ambayo itakupa picha kamili ya tatizo lako kwa kuwa wakati mwingine tatizo linaweza kuwa ndani ya system yako ya damu na si kwenye ngozi tu.

Anonymous said...

Mambo mengi Dinah umeyaongea kwa uzuri na ufundi mkubwa, Bt KIUKWELI HIYO NI THEORY ZAIDI, PRACTICALLY HAYO ULIYOYASEMA HAYATEKELEZEKI KIRAHISI RAHISI KAMA YANAVOTAMKWA AU KUANDIKWA, kwa kifupi, the are 'not sustainable', mwisho wa yote hayawezi kuendelea, mbinu zote utazofanya, ipo siku lazima yatakuwa Marudio! Mfano, nlizungumzia hapo, kufanya ngono kila siku sio vzuri coz it reduce intimacy huko mbeleni. Sikuwa na maana ya juujuu tu bali kuna alot of physiological changes that may ruin a man's healh, inaweza sababisha seminal leakege, weak erection, decrease in orgasm sensation in males, inability to achieve orgasm, PE and in extreme cases it may result into ED, thin semen, fatigue, testicular pain and memory loss, Hot flashes, mood swing, blurred vision, hair loss and numbness and alot of inflamations in the body eg kwenye vipele vya ndevu, groin areas, matakoni na makwapani. Jaman, fanyeni ngono kwa afya, ukifanya leo kesho pumzika. Kwa wiki fanya siku tatu na ktk cku yasizidi mabao matatu, haijalishi una mhemko kiasi gani just use ur mental wil to control ur sexual urge. Híi ina faida kwa wanaume, they wil live a happy and strong sexlife mpaka miaka 70 na kinyume chake ni hasara. Effects za kufanya ngono kila cku huwezi kuziona leo hiihii, inachukua mpaka miaka mitano hadi 8 kuanza kujitokeza, hapo ndipo wanaume wanaanza kupata tabu kutafuta viagra ili kutibu weak erections and PE, na kutwa kusearch madawa ya nguvu za kiume bila kujuwa chanzo, jaman! Source is Overejaculation!. Keep in mind sex is healthy bt evrythng too much is harmful,like wise eating food is a natural and healthy thng bt too much/overfeeding is harmful!. Kufanya ngono kila cku hyo ni sexual addiction na itakuletea madhara ya weak erection, ED, low libido, los of apetite, loss of erection in the midle of sexual activity, yani kwa kifupi wanaume kuweni makini, msipokuwa makini mtapoteza ngovu zenu za kungonoka mkiwa na miaka 45(ie mtaanza kuexperience menopause symptoms, inaitwa male menopause) tu halafu masharobaro watawatombea wake zenu. Somo la leo hilo, Dinah kama hujui mambo haya, naomba upunguze spidi ya ngono for better sexlife in the coming days hasa kwa mumeo na wewe pia. Its me Nazmuls

Anonymous said...

dada ulouliza suali 6:35.. kuna uwezekano mkubwa ukawa umepata maradhi ya zinaa, rudi tena hospital wakufanyie test zaidi utakapoweza kujua ni vidudu gani vimekuathiri utapata matibabu ya uhakika zaidi,, virus wanaofanya warts sana ni HPV(human papilloma virus)