Friday, 22 April 2011

Ni kawaida au ndio kwisha habari yangu?"Dinah na wengine naomba kuwauliza, tangu nimejifungua nahisi hewa inatoka huku mbele. Hali hii hujitokeza ikiwa sijavaa chupi au nguo, yaani nikiinama na kuinuka nasikia hewa inatoa.


Sasa sijui nikiinama hewa ndio inaingia na nikiinuka ndio inatoka, hivi ni kawaida au ndio kwisha habari yangu?"

Tuesday, 12 April 2011

Mume wangu anamwaga kiduchu je anatosheka kweli?


"Mpendwa dada Dinah,

Nimeigundua blogu yako siku za karibuni na nimevutiwa sana na ushauri unaoutoa pamoja na michango mbali mbali ya uwazi kutoka kwa wajumbe. Leo naona nami nitume swali langu kwako, ambalo linamhusu mume wangu.Mimi na mume wangu tumekuwa kwenye mahusiano miaka saba sasa (mitano baada ya ndoa) na miwili kama wapenzi tu(wachumba).Kwa kipindi chote hicho, kusema ukweli sioni tatizo lolote kimapenzi - yaani tunaridhishana.

But kuna sehemu nilisoma ndani ya blogu hii, mtu mmoja akawa anasema Shahawa zinatiririka kutoka Ukeni na akaambiwa na wachangiaji kuwa ni kawaida kama jamaa anamwaga Shahawa nyingi. Jambo hili lilinistua kidogo - kwa vile mimi na mwenzangu sijawahi kuona siku zimetoka Shahawa nyingi - hata akitumia condom, zinaishia humo humo - yaani hata ungezikomba na kijiko cha chai hazitajaa hata robo yake.

Na akiwa kwenye mzunguko wa pili ndio kabisaaaaa hakuna kinachotoka. Sasa swali ni je, hii ni kawaida au ana matatizo? Nahisi mume wangu hapati raha kama wanaume wengine (naimagine labda wingi wa Shahawa unamaanisha starehe zaidi?). Na je, mwanamke ukimwagiwa Shahawa nyingi kuna feelings zozote tofauti? labda kunyegeka zaidi, au?Hatujawahi kuzungumza na mwenzangu juu ya jambo hili - na wala halinisumbui kwa vile watoto tunao. Na mimi huyu ni mwanaume pekee niliewahi kungonoka naye, so sina uzoefu kwa hao anaomwaga spoon fulls! Jamani niambieni - kuna raha anayoikosa mume wangu kwa kuwa na Shahawa kidogo? je kama ni tatizo asaidiweje?


Wadau naombeni mawazo/ushauri. (Labda umri - nilikutana naye akiwa 28 na leo yupo 35 yrs),tuna watoto 2. Jamaa yuko busy saana, na kama miaka 2 hivi amekuwa akimeza madawa ya BP - nahisi makeke yake yakipungua - labda kwa sababu ya dawa za BP kwani ndivyo daktari alivyotuambia. Lakini hili la Shahawa kiduchu alikuwa nalo tangu tukutane! Naingojea hii corner nipate maoni na ushauri wenu. Asanteni.

Nar".

Tuesday, 5 April 2011

Mume wangu anatereza nje na "dada" zake na kuzaa ovyo, nifanye nini?


"Dada Dinah,Salaams.

Naona nianze moja kwa moja matatizo yangu. Mimi ni mwanamke umri miaka 38, nimeolewa miaka mitatu iliyopita, sina mtoto. Ninaishi na mume wangu pamoja na binti wa mume wangu ambaye anasoma boarding.


Tatizo kubwa ni kuwa nimeshindwa kumzalia mtoto mume wangu na hivyo ume wangu kazaa na housegirl wetu. Kabla hajampa ujauzito, aliomba nimfukuze akidai hana adabu. Baadaye nikaambiwa na majirani kuwa housegirl wetu ana mimba. Sikujua ni ya nani hadi hapo baadaye.


Baada ya muda nikagundua kuwa mume wangu anatembea na msichana jirani aliyekuwa akimuita dada kwa vile wanatoka sehemu moja. Dada huyo alikuwa akija kututembelea na wakati mwingine akitusaidia kazi wakati mimi nikisafiri. Kazi yangu ni ya kusafiri na baadaye nikahamishiwa Wilayani kabisa.


Kurudi kwangu nyumbani ni siku za weekend tu.Kumbe yule dada akawa anakuja kulala na mume wangu usiku. Nikaambiwa na majirani. Nilipomuuliza kama kawaida alikataa. Yule mwanamke baada ya kuona nimegundua amehama mkoa na kuhamia Dar.


Hivi karibuni nimetumiwa sms na msichana akiniambia kuwa ana mimba ya mume wangu na kuwa kaipatia nyumbani kwangu kwenye kitanda changu na kuwa eti nisubiri kuletewa watoto. Nilipofuatilia nikagundua kuwa huyo msichana ni mwanafunzi wa Sekondari na wanatokea sehemu moja pia na mume wangu.


Nilipomuuliza mume wangu alikanusha kama kawaida. Lakini baadaye nikapata taarifa kuwa mume wangu kampiga sana yule msichana hadi kulazwa Hospitali kwa kuwa eti kanitumia sms. Nilipomuuliza alikubali, halafu baadaye alikanusha akidai kuwa ingekuwa ni stori ya kweli basi angeshitakiwa police.


Kweli mambo ni mengi, mojawapo likiwa la mume wangu kutopenda kabisa mimi kugusa simu yake. Nilishakuta sms za wanawake wawili kwenye simu yake, mmoja ninayemfahamu. Hata nikiamka kujisaidia usiku, yeye anashituka akihofia simu zake zisiguswe. Mume wangu anao marafiki wengi wa kike yeye akiwaita ni dada zake na wengi wa kabila lake la Wapare, ambao wengine ndio hao anaotembea nao.


Sasa mimi sielewi hili kabila, nimegundua kuwa ni Malaya sana, hadi najuta. Mimi nafanya kazi na kipato changu ni kikubwa kuzidi cha mume wangu. Namnunulia nguo nzuri anapendeza, nimemsaidia kumjengea nyumba mama yake na sasa tunajenga ya kwetu. Nampenda sana mume wangu na yeye anadai kunipenda.


Kutokana na hali hiyo afya yangu Kisaikolojia imeharibika, naombaeni ushauri wenu. mngekuwa ni nyie mngefanya nini"?

Monday, 4 April 2011

Nikimhitaji mume wangu kimwili ananishushua, nifanyaje....


"Hallo dada Dinah pole kwa shughuli hasa hii ya kutuelimisha sie wanawake. Asante sana.

Mimi nina swali, nina mume asiyejua mapenzi japokuwa nahisi anaelewa ila ananisoma tu,hivyo najizuia sana kumfanyia na kumuonyesha mapenzi kwa sana kwani naogopa atanidhania mhuni.


Pia hapendi kufanya mapenzi mara kwa mara, ukweli ni kuwa anakaa mbali nami lakini nikimwomba niende anadai yupo busy! nina wakati mgumu sana kwa hilo,anadai nifanye kazi yaani kuchakarika na life nisiwaze hayo mambo ya mapenzi,eti ooh "huna kazi nini"?

Naomba ushauri pia ktk hili".