Thursday, 24 March 2011

Baada ya kutendwa ndoani, nachukia wanaume wote....nifanyeje?

"Pole na kazi ya kushauri,kuelimisha n.k jamii. Kwanza napenda kukupa kheri ya mwaka mpya dada DINAH. Mimi ni mwanamke wa miaka 29 ingawa mapema sana this year natimiza 30. Nilipokua na umri wa miaka 24 nilibahatika kupata mchumba na hatimaye kuolewa na kupata mtoto wa kiume, Kwa sasa nimeachika. Wakati wa Uchumba na mwanzoni mwa Ndoa Mume wangu alikua mchaMungu wa kweli kiasi kwamba tulikua tunagombana nisipo swali[ni waislam] Hali ya kimaisha niliyomkuta nayo mume wangu haikua nzuri, ikabidi Baba yangu atusaidie mimi na mume wangu. Hivyo mambo yakawa mazuri tena sana kwani tulianzisha Biashara zetu ambazo kiukweli zilitukubali. Baada ya mambo kuwa mazuri, mwenzangu akaanza kubadilika akawa mlevi,wanawake ndio usiseme! Nilipokwenda nyumbani kujifungua, huku nyuma akawa anaingiza wanawake kila siku tena kwa kuwabadilisha. Niliporudi nikapewa habari zile nikamuuliza akakataa. Basi nikaanza kuchunguza na Mungu aliniwezesha nikabaini ukweli niliyokua nikiambiwa. Kwavile nilibaini mwenyewe,nilikua na vielelezo nilipompatia alikua mpole na kukiri ni kweli akaomba msamaha nami nikamkubalia. Ila kumbe hakua ameacha tabia yake. Nikawaeleza wazazi wake wakamuita na kumsema hakusikia. Tukapelekana BAKWATA akaitwa akasemwa na wakamwambia kwavile amekua mchafu wa tabia kwanza tukapime afya lakini yeye akakataa na kusema kama ni hivyo bora anipe Talaka yangu. Mimi tangu nitoke kujifungua sikua nimeshiriki nae tendo la ndoa na hata baada ya kumsamehe pia sikutaka kushiriki nae kwani nilikua nikimwambia tukapime ndio tushiriki. Kinachonifanya niombe ushauri ni kwamba kwa sasa simuamini mwanamme yeyote naona wote ni wadanganyifu. Niliwahi kupata mwanamme ila aniponitamkia kunioa nikamchukia na kuachana nae. JE,NIFANYEJE?" Dinah anasema: Heri ya mwaka mpya kwako pia, asante sana kwa kuniandikia na kwa uvumilivu, vilevile nakupa pole kwa yote uliyokabiliana nayo katika umri mdogo. Hongera sana kwa kuwa na msimamo wa kugoma kushirikiana nae kimwili mpaka mkapime afya zetu....well technically afya yake yeye mwenye tabia chafu. Hakika, ukiumwa na Nyoka mara moja lazima utaogopa sana hata ukiguswa na jani. Unahitaji muda kuweza kumuamini mwanaume na hiyo ni hali ya kawaida kabisa, wala usihisi presha kutoka kwa Jamii inayokuzunguuka kuwa una mkosi au huwezi kuolewa tena(Hakuna kitu kibaya kama kufungandoa ili kuridhisha Ulimwengu, kumbuka walimwengu hawana wema na huwezi kufurahisha kila mtu kwenye jamii yako). Kitendo cha kuanza kutoka na wanaume wengine kinaonyesha umeanza "kupona" maumivu aliyokupa Mumeo wa ndoa, lakini linapokuja suala la kuwa na uhusiano wa kudumu unashindwa kuji-commit kitu ambacho kinaeleweka. Nini ch akufanya: Usiwe na haraka na usijali wasemayo Walimwengu kuhusu ndoa ya awali au lini utaolewa tena, nenda taratibu na tumia muda wako vema huku ukifurahia maisha kama mwanamke anaejitegemea na mwenye uzoefu (ndoa yako iliyopita ichukulie kuwa ni uzoefu unaokufanya ujue utakacho maishani mwako na sio Mkosi). Ikitokea tena umemdondokea mwanaume kimapenzi, hakikisha unakuwa muwazi kabla uhusiano haujaota mizizi. Mueleze mpenzi huyo nia yako(kwamba huna haraka sana kufunga ndoa). Unatakiwa kuwa a bit smart unapoliweka hili suala wazi kwani kamamwanaume ni mjinga-mjinga anaweza kudhani kuwa unataka akuchumbie kumbe wee huna mpango huo. Sasa unatakiwa kujiwekea malengo, mfano:- Napenda kutekeleza hili na lile kabla sijaamua kutulia na kujenga familia n.k. Natumaini maelezo ya wachangiaji na haya yangu yatakuwa yamesaidia kiasi fulani kujua nini chakufanya, ila kubwa zaidi ya yote ni kujipa muda na kufurahia maisha kama Mdada/mwanamke/single.....kumbuka umeolewa ukiwa na miaka 24, huu ndio u mri wa kufurahia "uanamke"....kwamba wewe ulitoka kuwa Binti wa moja kwa moja na kuwa mke wa na Mama wa.....hujawahi kuwa wewe bila kuwa chini ya.... Kila la kheri.

Tuesday, 22 March 2011

Haya nimerudi full time, Shukrani za dhati kwa ushirikiano na uvumilivu!

Habari za siku nyingi mpenzi msomaji, mchangiaji, mtembeleaji na wewe ulieendelea kunitumia maswali japokuwa sikuwa na muda wa kuyajibu kutokana na sababu nilizozieleza kwa kifupi (kulia hapo kwa juu).

Kwa kawaida blog hii huwa haihusishi masuala yangu binafsi isipokuwa yanayohusu maisha halisi ya kimapenzi ya mtu yeyote, lakini kutokana na nitakachogusia hapo chini, nimeshindwa kujizuia bali kukushirikisha ili utambue kuwa Blog haikunishinda bali nilikuwa nakabiliana na mabadiliko ya Kimwili, Kisaikolojia na kihisia kutoka Dinah kuwa mama kwa mara ya kwanza.

Baada ya safari ndefu ya Ujauzito na mkanganyiko wa Homono zilizonifanya nichukie mambo yote yanayohusisha Teknolojia (ndio maana sikuweza kufanya kazi yangu hapa) yote kwa yote namshukuru Mungu nimejifungua salama mtoto wa Kiume siku chache zilizopita.

Mungu awabariki na awape moyo huo huo wa ushirikiano katika kujaribu kusaidiana ili kuendesha maisha ya amani, furaha na upendo kwenye mahusiano na ndoa.

Asanteni.

Friday, 4 March 2011

Nianzie wapi Kisheria kumtaliki mume wangu?-Ushauri

"Kwanza napenda kukupongeza kwa kazi yako nzuri, pili mie nilitoa malalamiko yangu kuhusiana na mume wangu ambae hataki kunipa Talaka dada dinah, naomba unielekeze wapi naanzia kwenye vyombo vya Sheria maana issue nataka pia atoke kwangu.

Kuna baadhi ya watu wananiambia Mahakamani hawavunji Ndoa na wengine wananiambia inaweza pelekea hata Miaka miwili kila siku unapigwa Tarehe tu, sio siri dada Dinah ni kama naishi na Chui ndani ya nyumba, kwamba muda wowote anaweza akanibadilikia na kunila nyama"

Tuesday, 1 March 2011

Uhusiano una Mwaka, Ex wa Mpenzi amejifungua mtoto wake mwaka huu! Nifanyaje?

"Habari dada Dinah pole na majukumu ya kila siku,
mimi ni dada wa miaka 27 nina mchumba ana miaka 35 tumekuwa pamoja kwa muda
wa mwaka na miezi mitatu hivi. Nampenda sana mchumba wangu na yeye naamini ananipenda.

Tatizo limejitokeza hivi karibuni; ni kwamba kabla ya kuwa na mimi alikuwa na mwanamke ambaye alinishanitaarifu kuwa aliachana nae ndio maana mimi nikakubali na tukawa wapenzi. Sasa ananiambia kuwa huyo dada ana mtoto wake tena kamzaa this year, ina maana
hiyo mimba kapata wakati ndio tunaanza uhusiano wetu.

Sijasikia kwa mtu mwingine zaidi yake amesema eti nikisikia kwa watu na yeye
hajaniambia nitamuacha, amesema yeye ananipenda mimi na anataka niwe mke wake. Hapa nilipo nimechanganyikiwa mbaya zaidi badonampenda sana huyu kaka na sijui nifanyaje!

Yaani mpaka sasa sijamuelewa ananidanganya au ananipenda kiukweli, mwenyewe ananiomba msamaha sana kuhusiana na tukio la kuzaa na ex wake.

NAOMBA USHAURI WENU, nifanye nini?