Wednesday, 17 August 2011

Nikisema sina hela ananuna, busu, kumbatio ni tatizo, nimbadilishe vipi?

"Hi da Dinah
Pole na hongera kwa kutoa elimu kwa vijana wa kitanzania. Mimi ni kijana wa miaka 23 na ni muajiliwa wa kampuni moja hapa Tanzania, tatizo langu ni kutopata mpenzi anayejali na kuthamini hisia zangu .

Natamani kuwa na mpenzi anayeendana na mitazayamo yangu ya kimaisha, kwa sasa ninae mpenzi lakini ni mtu anayependa pesa zaidi, siku ukimwambia huna basi atanuna na wakati mwingine anasema kuwa anahisi humpendi.

Na mbaya zaidi huwa hapendi kutoka na mimi ila marafiki zake its okay na hata hugs and kisses huwa kwake ni tatizo.Niini nifanye niweze kumbadilisha au niachane nae na kupata yule anayeendana na hisia nizitakazo? kwamba tupendane na tuendane kwenye masuala ya kimaisha?

Kwasababu wakati mwingine nahisi kuwa labda nina mkosi na sitokuja pata chaguo la moyo wangu nitakae mpenda na yeye anipende na sio kupenda pesa zangu."

11 comments:

Anonymous said...

Wewe kinaja mdogo sana umeanza kuteseka na kitu mapenzi hadi unaweweseka hapa?? Mbona unajitesa kihivyo dogo? wa nini mtu asiyejua umuhimu wako?

Kwa kuwa una kazi basi unaona umri huo ni wa kujishughulisha ka suluba za mapenzi vipi huna plan zingine za maisha? Kwa umri wako naamini hata digrii bado hujasma umebahatika kupata kazi mapema kwa nini usiendelee kusoma na kutumia pesa zako kujiendeleza kielimu kuliko kuhangaika na huyo binti asiykujali wala kukuthamini?

Mapenzi yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwapo.Watoto wa kike wazuri walikuwepo, wapo na wataendelea kuzaliwa kuwapo na kuwa wazuri zaidi, na kuja kumpata the real girl ipo kazi muhimu ni kujituliza mwenyewe huyo umtakaye atakuja kwa wakati.Watoto wa kike waliko duniani miaka hii wote wanastahili kuingia sokoni.Wamejimake up vilivyo, so why dealing with somene who doesn't care about you?

Usimnunue mwanamke kwa pesa utafilisika.Bali mnunue mwanamke kwa uzuri wa moyo wake na thamani yake ya utu.

Jenga maisha kwanza achana na mademu,you are still very young kuingia kwenye mapenzi ni kujitafutia magonjwa ya stress na pressure bure.

Anonymous said...

miaka 23 mbona mdogo sana, utakuwa unapata watoto wenzio ndo mana wanakusumbua, wasichana unaopata ni wa umri ambao bado wanapenda vitu kama hivyo na hawajawa tayari kusettle, hayo wanayotaka kwako au kuyafanya ndo vitu pekee vilivyopo kichwani mwao kwaajili ya utoto. So wala usiwaze mikosi mdogo wangu ni kawaida kama umri mlionao. Subiri ukue upate watu wazima wenzio wanaojua nini maana ya mahusiano

Anonymous said...

Ndugu yangu pole sana na hiyo dhahama unayokutana nayo, mie nadhani tumia busara tu kumuelewesha akuelewe kuwa tabia alokuwanayo hupendezewi, ukiona bado hakuelewi mwambie tu ukweli nadhani ni bora tuvunje huu uhusiano wetu, nimeshakutana na jambo kama lako hilo, nilipooona mwenzangu hanielewi nikamuambia kuwa nadhani kuna shida kati yetu tuachane kwa amani tu, yule binti alipata mtu mwingine lakini hadi leo hii ananikumbuka maana mie nilimpenda ila yeye alikuwa analeta mapozi, God be with you kaka, usikate tamaa Mungu atatkusaidia tu kwa hilo tatizo ulokuwa nalo

Anonymous said...

pole sana,achana nae hakupendi huyo.

Anonymous said...

mmmh hapo mapenzi hamna

Anonymous said...

Acha kulialia mwanaume mzima!! Unataka ununue penzi kwa pesa kwani mnafanya uchangudoa au mnajenga mahusiano? Mtupilie mbali wewe endelea na maisha mengine yenye maana.Unateseka bure wakati mabinti warembo wapo kedekede???

Anonymous said...

Ningekuwa mimi ningemkomesha kweli huyo.Siku ya kumvua chupi nahakikisha baada ya mchezo anashindwa hata kunyenyuka ili alipe fidia ya tamaa zake za pesa.

manyagag@gmail.com said...

kiukweli nawaelelewa sana na shukrani kwa mawazao yenu mazuri but you need to understand that love is magical feeling.age is not a issue when you real need to talk about love.labda nikueleweshe tu uliyesema uliyesema nirudi shule nafanya hivyo kwa sasa although love imekua part and parcel of my life.sipend kuwa player boy ndo maana nahitaji yule niliyenae nimfanye awe kama nitakavyo na huo mtazamo wa fikra zangu sijui kama mnaweza nishauri vingine.

Anonymous said...

unajua kaka yangu kumbadilisha mtu sio kazi ndogo. hapo labda umpende jinsi alivyo au uachane naye sababu huwezi kumbadisha mtu hata siku mmoja hata ukijitahidi vipi ataacha kwa muda lakini badaye atarudi tena hukohuko mimi mwenyewe yamenikuta nilikuwa najaribu kumfanya boyfriend wangu abadilike lakini kadri siku zinavyoenda naona hakuna mabadiliko yeyote nimechoka na nimeamua kuendelee na maisha yangu inaboa sana lakini sasa utafanya je.

Anonymous said...

u know wat guys age is just a number like 1+1,so i don't think if age is the big deal. na kuhusu huyo mpenzi wako honestly me sioni kama anakupenda she is just after money. love doesnt have conditions bwana.
Wish you luck buddy.
Liz

precious said...

huyo msichana hakupendi kaka,anapenda pesa zako tu wala usijali utapata mwanamke atakayekupenda kiukweli na sio kukupendea pesa....muombe mungu atakupa msichana wako bora tu uachane na huyo msichana wako cz anakupendea pesa..........utapata tu mtu atakayekupenda trust me