Sunday, 6 February 2011

Mume Mzinzi lakini hataki kunipa Talaka, nifanyaje?

"Habari dada Dinah pole na majukumu, naomba mnisaidie niko njia panda, mimi niliolewa miaka mitatu ilipota histori fupi ya mimi na huyu mume dada Dinah ni hivi: Tulikuwa wapenzi toka tuko shule, baada ya kumaliza mwenzangu akapata kazi kwenye hotel kubwa tu hapa dar.

Wakati huo mie nikawa niko field Airport tukawa tunaishi pamoja kam amume na mke, visa vikaanzia hapo. Mwanaume akawa anapigiwa siku na wanawaka mara akanza kuwa anarudi nyumbani asubuhi. Ikafikia hatua ya kunifukuza pale na kuanza kubadilisha wanawake dada dinah.

Vitu vilivyoko pale nyumbani vingi tulishirikiana kama wapenzi kwakweli niliumia sana kwasababu nilikuwa nampenda. Basi tulitengana nikarudi kwetu na nikapata ajira baadaya Field. Baada ya miezi kama sita hivi akaja kunibembeleza huku akiniahidi hatarudia tene na amekuja kwa ajili ya kunioa.

Nilikubali dada, tukafunga ndoa na tukabahatika kupata mtoto wa kike, ndungu zangu wakanisaidia kunishughulikia tukapata nyumba ya NHC naye pia alitoa pesa zake ila hati zote ziliandikwa jina langu.

Kama ilivyokuwa kabla ya ndoa akaanza visa tena, sasa akawa ananitukana matusi makubwa mbele ya h/girl mpaka majirani wanasikia mara aniambie "wewe mwanamke gani mie sinimekusaidia tu kukuoa", mara anipige, anarudi Alfajiri akiwa amelewa.

Nimejaribu kumwambia nataka Talaka yangu hataki kunipa, sasa nilichoamua mwezi wa tatu sasa sitaki kabisa kushare nae love. Kinachonikera kwasasa ni kwanini hataki kunipa Talaka yangu aendelee kufanya mambo yake!

Naombeni mnishauri, nitaipataje Talaka yangu kutoka kwa huyu mume ili na mimi niwe huru?
Asanteni.