Sunday, 31 July 2011

Niliolewa nikiwa nampenda wa zamani, nimuepuke vipi?

"Hi Dinah na wachangiaji wengine,
Kwa kweli napata tabu hebu nisaidie kwa hili; Mpenzi niliekuwa nae zamani nilimpenda sana lakini kwa bahati mbaya tukakosana. Sasa nimeolewa as you know ndoa hupangwa na Mungu lakini bado nampenda na huku nina mume what should I do kuepukana nae huyo wa zamani"?

Wednesday, 27 July 2011

Mpenzi hanijali, hanithamini tena,nifanyeje?

"Dada Dinah pole na kazi za kutueimisha sisi tulio katika ulimwengu huu wenye raha na karaha zake. Mimi ninaishi na mwanaume ambaye hatujafunga ndoa ila tumezaa mtoto mmoja na ilibidi tuanze kuishi pamoja kabla ya ndoa kwa sababu ya kusaidiana malezi ya mtoto.

Kikubwa kinachonikera kwake ni kwamba hanijali tena, hanithamini wala haoni na mimi ni sehemu ya maisha yake,nasema hivyo kwa sababu kila ninapohitaji msaada wowote toka kwake hanisaidii kabisa.

Ukija katika suala la kugonoka jamani mimi mwenzenu naweza kaa hata mwezi mzima hajanigusa wala nini na tunalala kitanda kimoja kila siku na hata tuki sex yeye anafanya mradi yafike basi na si kutombana ili kila mmoja wetu aridhike nakumfurahia mwenzie.

Kingine, anachelewa kurudi nyumbani yeye ni mfabiashara k/koo na duka anafunga saa kumi na moja kamili ila mpaka afike nyumbani ni saa 3-4 au hata saa 5 usiku nimeshaongea naye lakini wala hanielewi kabisa.

Jamani naomba ushauri wako dada na wachangiaji wengine kwani nahisi kutokumpenda tena, mwenzenu nifanyeje ili tuwe na mapenzi kama walivyo wengine? Poleni kwa msg ndefu".

Tuesday, 19 July 2011

Miaka 10 kwenye uhusiano na mtoto moja bila ndoa, je nimuache?

"Habari dada Dinah,
Pole kwa majukumu na hongera kwa kuelimisha jamii. Mimi ni mdada nina miaka 32 toka Arusha. Nina uhusiano na mwanaume kwa muda wa miaka 10 na nimezaa naye mtoto mmoja.

Kabla ya kuwa na mimi huyu mwanaume alishawahi kuwa na wanawake tofauti na amezaa watoto wawili kila mmoja na mama yake.Katika uhusiano wetu tumefanikiwa kununua nyumba moja yeye alichangia hela nyingi kuliko mimi ila mimi niliifanyia ukarabati mkubwa, hati nilisaini mimi na alinikabidhi.

Nyumba hiyo ninaishi mimi na mtoto wangu, yeye anaishi nyumba nyingine na watoto wake hao wawili na huwa nafika hapo ila hajawahi kunikaribisha ndani wala kunitambulisha kwa watoto wake.

Alishawahi kunitambulisha kwa baadhi ya ndugu na rafiki zake na kwa staff wenzie ofisini. Huyu mwanaume amekuwa msaada sana kwangu na familia yangu, kwetu wanamfahamu kama baba wa mtoto wangu.

Mimi nataka kuachana na huyu mwanaume kwa sababu naona ananipotezea muda pamoja na kwamba ananisaidia. Ila kuna ndugu zangu wananishauri nisimuache. Mimi binafsi naona hayupo serious kwani angekuwa serious na mimi au kuwa na mpango na mimi sidhani kama angekaa nyumba tofauti na mimi.

Pili, muda wa miaka kumi ni mrefu sana kama angekuwa na mpango na mimi nadhani angenioa. Nimejaribu kuongea naye mara nyingi takribani miaka 6 sasa kuhusu suala la ndoa lakini kila siku jibu lake kuwa ana mipango anaikamilisha kwanza lakini haniweki wazi ni mipango gani hiyo.

Tatu, Pamoja na kwamba huwa anakuja kwangu na tunafanya mapenzi lakini si kivile na mara nyingi huwa nakuwa mpweke, kwa kifupi huwa anakuja anavyotaka yeye so nakuwa sipo uhuru na mapenzi.

Nne hakuna relation yeyote kati ya mtoto wangu na watoto wake yaani kwa kifupi mambo yake mengi haniweki wazi hizo ndio sababu ambazo zinanifanya niamue kuachana naye pamoja na kwamba ananihudumia kwa kila kitu.

Binafsi bado nampenda sana, tena kwa dhati ila kwa kweli nimechemsha kwa hilo. Nilishawahi kumwambia kuwa nimechoka na ninataka tuachane, aliumwa presha mpaka akalazwa. Toka nimekuwa na uhusiano naye sijawahi kuwa na mwanaume mwingine nje ya uhusiano wetu na nilishawakataa wengi kwa ajili yake lakini kwa sasa nimechoka.

Hofu yangu ni kuwa baada ya kuachana itabidi tuuze hiyo nyumba na nitahangaika na makazi mimi na mwanangu. Pia nahofia usalama wake maana bado atabaki kuwa baba wa mtoto wangu.

Ninaomba wana-blog wenzangu mnishauri katika hili ili niweze kuchukua maamuzi sahihi. Samahanini sana kwa maelezo yangu marefu, Madada wa Arusha".

Monday, 4 July 2011

Wazazi na jamaa wanasema nitafute msomi kama mimi, does it matter?

"Pole na kazi dada Dinah, kwanza nitangulize shukrani zangu kwa watu wote wanao toa ushauri na kutuelimisha mambo mbali mbali katika hii blog. Mimi ni mwanamke mwenye umri miaka 25, nimekuwa na boyfriend wangu kwa muda wa miaka 6, nilianza mahusiano nae nikiwa namalizia kidato cha nne, ila kwa sasa nipo chuo nachukua masters degree.

Mimi na boyfriend wangu huyu tunapendana sana, na pia namsaidia mambo mengi sana ya kifedha na hata yakimaisha (nikimaanisha ushauri), kwani kwa bahati mbaya hakufanikiwa kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia, elimu yake ni ya kidato cha nne.

Hiyo yote ni kutokana na Wazazi wake kutojishughulisha nae tokea zamani, hawakujali suala la elimu, kutokana na hili alipitia maisha magumu saana kiasi cha kumfanya aanze kufanya dili mbalimbali ili apate hela za kuendesha maisha, na pia aliweza hata kupanga chumba akawa anaishi mwenyewe na kununua assets mbalimbali za nyumba.

Kwa ujumla ni mtu ambae anajipenda na anapenda maisha mazuri tatizo ni uwezo tu na kazi ya maana ambayo itakidhi mahitaji yake yote. Pamoja na hili anasaidia hata ndugu zake pia. Hivi karibuni mambo hayamuendei vizuri kabisa japo hajakata tamaa.

Anajitahidi hivyo hivyo, kwa sababu hii mara nyingi ananiomba mimi nimsaidie kifedha kwa sababu nampenda inabidi nimsaidie nimpe hela za matumizi na muda mwingine hata za kulipia nyumba. Na fanya hivyo kwasababu nampenda, na yeye ananipenda, yupo tayari hata kesho kuishi na mimi.

Swali langu lina kuja hivi, mimi nimesoma nategemea kupata master degree yangu miezi kadhaa ijayo, kwa ujumla namshukuru Mwenyezi Mungu ninamahitaji yangu yote, ila tatizo huyu boyfriend wangu, hajasoma ila ni mtu ambaye anajitahidi hivyo hivyo sio mvivu anapenda maisha mazuri, ila watu wanasema hatutadumu kwa muda mrefu kutokana na tofauti zetu, je mnasemaje kwa hili?

Swali la pili ni hili, tumejuana kabla hata sijaanza chuo, kwa kipindi chote hicho tulikuwa pamoja mpaka sasa nategemea kumaliza masters tupo pamoja, na pia ndio boyfriend wangu wa kwanza sijawahi kuwa na mwingine, je mnanishauri vipi hapa?

Kwani baadhi ya watu wananiambia nitafute mtu aliesoma kama mimi kwani tutaelewana zaidi kimaisha. Kuhusu suala la wazazi, wazazi wake wananipenda saana, ila tatizo lina kuja upande wa wazazi wangu wanataka nitafute msomi mwenzangu, ila kwa mimi siko tayari kwani nampenda huyu nilionae.

Kwasasa haijalishi kwani nipo tayari kumsaidia kwa lolote ili tu awe na maisha mazuri. Je hii ni sahihi? Naombeni ushauri wenu, je kuna future hapa kweli au tunaforce mambo tu kwa muda kwani yatakuja nizidia huko baadae kama asipo pata kazi au biashara ya maana.

Naombeni ushauri wenu na mtazamo wenu.

Dada K".

Dinah anasema:Asante mdogo wangu, natumaini kuwa umefanyia au unaendelea kufanyiakazi maelezo mazuri kutoka kwa wachangiaji, yasome yote kisha uyachanganue alafu uchanganye ndio ufanye uamuzi.